Kinana amejitahidi sana kufafanua hili suala la maridhiano na pia kuhusu Katiba. Pia kaweza kuilinganisha Serikali ya CCM na nchi nyingine jirani, hususan za Commonwealth. Binafsi sina chama bado ingawa nilikuwa TANU na Youth League. Maoni/maswali yangu ni yafuatayo:
1.Suala la uhuru wa Mahakama lazima lishughulikiwe kama Tume huru ya uchaguzi linavyotafutiwa ufumbuzi. Vingenevyo hizo Kamati za Usaili zinazompelekea Rais mapendekezo kama anajivunia Mahakama hii kuhusishwa litakuwa igizo lingine.
2. Ameshasema Bunge la 2020 halikuwa halali, sasa anategemea vipi kuwa utendaji wa Bunge hili na Kamati zake uaminiwe na wananchi.
3.Baadhi ya nchi anazotolea mfano taasisi za kumshauri Rais zina utaratibu wa kuteuliwa shirikishi kuliko hapa petu kwa hiyo hakuna ulinganifu.
4. Kama Chadema hawakuuliza, je, CCM imeafiki kuwa roho za wananchi wake hazina thamani tena? Haya maridhiano hayana ukurasa wa watu waliopotezwa wakiwa mikononi mwa Serikali? Mbona CCM hamwuigi maridhiano ya nchi nyingine?
5. Serikali, hasa kupitia kwa Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM, inapovunja sheria za nchi ambapo yenyewe ndiyo yenye jukumu la kuzisimamia inakuweje? Udhu wake unarejeshwaje?