Kinana awataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Kinana awataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Kinana amewataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Hii itasaidia wananchi kuelewa ujumbe wanaopewa nyakati za kuielezea Ilani ya CCM na utekelezaji wake

Source TBC
 
Jukwaa ndio mahali sahihi kwa mwanasiasa

Mwanasiasa asiejua jukwaa sio mwanasiasa huyo
 
Chama kinachotegemea vyombo vya dola wanachama wake wataweza vipi kujenga hoja majukwaani. Wao wanajua vyombo vya dola vipo vitasimamia wao kupata madaraka. Hata wanaoongea majukwaani wengi wao huongea sio kwa ushawishi, bali ni kwa jeuri ya chama kuwa madarakani.
 
Utawajua vizuri 2025
 
UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Wenzetu wa UVCCM kazi yao kuchochea polisi wazime kazi nzuri ya siasa za ushawishi za BAVICHA, vijana wa chama-dola CCM hawana uwezo wa kujenga hoja katika jukwaa lolote liwe la madhabau ya mbao la vyuo vya elimu ya juu wala mitaani au dijitali
 
Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Kinana amewataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Hii itasaidia wananchi kuelewa ujumbe wanaopewa nyakati za kuielezea Ilani ya CCM na utekelezaji wake

Source TBC
UVCCM inaVIJANA wasio na UWEZO wa KUJENGA HOJA zaidi ya VITISHO na MATUSI hebu Msikilize Huyu Alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Enzi ya Mzee KATILI Mwendazake
 
Chama kinachotegemea vyombo vya dola wanachama wake wataweza vipi kujenga hoja majukwaani. Wao wanajua vyombo vya dola vipo vitasimamia wao kupata madaraka. Hata wanaoongea majukwaani wengi wao huongea sio kwa ushawishi, bali ni kwa jeuri ya chama kuwa madarakani.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] sasa wazee ndiyo wamekalia viti vijana watapata wapi, badala vibabu viwe vishauri lakini kila siku kwenye magari [emoji48][emoji48][emoji48]
 
Wenzetu wa UVCCM kazi yao kuchochea polisi wazime kazi nzuri ya siasa za ushawishi za BAVICHA, vijana wa chama-dola CCM hawana uwezo wa kujenga hoja katika jukwaa lolote liwe la madhabau ya mbao la vyuo vya elimu ya juu wala mitaani au dijitali

Lindi, Tanzania

Serikali ya CCM .wajaribu kuzuia shughuli za kukuza chama cha CHADEMA

Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Kinana amewataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Hii itasaidia wananchi kuelewa ujumbe wanaopewa nyakati za kuielezea Ilani ya CCM na utekelezaji wake

Source TBC
Hivi siku hizi chama kina ilani tu hakina itikadi?

Utasikia mama kateremsha mapesa, hela zenyewe mikopo toka nje😂.

Suala la kujitegemea na haki na usawa halizungumzwi tena. Chama kimejaa wapigaji ndio viongozi wanaoweza kuchaguliwa awamu hii.
 
CHADEMA YAWATOA HOFU WANA-CCM WENYE UZALENDO WA KWELI

Tutashusha madaraka yawe mikoani / majimbo ili Masuala kama ya visima vya maji, matundu ya vyoo shuleni n.k yasiwe yanapoteza muda wa kikao cha bunge Dodoma ... bali wananchi majimbo / mikoani watakuwa wanawabana magavana waliowachagua wakamilishe miradi hiyo midogo huku huku chini mikoani na akishindwa basi gavana huyo wananchi wataweza kumtimua ...
 
Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Kinana amewataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Hii itasaidia wananchi kuelewa ujumbe wanaopewa nyakati za kuielezea Ilani ya CCM na utekelezaji wake

Source TBC
Mi nadhan angewashauri wawe waadilifu na uzalendo ili wanapopewa nafasi za uongozi kama Ma-DEDs na DCs (kama ilivyo ada) wasifuje Mali za Umma na kuleta tija katika maeneo yao ya Kazi. Wakishafanya hivyo nadhan watanzania walio wengi hawatajali kama wanajua kuongea sana/vizuri majukwaani au la. Ilani ikifanyika site huna haja ya kuisemea jukwaani... wananchi tutaiona ilivyofanyika na tutakupeni Ridhaa ya kuongoza Bila kutupa kanga,ubwabwa na kofia.
 
Mtama, Lindi
Tanzania

Kiongozi azungumzia jinsi nyumba yake ilivyozingirwa usiku kucha, lakini pamoja na hilo Aluta Continua Mapambano Yanaendelea

Mtama yawapa pole ujumbe wa viongozi kutoka makao ya chama taifa CHADEMA ...... Mtama waelezea jinsi Lindi ilivyojaa askari polisi ili wananchi wasitayarishe mkutano wa ndani na viongozi wa CHADEMA taifa kutoka makao makuu Dar es Salaam ..
 
Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Kinana amewataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Hii itasaidia wananchi kuelewa ujumbe wanaopewa nyakati za kuielezea Ilani ya CCM na utekelezaji wake

Source TBC
Awafunde vijana wake mana wengi ni weupe na hawana uwezo wa kujenga na kupanguwa hoja.
 
Lindi, Tanzania

SPIKA ZA MKUTANO WA NDANI WA CHADEMA KANDA YA KUSINI, ZAWAKERA MAMLAKA

Mamlaka za serikali kupitia OCD wa polisi yadai spika zinasumbua majirani .... katiba au sheria inavunjwa wapi Public Address system na mic zikitumika mkutano ... OCD Polisi aelemishwa asiburuzwe ....
 
Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Kinana amewataka UVCCM wajijengee uwezo wa kuongea Majukwaani

Hii itasaidia wananchi kuelewa ujumbe wanaopewa nyakati za kuielezea Ilani ya CCM na utekelezaji wake

Source TBC
uvccm yamekua midebwedo kaz yaliyobaki nayo ni kusifu upumbavu na kugombania rushwa.
 
1669630700145.png

Kikwete - CCM msitegemee polisi​

“Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao…au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,”alisema Kikwete na kuongeza:

RAIS Jakaya Kikwete juzi aliwaonya wanachama wa CCM akiwataka waache kubweteka kwa kuwategemea askari polisi katika masuala ya kisiasa, kwani kufanya hivyo watakuwa wanajidanganya.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM uliofanyika kwa siku tatu mfululizo katika Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema kitendo cha wanaCCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la Polisi hakipaswi kukubaliwa kwani kimepitwa na wakati.

“Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao…au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,”alisema Kikwete na kuongeza:

“Sasa mnataka wakisema Serikali ya CCM haijafanya kitu polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, polisi wakawakamate? Kama wakisema hatujafanya kitu ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine.”

Licha ya kwamba hakuwataja moja kwa moja, kauli za Rais Kikwete zilikuwa zikielekezwa kwa uogozi wa Chadema ambao kimsingi kinaonekana kuwaumiza vichwa CCM.

Huku akirudia mara kadhaa maneno hayo alisema, “Nataka mfahamu ndugu zangu kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli.”

Kikwete aliwatuhumu viongozi wa upinzani kwamba ni waongo na kwamba wakati mwingine wamekuwa wakizusha mambo ambayo hayapo, huku wakijifanya kuwa na ushahidi wa kimaandishi.

Alimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwamba kuna wakati aliwahi kuzusha kwamba yeye (Kikwete), na makada kadhaa wa chama hicho wakiwamo Rostam Aziz walikuwa jijini Mwanza usiku, wakati si kweli kwani siku waliyodai alikuwa Nachingwea mkoani Lindi kwenye mikutano ya kampeni za urais.

Katika mazingira hayo, aliwataka wanaCCM kila mahali kujibu hoja za wapinzani kwa kauli na vitendo na wasikubali kuburutwa kwani uongo ukiachwa kwa muda mrefu unageuka kuwa ni ukweli.

Aliwaeleza kuwa ukimya wao katika kujibu hoja za wapinzani ni sumu kwao na kwamba wenzao wameanza kuaminika zaidi yao licha ya kuwa CCM ndio wenye majibu yote.

“Mkijibu kwa hoja wanatulia, sio Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani,” alisisitiza Kikwete.

Mbali na hilo aliwaonya kuacha malumbano ya mara kwa mara akieleza kuwa hali hiyo inakibomoa chama.

Alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakitumia muda mwingi kukosoana wao kwa wao, huku wakitoa nafasi kwa adui zao.

Mwenyekiti huyo alisema hakuna mtu kutoka nje ya chama anayeweza kukidhoofisha CCM kwa hoja isipokuwa chama hicho kinaumizwa na wanachama wake ambao wamekuwa wakilumbana bila sababu.

Akizungumzia suala la wagombea urais aliwataka wanachama wenye nia kufuata taratibu zote za chama pamoja na kuvumiliana ili ifikapo Mei 2015, mkutano utafanya uamuzi wa nani anasimama kupeperusha bendera ya chama hicho.

“Kwa wale mnaotaka kugombea, andikeni hiyo tarehe tutakuja hapa kuteua, lakini msituvuruge lazima mfuate utaratibu. Utaratibu huo utatangazwa, maana mkianza kupita huko na huko ndiko tunakopata matatizo,” alisema Kikwete.

Kikwete juzi alichaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata asilimia 99.92 ya kura zilizopigwa, huku kura mbili zikimkataa. Kadhalika mkutano huo uliwachagua Dk Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania – Zanzibar) na Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara).
 
RAIS Jakaya Kikwete juzi aliwaonya wanachama wa CCM akiwataka waache kubweteka kwa kuwategemea askari polisi katika masuala ya kisiasa, kwani kufanya hivyo watakuwa wanajidanganya.
Yuda Iscariot at his best
 
Back
Top Bottom