Kinana: Msilaghaike na kikundi cha wasaka madaraka kwa mgongo wa hoja ya serikali tatu.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,266
Hii ni sehemu ya hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM, kinana katika viwanja vya Gombani ya Kale, Pemba.

[video=youtube_share;gSl5Pl-1Eh4]http://youtu.be/gSl5Pl-1Eh4[/video]

SIKU moja baada ya viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuondoka Pemba, wakidai kuelezea sababu za wao kususa Bunge Maalumu la Katiba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Watanzania kutoamini hadaa za watu wasioitakia mema Tanzania.

Chama hicho kimesema watu hao watengeneza chokochoko kupitia kigezo cha mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya, na kusema Katiba hiyo si mwarobaini wa matatizo yaliyopo sasa hapa nchini.

Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana, aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale visiwani hapa jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 2 katika visiwa vya Unguja na Pemba kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010/2015 na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Katika mkutano huo alizungumzia matukio yanayoendelea kutokea nchini, hasa upotoshaji unaoendelea hivi sasa, ambapo aliwatoa hofu watanzania kuwa, hayazuii kupatikana kwa Katiba hiyo.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya nchi duniani ambazo zina Katiba bora sana kama vile Afrika Kusini na Namibia lakini katiba hizo hazijasaidia kuboresha maisha ya wananchi wake, kwa kuwa utekelezaji wa kuboresha maisha ya wananchi unakwenda hatua kwa hatua.

Alisema kinachoendelea kwa sasa bungeni ni wazi kuwa baadhi ya watu kutoka vyama vya upinzani akili zao zimejikita katika uroho wa madaraka na ndio maana wanang’ang’ania mfumo wa Serikali tatu wakiwa na imani kuwa huenda zikipatikana wataongeza nafasi ya kupata madaraka.

Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Ukawa ni kikundi cha wachumia tumbo ambacho kinategemea fedha za wasioitakia mema Tanzania kuvuruga amani iliyopo.

Alisema Ukawa ni genge la wataka madaraka na kwamba hiyo ni janja ya baadhi ya wanakikundi hicho ambao ni Chadema ambao wanawaburuza wanasiasa uchwara wasiojitambua.

Nape alisisitiza kuwa huu si wakati wa kupigizana kelele na watu wanaoungana bila kuwa na malengo mahususi, badala yake aliwaambia wananchi kuwakataa kwani hawana nia ya kuungana kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi, badala yake ni kwa malengo ya kuboresha maisha yao wenyewe na watoto wao.

Aliwataka Chadema akiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kujibu kwanini hakuwaingiza wapinzani wenzake katika Baraza Kivuli la Mawaziri? Kama sio ujanja wa kuwahadaa wenzake baada ya kugundua kuwa wanapenda vyeo vya dezo.

Chadema, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 iliingia bungeni na kuunda Kambi ya Upinzani bila kushirikisha vyama vingine kikiwemo CUF chenye wabunge wengi.

NCCR –Mageuzi, TLP vyenye wabunge, navyo viliwekwa kando. Lakini katika Bunge Maalumu la Katiba, vyama vingine viliingiwa katika `uswahiba’ na Chadema na kuunda Ukawa kwa lengo la kuongeza nguvu ya ushawishi dhidi ya CCM chenye wabunge wengi, ikiaminika kuwa kwa wingi wao wangewaburuza wengine katika maamuzi.

Katikati ya wiki, viongozi wa Ukawa wakiwa katika mkutano wa hadharani mjini Pemba, Mbowe alikaririwa akisema anakusudia kuvunja baraza la mawaziri kivuli ndani ya Bunge.
Chanzo:Habarileo.
 
Kupitia Bunge la Katiba, wananchi wapenda Taifa endelevu wanazidi kubainishiwa ukweli ulioko ndani ya mioyo na fikra za baadhi ya viongozi kupitia kundi la vyama vya siasa wanaojiita kwa sasa UKAWA.

Waingereza wanasema, Birds of a feather flock together kwa maana kuwa, kwa sasa Bunge la Katiba limewakutanisha vinara wa ubaguzi na wasaka madaraka kwa njia zozote zile kuanzia viongozi wa vyama ambao baadhi yao wamekuwa katika uongozi wa juu wa vyama vya siasa kuanzia mwaka 1995 huku wengine wakijaribu kuwaomba wananchi wawaamini na kuwapa ofisi kuu nchini kupitia kura za Urais (Rais wa Tanzania) lakini hawakufanikiwa kwa vile kile ambacho wananchi walikuwa wana wasiwasi nacho kuhusiana na fikra na mitazamo yao kama viongozi wakuu imeanza kudhirika katika bunge Maalum.

Ubaguzi wao umezaliwa ndani ya vyama vyao, ukamea na kuimarika huku baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi ndani ya vyama wakiishia kuwa ni wahanga wa ubaguzi huo. Wengine walifukuzwa na huku wengine wakinyang'anywa madaraka. Kwa sasa ubaguzi unatafuta njia nyingine ya kujipandikiza kitaifa kupitia mchakato wa katiba baada ya kutamalaki ndani ya vyama vyao ili waendeleze nia yao ya kusaka madaraka kwa gharama zozote.

Pamoja na baadhi ya viongozi wa UKAWA kupewa pesa kutoka nje kwa ajiri ya mradi wa kusaka madaraka. Dhambi ya ubaguzi itawatafuna wao wenyewe na katika dhambi hiyo, hawawezi kufanikiwa kupata kile wanachokitaka kwa nguvu zote. Huwezi kutenda dhambi mbaya kama hii halafu usalimike.

Huwezi kufanya ubaguzi na siasa za matukio halafu ufanikiwe. Siyo muda mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao.
 
...hatutahadaika na majangili na mafisadi yanayolinda madaraka yao kwa nguvu zote hata kuua watu ilimradi tu walinde maslahi yao kwa kukandamiza demokrasia,haki na uhuru wetu....
 
Ndugu, Kama CCM ingekuwa inahadaa wananchi basi isingepata fursa kutoka kwa wananchi hao hao kuiongoza nchii tokea uwanja wa siasa za vyama vingi uanzishwe kikatiba.
 
Kupitia Bunge la Katiba, wananchi wapenda Taifa endelevu wanazidi kubainishiwa ukweli ulioko ndani ya mioyo na fikra za baadhi ya viongozi kupitia kundi la vyama vya siasa wanaojiita kwa sasa UKAWA.

Waingereza wanasema, Birds of a feather flock together kwa maana kuwa, kwa sasa Bunge la Katiba limewakutanisha vinara wa ubaguzi na wasaka madaraka kwa njia zozote zile kuanzia viongozi wa vyama ambao baadhi yao wamekuwa katika uongozi wa juu wa vyama vya siasa kuanzia mwaka 1995 huku wengine wakijaribu kuwaomba wananchi wawaamini na kuwapa ofisi kuu nchini kupitia kura za Urais (Rais wa Tanzania) lakini hawakufanikiwa kwa vile kile ambacho wananchi walikuwa wana wasiwasi nacho kuhusiana na fikra na mitazamo yao kama viongozi wakuu imeanza kudhirika katika bunge Maalum.

Ubaguzi wao umezaliwa ndani ya vyama vyao, ukamea na kuimarika huku baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi ndani ya vyama wakiishia kuwa ni wahanga wa ubaguzi huo. Wengine walifukuzwa na huku wengine wakinyang'anywa madaraka. Kwa sasa ubaguzi unatafuta njia nyingine ya kujipandikiza kitaifa kupitia mchakato wa katiba baada ya kutamalaki ndani ya vyama vyao ili waendeleze nia yao ya kusaka madaraka kwa gharama zozote.

Pamoja na baadhi ya viongozi wa UKAWA kupewa pesa kutoka nje kwa ajiri ya mradi wa kusaka madaraka. Dhambi ya ubaguzi itawatafuna wao wenyewe na katika dhambi hiyo, hawawezi kufanikiwa kupata kile wanachokitaka kwa nguvu zote. Huwezi kutenda dhambi mbaya kama hii halafu usalimike.

Huwezi kufanya ubaguzi na siasa za matukio halafu ufanikiwe. Siyo muda mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao.

Toa huu uchafu hapa. Hivi serikali tatu ni hoja ya vyama vya upinzani au wananchi? Wachumia tumbo wakubwa nyie.
 
Mzee utachomwa moto sana..unaitangaza ccm kwa nguvu sana hulali..lakini unatangaza zimwi linalo nyonya na kumaliza watanzania

Mkuu naomba unielimishe tafadhali: Hivi UKAWA ni Chama, NGO, SACCOS au kitu gani?
 
MwanaDiwani Nilikuuliza wagombea madaraka ni wepi waliopo madarakani miaka 50yrs
au wanaotaka kuondoa uozo huu???
Mdude Chadema Nyagali > Sauti ya Tanganyika DENI LA TAIFA KUTOKA TRION 27 MWAKA JANA MPAKA TRION 40.6
KWA NINI DENI LA TAIFA LINAONGEZEKA WAKATI MATUMIZI NI YALE YALE?
1.MISHAHARA KWA WATUMISHI NI ILE ILE
2.BARABARA NI ZILEZILE.
3.HOSPITAL NI ZILEZILE NA BADO HAZINA MADAWA
4 KAMA NI KATIBA TOKA MCHAKATO UANZE KWA JAJI WARIOBA MPAKA BUNGE LA KATIBA NI BILON 82 TU NDO ZILIZOTUMIKA.

HUENDA MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI NDIYO YANAYOSABABISHA DENI HILI KUWA KUBWA EBU TUANGALIE MATUMIZI KWENYE OFISI LA RAIS USUSANI SAFARI ZA NJE .

1.Rais kama anasafiri nje ya nchi huongozana na maafisa wasiopungua 22 wakiwamo afisa usalama madoctor n.k.

2.mjumbe ama afisa yoyote anayekuwa kwenye msafara wa rais analipwa 600000/= laki sita kwa siku sasa unapaswa kuzidisha pesa hiyo kwa wajumbe wote 22 ambapo utapata milion 13200000/=milion kumi na tatu laki mbili kwa siku.

3.mjumbe ama afisa anayekuwa kwenye msafara wa rais analala HOTEL yenye thamani ya DOLA 1200 ambayo sawa na 1900000/= milion moja na laki 9 pesa hiyo uizidishe mara wajumbe 22 unapata 41800000/= milion arobaini na moja na laki nane kwa siku moja

4.hivyo basi ukijumlisha posho na malazi ya maafisa ama wajumbe kwenye msafara wa rais unapata shilingi 55000000/=milioni hamsini na tano kwa siku moja.

jumla ya safari za rais nje ya nchi ni 395 ukizidisha 395 mara shilingi milion 55 utapata hesabu kamili ya matumizi ya safari zote za rais nje ya nchi kwa maana calculator yangu imenock kwa kulingana na ukubwa wa hesabu.

5.bado usafiri ndege ya rais iliruka angani kwa muda wa saa moja hutumia milion 16.2
bado matumizi mengine kwenye ofisi ya rais kama vile safari za ndani n.k

6.baraza la mawaziri ;waziri mmoja hutengewa mafuta lita 200 ambazo sawa na laki nne 400000/= kwa siku ata kama anakoenda hakujulikani na hakuna faida kwa serikali na kuna mawaziri 60 ukizidisha idadi ya mawaziri hao mara laki 4 unapata 24000000/=milion ishilini na nne kwa siku moja

SASA NDUGU ZANGU KWA MATUMIZI HAYA KWA NINI TAIFA LISIPATE DENI KUBWA?
KWA NINI WATANZANIA MNAENDELEA KUKUMBATIA CCM KWA MATUMIZI MABAYA KAMA HAYA WAKATI HUO KUNA SHULE HAZINA MADARASA?

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Bado tuu unatetea wezi, mafisadi na rushwa Mikataba mibovu ya siri???
 
Last edited by a moderator:
Toa huu uchafu hapa. Hivi serikali tatu ni hoja ya vyama vya upinzani au wananchi? Wachumia tumbo wakubwa nyie.

Wananchi hawana haja na idadi ya Serikali, ndio maana hata Warioba mwenyewe alionesha kuwa zaidi ya 80% hawakuzungumzia kabisa juu ya muundo wa muungano kwa kuwa hawakuwa na tatizo nao!
Wewe fikiria tukianza kuwa na passport na visa ili kuingia Zanzibar au Tanzania Bara warakaoathirika si viongozi ni wananchi wa kawaida na haiingii akilini eti wananchi walio wengi wakubali hoja dhaifu za kuwagawa!
Wewe waangalie wana-UKAWA wanachopigania ni mambo ya utawala (madaraka) na si mambo ya maendeleo ambayo ndio shida hasa ya wananchi!
 
Kupitia Bunge la Katiba, wananchi wapenda Taifa endelevu wanazidi kubainishiwa ukweli ulioko ndani ya mioyo na fikra za baadhi ya viongozi kupitia kundi la vyama vya siasa wanaojiita kwa sasa UKAWA.

Waingereza wanasema, Birds of a feather flock together kwa maana kuwa, kwa sasa Bunge la Katiba limewakutanisha vinara wa ubaguzi na wasaka madaraka kwa njia zozote zile kuanzia viongozi wa vyama ambao baadhi yao wamekuwa katika uongozi wa juu wa vyama vya siasa kuanzia mwaka 1995 huku wengine wakijaribu kuwaomba wananchi wawaamini na kuwapa ofisi kuu nchini kupitia kura za Urais (Rais wa Tanzania) lakini hawakufanikiwa kwa vile kile ambacho wananchi walikuwa wana wasiwasi nacho kuhusiana na fikra na mitazamo yao kama viongozi wakuu imeanza kudhirika katika bunge Maalum.

Ubaguzi wao umezaliwa ndani ya vyama vyao, ukamea na kuimarika huku baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi ndani ya vyama wakiishia kuwa ni wahanga wa ubaguzi huo. Wengine walifukuzwa na huku wengine wakinyang'anywa madaraka. Kwa sasa ubaguzi unatafuta njia nyingine ya kujipandikiza kitaifa kupitia mchakato wa katiba baada ya kutamalaki ndani ya vyama vyao ili waendeleze nia yao ya kusaka madaraka kwa gharama zozote.

Pamoja na baadhi ya viongozi wa UKAWA kupewa pesa kutoka nje kwa ajiri ya mradi wa kusaka madaraka. Dhambi ya ubaguzi itawatafuna wao wenyewe na katika dhambi hiyo, hawawezi kufanikiwa kupata kile wanachokitaka kwa nguvu zote. Huwezi kutenda dhambi mbaya kama hii halafu usalimike.

Huwezi kufanya ubaguzi na siasa za matukio halafu ufanikiwe. Siyo muda mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao.
Nani kabaguliwa zaidi ya ile ya Lukuvi aliyosemea kanisani wasuruhusu uislam zanzibar?unaandika uharo tuu hapa.Kama ni serikali 2 kwa nini msirekebishe katiba iliyopo na mboreshe muungano kama mnavyotaka?kulikua na haja gani kuunda kuunda tume na kuiita katiba mpya wakati bado mnafikra za kizamani?
 
Toa huu uchafu hapa. Hivi serikali tatu ni hoja ya vyama vya upinzani au wananchi? Wachumia tumbo wakubwa nyie.
Ndugu, Kwani wewe unachumia mdomo?.

Walaghai wote wanatumia midomo katika ulaghai wao.

Unachokiona ni uchafu kwa binadamu wengine ni usafi lakini vile vile unakiona wewe ni usafi kwa binadamu wengine pia wanakiona ni uchafu.

Wewe uliyeukuta huu uchafu ndiyo unatakiwa uondoke!.
 
Wananchi hawana haja na idadi ya Serikali, ndio maana hata Warioba mwenyewe alionesha kuwa zaidi ya 80% hawakuzungumzia kabisa juu ya muundo wa muungano kwa kuwa hawakuwa na tatizo nao!
Wewe fikiria tukianza kuwa na passport na visa ili kuingia Zanzibar au Tanzania Bara warakaoathirika si viongozi ni wananchi wa kawaida na haiingii akilini eti wananchi walio wengi wakubali hoja dhaifu za kuwagawa!
Wewe waangalie wana-UKAWA wanachopigania ni mambo ya utawala (madaraka) na si mambo ya maendeleo ambayo ndio shida hasa ya wananchi!
Wewe unayepigania mambo ya nchi mbona umemuacha kada mwenzako IDD SIMBA kauza UDA na pesa kaweka mfukoni kwake hujasema kitu?Nchi za malaysia singapore thailand korea indonesia walikubali kubadilika ndiyo maana wakaendelea nyie ma INTARAHAMWE hambadiliki
 
Hahaaaahaa

Kila ukianzisha uzi wako wa propaganda huwa unaweka picha, vp pemba kamera ziligoma?

Hahaaa mtakufa kwa vihoro mwaka huu, Serikali tatu ni lazima sio ombi wala hisani.
 
Buchanan's kwani sasa huoni unaishi kwenye Serikali tatu??
Mambo ya muungano yanashughulikiwa na mafisadi wa CCM, hiyo ni Serikali, mambo ya TZ bara hiyo ni Serikali na Serikali ya wazi ya Zanzibari, kilichobaki kuzindua Serikali ya Tanganyika, ambayo ipo inaitwa TZ bara!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naomba unielimishe tafadhali: Hivi UKAWA ni Chama, NGO, SACCOS au kitu gani?
Ni umoja wa wazalendo wa nchi ya tanzania kwa ajili ya kutetea na kuleta katiba mpya na mabadiliko ambayo yatamkwamua mtanzania kwenye lindi la umaskini wa kutisha.. ambao probably huo umaskini haujui ma hauluumizi mtu kama wewe
 
Wananchi hawana haja na idadi ya Serikali, ndio maana hata Warioba mwenyewe alionesha kuwa zaidi ya 80% hawakuzungumzia kabisa juu ya muundo wa muungano kwa kuwa hawakuwa na tatizo nao!
Wewe fikiria tukianza kuwa na passport na visa ili kuingia Zanzibar au Tanzania Bara warakaoathirika si viongozi ni wananchi wa kawaida na haiingii akilini eti wananchi walio wengi wakubali hoja dhaifu za kuwagawa!
Wewe waangalie wana-UKAWA wanachopigania ni mambo ya utawala (madaraka) na si mambo ya maendeleo ambayo ndio shida hasa ya wananchi!

Wewe unaongea nini na upo nchi gani? Inamaana kweli hujui taratibu za kuingia Zanzibar kuwa sharti uwe na kitambulisho? Ninyi maInterahamwe fuatilie mambo kwa undani.
 
Uhusiano kati ya CCM na wananchi hauna tofauti kati ya ule wa mbu na wanadamu. Mbu akija kwako atakunyonya damu na na wakati mwingine hukuachia magonjwa. Hivi dawa ya mbu ccm ni nini jamani? Maana hata tukitumia net yeye anaanza na sisi sebuleni.
Halafu jamaa anasifu mbu hawa wanaotunyonya hivi jamani. Hata haya hana. Looo!!!!!!!
 
CCM jalini maoni ya wananchi waliyo wengi na si akina komba pale Dodoma waliyopotoka. Ni aibu mtu mzima unakuwa na akili kama za kuku(CCM).
 
Back
Top Bottom