kupitia bunge la katiba, wananchi wapenda taifa endelevu wanazidi kubainishiwa ukweli ulioko ndani ya mioyo na fikra za baadhi ya viongozi kupitia kundi la vyama vya siasa wanaojiita kwa sasa ukawa.
Waingereza wanasema, birds of a feather flock together kwa maana kuwa, kwa sasa bunge la katiba limewakutanisha vinara wa ubaguzi na wasaka madaraka kwa njia zozote zile kuanzia viongozi wa vyama ambao baadhi yao wamekuwa katika uongozi wa juu wa vyama vya siasa kuanzia mwaka 1995 huku wengine wakijaribu kuwaomba wananchi wawaamini na kuwapa ofisi kuu nchini kupitia kura za urais (rais wa tanzania) lakini hawakufanikiwa kwa vile kile ambacho wananchi walikuwa wana wasiwasi nacho kuhusiana na fikra na mitazamo yao kama viongozi wakuu imeanza kudhirika katika bunge maalum.
Ubaguzi wao umezaliwa ndani ya vyama vyao, ukamea na kuimarika huku baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi ndani ya vyama wakiishia kuwa ni wahanga wa ubaguzi huo. Wengine walifukuzwa na huku wengine wakinyang'anywa madaraka. Kwa sasa ubaguzi unatafuta njia nyingine ya kujipandikiza kitaifa kupitia mchakato wa katiba baada ya kutamalaki ndani ya vyama vyao ili waendeleze nia yao ya kusaka madaraka kwa gharama zozote.
Pamoja na baadhi ya viongozi wa ukawa kupewa pesa kutoka nje kwa ajiri ya mradi wa kusaka madaraka. Dhambi ya ubaguzi itawatafuna wao wenyewe na katika dhambi hiyo, hawawezi kufanikiwa kupata kile wanachokitaka kwa nguvu zote. Huwezi kutenda dhambi mbaya kama hii halafu usalimike.
Huwezi kufanya ubaguzi na siasa za matukio halafu ufanikiwe. Siyo muda mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao.