Kinana: Serikali iwachukulie hatua waliotajwa Ripoti za CAG

Kinana: Serikali iwachukulie hatua waliotajwa Ripoti za CAG

njaa mbaya

kwa mara ya kwanza Dr.Slaa anamsifu Jakaya Kikwete

anasema kuna kipindi alimpiga kashfa na tuhuma nzito nzito sana Jakaya halafu asubuhi yake Jakaya akashiriki kwny Fund rising ya Taasisi aliyokuwa anaisimamia Dr Slaa…japo hakuitaja lakin alikuwa anamaanisha CCBRT
Slaa ni mnafiki mkubwa

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema ni wakati wa Serikali kuchukua hatua dhidi ya watu waliokutwa wameenda kinyume na maadili katika Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Amesema, "CAG hazushi, anafanya kazi zake kitaaluma. Katika Ripoti zake anaeleza kasoro nyingi na mambo yasiyofaa ambayo yamefanyika ikiwemo upotevu wa Fedha za Umma na matumizi mabaya"

Amesema Vyombo husika vya Serikali vina wajibu wa kuchukua hatua ili Fedha za Wananchi zisichezewe
Samia anapita mle mle kwa JK, kutumia siasa za utendaji haki kwa wanaokuwa chini yake. Kwamba CAG anaposema fulani na fulani ni wachafu na wametuibia pesa nyingi, anakuja KInana kama makamu mwenyekiti na kutoa agizo la kuwashughulikia wezi wote.

Hivyo amri ya SSH itakayokuja haitakuwa na misingi ya uonevu, Kinana anaagiza kwa misingi ya report ya CAG, Maagizo ya SSH yanatokana na vyombo viwili vya chini yake.

Anakwepa kutumia mno nguvu zake zilizo ndani ya katiba, hapendi kuogopwa na mamlaka zilizo chini yake.
 
Tuanze na hawa hapa:
1650738463682.jpg
 
Ukipanda bus la Mzee Mtei na umbeba magendo inamhusuje mwenye bus. Ukipakia mizigo kwenye treni ikashikwa na kugunduliwa pembe za tembo jee shirika la reli na serekali yenye mali wanahusika na hizo nyara? Tuwache unyumbu

Kumbe kupakia mizigo for export trade kwenye meli taratibu zake ni sawa na kupakia tungule hapo kwa wakwe zako Ilula Iringa.
 
Comrade alipofika umri wa miaka 60 plus alikuwa kachoka sana akaomba apumzike baada ya kutumikia nchi kwa miaka mingi

alipofikisha miaka 70 plus mchoko umeisha karudi ulingoni

mwansiasa mtu hatare sana
Hivi zamu yako inaisha lini kule chattle
 
Hii ni kwa makusudi kabisa.
Mods tafadhalini msiende kuunganisha huu uzi na zile za mwaka huu.
 
CAG hazushi, anafanya kazi zake kitaaluma. Katika Ripoti zake anaeleza kasoro nyingi na mambo yasiyofaa ambayo yamefanyika ikiwemo upotevu wa Fedha za Umma na matumizi mabaya"

Vyombo husika vya Serikali vina wajibu wa kuchukua hatua ili Fedha za Wananchi zisichezewe

Wakiamua iwe hv msumeno uwe kwa kila mtu sio kwingine unapindia pembeni

Hivi Serikali itawachukulia hatua bila bunge kuipitia na kuwahoji kwa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali?

Hayao mambo anayasema kwa kuwahadaa wana nchi ila yakigusa washirika hutamsikia tena.

Hata hivyo ni danganya toto ili ionekane kaja na jipya ila baada ya hapo hawezi kuleta mrejesho.

Ushahidi unao ?!!!

Je makosa ya jana yarejewe kesho ?!!!

Kama ni kweli watafutwe. Washugulikiwe ipasavyo wafikishwe Mahakamani-na tusije sikia walibambikizana-na kushitakiwa. Zaidi ya hapo ni porojo za nenda rudi na siasa za vita za ndani ya chama, vita za kitamaduni za ndani ya Chama cha kisiasa cha CCM.

Safi sana.
kwa kuwa ripoti ya CAG imebaini baadhi ya maeneo kuwa na ubadhirifu wa fedha za umma tena kizembe basi wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria sio kuachishwa tu bali wafikishwe mahakamani
 
Tangu alipotamka ni wangapi wamechukuliwa hatua ?
Wakichukuliwa hatua tunawashupalia Viongozi na kuwaita madikteta, makatili n.k Tumefikia hata kuanza kudai mahakama za ufisadi hazifai?

Hatuna misimamo thabiti, ila hila tu na tunabeba visasi binafsi kwenye siasa za Nchi
 
Hivi huyu hajawahi kutajwa kwenye tuhuma zozote ? Alichukuliwa Hatua ?

Naomba tufuate ushauri wake ipasavyo... ila sio CAG tu bale tuhuma zozote zichunguzwe na mwisho wa siku haki itendeke
Toa hizo tuhuma na ushahidi kama ripoti hii ilimtaja Kinana,sio unaleta pumba za yule mpuuzi hata jina nimelisahau
 
Haya maneno ya Makamu wa Mwenye Kiti wa CCM, yawe yanatoka kwenye moyo wake,yasiwe maneno ya kisiasa,kuwazuga na kuwatuliza Watanzania.
 
Shida wote wanajuana, kinana hana moral authority ya kukemea hao wanaoiba pesa
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema ni wakati wa Serikali kuchukua hatua dhidi ya watu waliokutwa wameenda kinyume na maadili katika Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Amesema, "CAG hazushi, anafanya kazi zake kitaaluma. Katika Ripoti zake anaeleza kasoro nyingi na mambo yasiyofaa ambayo yamefanyika ikiwemo upotevu wa Fedha za Umma na matumizi mabaya"

Amesema Vyombo husika vya Serikali vina wajibu wa kuchukua hatua ili Fedha za Wananchi zisichezewe
Zilipendwa.
 
Back
Top Bottom