Standards Person
JF-Expert Member
- Apr 22, 2021
- 672
- 860
Katika mapokezi ya makamu mwenyekiti wa CCM bara ndugu Abrahaman Omari Kinana jana, amesema amepewa maelekezo na mwenyekiti wake aanze kupitia baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa Tanga.
Kinana utakapo karibia Tanga fanya liwezekanalo hata kwa dakika chache uonane na aliyekua afisa elimu taaluma upande wa sekondari anayeitwa Bhoke ili upate picha ya ukatili uliopo jiji la Tanga
Baada ya mama huyo kuibua wizi wa mamilioni ya fedha za ujenzi zilizoliwa na mkuu wa shule moja jijini hapo na mabosi wake,manyanyaso yalianza ofisini kutoka kwa afisa elimu sekondari na aliyekua mkurugenzi wa jiji ambae kwa sasa hayupo. Kutokana na manyanyaso hayo mama huyo akaamua kuacha kazi. Je nimanyanyaso ya namna gani? Kinana mtafute mama huyo utapata picha kamili ya uozo uliopo Tanga jiji.
Baada ya wizi huo mkuu wa shule alisimamishwa kazi na TAKUKURU wakaingia kazini. Kumbe waliokua wanachunguza nao waliingia bei wakaanza kunyanyasa waliotoa ushahidi na kumuacha akijitamba mtaani mwizi huyo.
Tena kwa kuthibitisha na kuonesha udhaifu mkubwa wa kila aina ya rushwa mkuu huyo wa shule ambae ni mwanamke ati akapewa nafasi akaenda kukalia kiti cha afisa elimu taaluma. Kutoka tuhuma ya wizi hadi kukaa kwenye kiti cha afisa elimu. Hii rushwa iangaliwe vizuri. Ikumbukwe afisa elimu naye ametajwa katika wizi huo mkubwa.
Baadae walikuja watu wa TAMISEMI wakatoa amri mwanamke huyo atoke haraka sana ndani ya ofisi ya afisa elimu sekondari.
Ili kuonesha Tanga imeoza mtu ambaye ana tuhuma ya wizi na anachunguzwa na TAKUKURU eti anapewa uafisa elimu kata.
Tanga ni rushwa na rushwa ni Tanga. Mifumo imekua ya rushwa.
Ofisi ya afisa elimu ichunguzwe vizuri dhidi ya mwanamke huyo. TAKUKURU nao watoe muelekeo wa fedha zilizoibiwa.
Pia TAKUKURU na afisa elimu sekondari wachunguzwe kwamba je wana maslahi gani katika mamilioni yaliyoibiwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Comrade Kinana usifanye makosa