BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewata wajumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro kuchagua watu sahihi wanaokubalika na wananchi.
Aidha, amewataka kuepukana na kasumba ya kupigana fitna na tabia ya watu wenye uwezo ndani ya chama kupigwa vita ili kuwarudisha nyuma katika harakati zao ndani ya chama.
Kinana amesema kumekuwa na mwendelezo wa matumizi mabaya ya fedha za umma, hatua zinatakiwa kuchukuliwa kama mfano.
“Serikali ifanyie kazi ripoti ya CAG ili wananchi waridhike mali ya umma haitumiki vibaya. Mnaunga mkono au tuwahurumie, haiwezekani vitabu vya CAG vinaandikwa kila mwaka hali inakuwa hivyohivyo,” - Kinana.
Nanye katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabihya amemwakikishia makamu mwenyekiti kwamba uchaguzi utafanyika kwa haki na kwamba mchakato wote umeshakamilika.
Source: Wasafi