Kinana: Viongozi wazuri wanaogopa kugombea sababu wanajua watatakiwa kutoa fedha nyingi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewata wajumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro kuchagua watu sahihi wanaokubalika na wananchi.

Aidha, amewataka kuepukana na kasumba ya kupigana fitna na tabia ya watu wenye uwezo ndani ya chama kupigwa vita ili kuwarudisha nyuma katika harakati zao ndani ya chama.

Kinana amesema kumekuwa na mwendelezo wa matumizi mabaya ya fedha za umma, hatua zinatakiwa kuchukuliwa kama mfano.

“Serikali ifanyie kazi ripoti ya CAG ili wananchi waridhike mali ya umma haitumiki vibaya. Mnaunga mkono au tuwahurumie, haiwezekani vitabu vya CAG vinaandikwa kila mwaka hali inakuwa hivyohivyo,” - Kinana.

Nanye katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabihya amemwakikishia makamu mwenyekiti kwamba uchaguzi utafanyika kwa haki na kwamba mchakato wote umeshakamilika.

Source: Wasafi
 
Anacho shangaa ni nini, huku hayo mambo aliyaanzisha yeye na rafiki take Kikwete-Magufuli akaipenda hiyo model naye akatembea nayo.
Kitu ukianzishe mwenyewe halafu Leo utake kukirekebisha wewe mwenyewe yatakuwa maajabu ya dunia.
 
According to Kinana, ili update uongozi ndani ya CCM lazima utoe hela. Ila sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani wagombea wanatoa 'hela nyingi' kiasi kwamba wale wenye hela kidogo wanaogopa kujitokeza kugombea uongozi.
 
 
According to Kinana, ili update uongozi ndani ya CCM lazima utoe hela. Ila sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani wagombea wanatoa 'hela nyingi' kiasi kwamba wale wenye hela kidogo wanaogopa kujitokeza kugombea uongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…