Elections 2010 Kinana Vs Prof. Mwesiga Baregu leo BBC

Elections 2010 Kinana Vs Prof. Mwesiga Baregu leo BBC

Ngoja niisikilize manake nina hasira na uyu Msomali,naona ndo yenyewe naona wanawatambulisha apa
 
Ndo nasikiliza apa Buregu anasema "Ujinga,umasikini na hofu" ndo vinawafanya watu wapite bila kupingwa maeneo fulani fulani.
Alafu Kinana anasema elimu bure haiwezekani bse 71% ya budget ya serikali itatumika kufanikisha ilo.
Tatizo ni kuwa anafikiria hayo kwa kuassume kuwa serikali bado itakuwa ya CCM na source za mapato ni yale yale toka enzi za walimu SODA,BEER,PAYEE
 
Kinana anasema midaharo kwa TV haina tija bse wabunge wa CCM wako bize ratiba iko tight.
U mean hawa wabunge wako busy mpaka usiku?
 
Na mimi nimewasikiliza lakini kama kawaida Kinana hana jipya. Yuko kwenye ulinzi wa maslahi yake.

Kaambiwa ukweli kwamba mazingira ya wapiga kura 2005 na sasa yamebadilika sana. Na huu ndio ukweli maana na mimi niko huku huku kwa wapiga kura. Naomba nimsahihishe mh Baregu kwamba ushindi wa Dr Slaa hautakuwa asilimia 50 bali utakuwa asilimia 70. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu rais aliye madarakani anakwenda kushindwa vibaya.

Kuna mahali nimepita leo nikakutana mama mmoja ambaye ni mgombea ubunge kupitia viti maalum kupitia CCM pia alikuwa katika bunge lililopita na akaniona nikiwa na kofia ikiwa imeandikwa chagua Chadema. Nilikuwa katikati ya watu anaowafahamu nao walikuwa wakimpongeza kwa kuchaguliwa tena kuingia bungeni kupitia viti maalum, akashukuru lakini mie nikadakia kuwa hajachaguliwa huyo maana anasubiri kura zitoshe za kumpeleka huko bungeni, na aliniangalia kwa hasira akijua wazi siko upande wake. Akawambia niliokuwa nao akidhani ni watu wa upande wake maana wao hawakuwa na vitambulisho rasmi kama mimi akisema "ahhhhh hawa tayari wameshashindwa" nikamwambia mama kura ni siri na hiyo siri utaibaini baada ya tarehe 31/10.

Na alipoondoka wale niliokuwa nao wakaanza kumbeza na kuichafua sisi m kwa jinsi ilivyonishangaza sana. Nikabaini kuwa pale nilipokuwa tu kulikuwa na watu wapata 20 wote wako upande wa Dr Slaa. Nilibaki nikimhurumia mama yule. Hali ndivyo ilivyo na ujumbe huu aujue Kinana kwamba sasa kuna mabadiliko. Tunazo daftari za wapiga kura na wote watakaopiga kura twawafahamu, safari hii sisi m inafulia.Twawasihi waje kwenye mdahalo lakini wasipopenda wajue kipigo ki pale pale

Habari ndio hiyo.
 
Naomba nimsahihishe mh Baregu kwamba ushindi wa Dr Slaa hautakuwa asilimia 50 bali utakuwa asilimia 70. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu rais aliye madarakani anakwenda kushindwa vibaya.

mkuu unazungumzia ushindi huu kwa tume hiihii? unakumbuka ya kivuitu? sidhani kama kwa katiba hii, tume hii, mbinu hizi kuna 70% victory

Cha maana ni kupunguza gap na representation bungeni iwe balanced kujiandaa na 2015 vizuri
 
Atishiwa kuuawa kwa kutoinadi CCM Moshi Mjini
Na Salome Kitomary , 11th September 2010

Buni.jpg

Athuman Ramole.

Mgombea aliyeshinda kura za maoni katika jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kisha kuenguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, ametishiwa kuuawa.
Athuman Ramole (pichani) maarufu kama Buni, ametishiwa kifo pamoja na kuhujumiwa katika biashara zake na watu wasiofahamika.
Taarifa zinadai kuwa vitisho hivyo vinatolewa kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kutoshiriki mikutano ya kampeni ya kumnadi mgombea aliyepitishwa na Nec kuwania ubunge wa jimbo hilo, Justine Salakana.
Akizungumzia vitisho hivyo jana, Ramole alisema kwa muda mrefu hakuwepo nchini kutokana na majukumu yake ya kibiashara na kwamba alirejea Septemba 9, mwaka huu.
Alidai kuwa baada ya kurejea mjini hapa, watu walio karibu naye (hakuwataja majina) walimfikishia taarifa za kufanyika kwa kikao kilichomjadili na kufikia uamuzi wa kumuua na kuhujumu biashara zake.
Kada huyo wa CCM ameshatoa taarifa Kituo cha Kati cha Polisi mjini Moshi na kufungua jalada lenye namba MOSH/RB/12212/2010 la Septemba 10, mwaka huu.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lucas Ng'hoboko, alithibitisha kupokea taarifa ya kufunguliwa kwa jalada hilo na kusema polisi inaendelea na uchunguzi.
"Tumepokea taarifa za kutishiwa kuuawa ambazo anadai kaelezwa na wasiri wake, tunazifanyia kazi kwa umakini mkubwa, maana kipindi hiki cha kampeni ni kigumu," alisema.
Ng'hoboko alisema baadhi ya tuhuma zinazotolewa kipindi hiki zinaweza kuwa na ukweli ama mbinu za kisiasa.
"Tunachunguza kwa makini, polisi tunalaumiwa kuwa tunatumiwa na wanasiasa, ila wajibu wa polisi ni kupeleleza taarifa zozote tunazoletewa,"alisema.
Ramole alisema anawashangaa watu wanaokutana kwenye kikao na kupanga njama hizo kwa madai kuwa hamuungi mkono Salakana.
Alisema dhamira yake ni kuona CCM inashindwa kiti cha ubunge Moshi Mjini kama na kwamba alishayakubali na kuyatambua maamuzi ya Nec.
Lakini alidai kwamba kuna baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya mkoa na wilaya, waliomtumia taarifa za kumlazimisha apande jukwaani na kumnadi Salakana.
"Nawaomba waache vitisho juu yangu, nimeshaenguliwa na nimeridhika, kwa sasa ni mwanachama wa kawaida, wasiniite kwa vitisho kwenye vikao vyao vya ushindi jimbo la Moshi Mjini," alisema.
Alisema ingawa ana nia ya kushiriki kampeni hizo, lakini hayupo tayari kujihusisha na masuala ya ndani kwa kuhofia kupakwa matope ikiwa siri za mikakati ya CCM zitavuja.
Ramole alisema kuna kikundi cha majungu katika jimbo hilo,ambacho kimekuwa kikipeleka maneno kwenye Kamati Kuu ya CCM kwa lengo la kuwachafua wanachama wengine.
NIPASHE iliwasiliana na Katibu wa CCM mkoani hapa, Steven Kazidi, ambaye alisema hajapata taarifa hizo.
Kazidi ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi ndani ya CCM mkoani hapa, alisema suala la Ramole kutopanda jukwaani kumnadi Salakana, hana uhakika nalo kwa kuwa hajashiriki kwenye mikutano yote ya kampeniya CCM jimbo la Moshi Mjini.
Katika kura za maoni zilizofanyika katika jimbo hilo, Ramole aliibukana ushindi wa kura 1,554, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Kilimanjaro,Thomas Ngawaiya (1,539) na Salakana (1,152).
Jimbo hilo limekuwa gumzo ndani ya CCM kuanzia ngazi yaTaifa, mkoa na wilaya kutokana na kushikiliwa na upinzani kwa vipindi vitatu, ambapo kwa sasa CCM imeweka nguvu kubwa kupata ushindi.


Chama Kikongwe, kazi kweli kweli mwaka huu. Au uko nao au ni adui nao.
 
Halafu kibaya zaidi, Kinana anabisha kuwa SI KWELI. Msomali bana!!!!!

Mgombea avamiwa na kucharazwa mapanga

11th September 2010
Mgombea udiwani Kata ya Kirumba, jijini Mwanza, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Novatus Manoko, amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Katika tukio hilo, Manoko alijeruhiwa sehemu za kichwani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoani wa Mwanza, Simon Sirro, alithibitisha kuwepo taarifa za tukio hilo, lakini alitaka kupewa muda kabla ya kufafanua undani wake.
"Nimesikia tu kuhusu tukio hilo lakini bado nalifuatilia, nitafute baadaye naweza kuwa nimelipata vizuri," alisema Sirro alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu
Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na mbinu chafu za kisiasa zenye lengo la kuwadhoofisha wagombea kupitia vyama vya upinzani ndani ya kata hiyo.
Habari zilizolifikia NIPASHE kwa njia ya simu jana zilidai kuwa, Manoko ambaye pia ni Mwenyekiti wa soko la kimataifa la Mwaloni lililopo Kirumba jijini hapa, alivamiwa saa nne za usiku juzi, wakati akitoka kwenye vikao vya ndani vya Chadema.
Katika tukio hilo, Manoko aliporwa simu mbili za mkononi na nyaraka kadhaa alizokuwa nazo.
Ilidaiwa kuwa mgombea huyo alivamiwa na kundi la watu baada ya kufika kwenye geti la nyumba yake iliyopo Kirumba.
Habari zinadai kuwa watu hao walimzingira Manoko ambaye wakati huo alikuwa kwenye gari lake na kumshambulia kwa mapanga.
Manoko alikimbizwa katika hospitali ya serikali ya mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure kwa matibabu.
"Sisi wakazi wa Kirumba tunaamini hizi ni siasa tu kwa sababu jamaa anakubalika mno," alisema mmoja wa wakazi wa kata hiyo ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake.
NIPASHE ilijaribu kumtafuta Manoko ili aweze kuthibitisha juu ya tukio hilo, bila mafanikio kwa vile simu zake hazikupatikana.
Hili ni tukio la kwanza kutokea Jijini Mwanza kwa mgombea wa chama cha siasa kuvamiwa na kukatwa mapanga tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Pia, Katibu Mkuu wa Chadema mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia simu kutoka nyumbani kwa Manoko, Mushumbusi alidai kwamba dalili zinaonyesha kuwepo sababu za kisiasa.
Alisema baada ya tukio hilo, Manoko alikwenda hospitali alipopata matibabu na baadaye kuruhusiwa kujerea nyumbani.


Habari zote kutoka IPPMEDIA.COm
 
Hizo pembe za ndovu zimeuzwa kinyemela ili kupata hela ya kampeni, kumbuka kauli mbiu ya CCM 'ushindi ni lazima' kwa hiyo kesi yake ni sawa na EPA au RADA watakaopatikana nazo wataambiwa wazirudishe halafu ndo itakuwa mwisho wa habari
 
Leo wana JF Kinana kathubutu kusema Kikwete sio SIZE ya Slaa, nimekubali kwa sababu Kikwete ni "Dakta ??" na Slaa ni "Doctor PhD" ni tofauti mno kiasi kwamba hawawezi kusizeshana!
usibishe mtu wangu, JK ni dokta wa ukweli dunian hakuna, kawahtubia wagosi wa tanga kuwa CCm imejenga maabara kubwa na ya kisasa ktk hospital ya bombo dunian hakuna.
 
Hizo pembe za ndovu zimeuzwa kinyemela ili kupata hela ya kampeni, kumbuka kauli mbiu ya CCM 'ushindi ni lazima' kwa hiyo kesi yake ni sawa na EPA au RADA watakaopatikana nazo wataambiwa wazirudishe halafu ndo itakuwa mwisho wa habari


....Waziri wa maliasili ..alikuwa na firm direction toka kwa muungwana ...kuhakikisha anapigana Tanzania ipate ruhusa ya kuuza meno ya tembo yaliyoko kwenye bohari la wizara ya maliasili pale dar...kama sio kenya kutia ngumu...lengo lao ni kupaata fedha za kampeni....
Meno ambaye kikwete na shamsa wanayauza kwa magendo kwa sasa ni yale ambayo yalikuwa yakikamatwa na vyombo vya dola toka kwa wawindaji haramu hasa wa kisomali...........
Baada ya vyombo vya kimataifa kuwanyima ruhusa ...ndo maana wameanza kuyauza kwa magendo.....na pesa zilizopatikana shamsa ambaye yupo kwenye kamati ya kutafuta ushindi kwa kiwete ..amechangia kampeni na nyingine alizitumia kugawa kwa wapiga kura kule ubungo[hata hivyo alishindwa]....ambapo hata hivyo shamsa ameshaahidiwa ubunge wa kuteuliwa na rais kwa ajili ya kazi hiyo...
 
kinana! sheikh yahaya husen! mh! na lowasa na rostam wako wapi vile? kama naota nngoja nikalale
 
Ndo nasikiliza apa Buregu anasema "Ujinga,umasikini na hofu" ndo vinawafanya watu wapite bila kupingwa maeneo fulani fulani.
Alafu Kinana anasema elimu bure haiwezekani bse 71% ya budget ya serikali itatumika kufanikisha ilo.
Tatizo ni kuwa anafikiria hayo kwa kuassume kuwa serikali bado itakuwa ya CCM na source za mapato ni yale yale toka enzi za walimu SODA,BEER,PAYEE
you are genious
 
Quote: Prof Baregu. "Kama tunataka kujenga demokrasia tuache kutumia umasikini wa watu kama ndio rasilimali ya chama chenu, kwa sababu inaelekea sasa chama CCM ili mtu kupita bila kupingwa ni mambo matatu yanatumika: moja ni ujinga, umasikini, hofu...."

akaeleza zaidi baada ya Kinana kumuattack

Prof Baregu. "..Sijasema kwamba watanzania ni wajinga, ni masikini, wala nini, ninasema kwamba CCM inatumia unyonge wa watanzania wa kila aina ili kujenga political capital..."
 
Back
Top Bottom