Kinana: Waacheni wakulima wauze mazao yao sehemu yoyote wanayodhani watapata bei nzuri

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466
IMG-20220903-WA0036.jpg

Kinana ashauri wakulima waachwe wauze popote wanapopata bei nzuri

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Ndugu Abdulrahman Kinana ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya wakulima pale wanapotaka kuuza mazao yao.

Akizungumza na wana CCM na wananchi waliyojitokeza kumlaki Nyakanazi, Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Kinana amesema nia ya mkulima na mfanyakazi ni kuondokana na umasikini na siyo kukutana kubaki katika umaskini kwa sababu ya vikwazo.

“Watu wanalima, watu wanafanyakazi ili kuondokana na umasikini sio kuendelea na umaskini kwa sababu ya vikwazo. Wakati wa kulima hatuwasaidii, wakati wa kupalilia hutuwasaidii, wakati wa kuweka dawa hatuwasaidii,wanapokwenda kuvuna hatuwasaidii, wakishavuna wanataka kuuza wanapoona watapata bei nzuri ndipo na sisi wenye utaratibu tunajitokeza sio sawa.

Ajabu shamba ni la mkulima, kahawa ni yake, mkulima ndio kavuja jasho lakini mnanizuia kuuza ninapoona bei ni nzuri basi nileteeni mwenye bei nzuri niwauzie. Naomba tujiepushe kuwawekea wananchi wetu mazingira magumu wanapotaka kuuza mazao yao.“ alisema Kinana huku akishangiliwa.

Kinana amemuomba mkuu wa mkoa wa Kagera kuwalinda wakulima wanapotaka kuuza kahawa yao nje.

“Hakuna kahawa ya magendo, Kahawa ni yangu nikitaka kuiuza popote kwa yoyote mwenye bei nzuri inakuaje magendo?” Aliuliza Kinana

Kinana ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika ziara yake iliyoanzia mkoani Kigoma anatarajiwa kuelekea mkoani Geita kabla ya kuhitimisha katika mkoa wa Mwanza.

#CCMImara #KaziIendelee
 
View attachment 2343997

hii ilikuwa sera ya chadema 2020, kuruhusu wakulima wauze popote
 
Huyu mzee anatafuta kufia kwenye majukwaa. Kama alishindwa kukiwa chama salama kipindi cha JK hadi chama kutaka kuwafia mikononi hatoweza sasa.

Kwanza kwa nafasi yake hakutakiwa kuwa mtu wa field, alitakiwa asimame kama mwenyekiti kwa maana ya msaidizi wa mwenyekiti ambaye ni rais. Kuhakikisha anasimamia oganaizesheni zote za chama.

Sasa hapa yeye ndio mpiga ngoma na yeye ndio mchezaji.

Labda kama anatafuta perdiem. Angalia hata idadi ya watu kwenye huo mkutano.
 
Nihabari njema Sana hii 😍
 
Kati ya viongozi wenye akili na uelewa mpana, huyo Kinana lazima ni miongoni. Kwa sasa, hakika, hakuna wa kumfikoa ndani ya Serikali. Viongozi wa Serikali wapokee ushauri wa Kinana.

Tazhngu amerudi kwenye siasa, kila alichoongea ni halisia na kina mantiki.

Ni lazima Serikali ikiache kilimo kiwe na faida. Kikiwa na faida, watu wengi watafanya shughuli za kilimo.

Kuna watu wameteswa na kuonewa sana kwa sababu ya korosho, wakati korosho ni zao. Waliporwa na kutengenezewa kesi zisizo na vichwa wala miguu.

Azamnhawapangiwa kwa kuuza juice. TBL hawapangiwi. Wazalishaji wa cement hawapangiwi. Kwa nini wakulima wapangiwe? Ukiweka taratibu mbaya kwenye kilimo, lazima sekta itakimbiwa na kila mwenye akili.
 
Huyu mzee anatafuta kufia kwenye majukwaa. Kama alishindwa kukiwa chama salama kipindi cha JK hadi chama kutaka kuwafia mikononi hatoweza sasa.

Kwanza kwa nafasi yake hakutakiwa kuwa mtu wa field, alitakiwa asimame kama mwenyekiti kwa maana ya msaidizi wa mwenyekiti ambaye ni rais. Kuhakikisha anasimamia oganaizesheni zote za chama.

Sasa hapa yeye ndio mpiga ngoma na yeye ndio mchezaji.

Labda kama anatafuta perdiem. Angalia hata idadi ya watu kwenye huo mkutano.
Ni mpuuzi wa kiwango cha Phd
 
Back
Top Bottom