Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona mmeanza kuwewesekaHivi mnafikiri CCM ni kama Chadema ambayo ikiguswa kidogo ina sambaratika.
Li ccm sasa kwishneyyyyyyyyView attachment 365947
bondi ameshatua dodoma mtagawana mbao 23 .07.2016Wote watafichuliwa.
Wadau amani iwe kwenu,
Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.
Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.
Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.
Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.
Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.
Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.
Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.
Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.
Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.
Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?
Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Ha ha ha dah kweli nimeamini kwa sasa mmeshikwa pabayaChama kimezaliwa upya. Wasaliti wanapaswa kwenda kutafuta maficho yao CHADEMA
Mkuu tuwekee ushahidi hapa tafadhaliKiukweli hata mimi najua na ushahidi ninao jinsi luhavi alivyoiba pesa cha kampeni kwenye uchaguzi mkuu wa 2015,magu asipomtumbua hatukubali.
Piga ua ana back-up ya JK usimu-underrate kihivyo. Kama umesikiliza hotuba ya mpendwa wetu alipohutubia wakurugenzi wapya alikuwa akiwajibu hawa. JPM naye si haba Ndugu yangu. Atatuongoza Penda usipende. Niishie hapoLuhwavi mwepesi sana
Dah seeing is believing!!Mashtaka yanayomkabili Gwajima ni ya kumtukana Pengo. Hakuhudhuria mara kadhaa kesi yake ilipotajwa ndipo mahakama ikatoa kibali kwa Polisi kumkamata na kumfikisha mahakamani. Kutafutwa kwake na polisi hakuna uhusiano na alichokisema kuhusu CCM
Humtakii mema JPM. Kwa mustakbari wa Ustawi WA nchi hii lazima kwa sasa awe mwenyekiti ili akibadili katiba ndipo aachie mwingineLiz mi naikubali kazi ya mheshimiwa ila kama anataka aoneshe dhamira ya kweli ktk hili aanze kuukana uenyekiti na wala si vinginevyo unless bisness as usual!
Hivi mkuu hajakuona tu kwenye teuzi zinazoendelea? Maana umejikosha vya kutosha kuonekana.Hahahahahaaaaaaa! Ni kazi ya mikono yangu hiyo Mkuu. Hutapata mahala pengine nje ya hapa JF. Lizaboni ni wa level nyingine Mkuu
Mzee wangu umenichekesha sana, wewe ni Kitwanga nini?Swali gani aliuliza huyo Ndugu???!!!! By the way hujui kuwa SWALI hujibiwa kwa SWALI???? Nikupe mfano mmoja: Miaka ya nyuma mjini Nairobi, Kenya Mwandishi wa habari mmoja mnoko alimuuliza Mwalimu Nyerere swali kwamba zipo tetesi kuwa mwalimu Nyerere anataka kumuondoa madarakaini Rais Mwinyi, je kuna ukweli wowote wa tetesi hizo? Mwalimu Nyerere akamwangalia mwandishi wa habari yule na akamjibu ifuatavyo: Wewe ukiambiwa kuwa .... ni mume wa mama yako, utakubali?....Kwa jibu hilo mwandishi wa habari yule akabaki anazungusha macho tu....
Ila unapenda misifa sana, nadhani unatamani upate udc lakini umeshachelewa. PoleMkuu, potezea. Kwa sasa tupo kwenye mjadala wa Luhwavi. Ukiwa na kazi ya kunisaka mimi hakika utaumia sana kwa maana mpaka unaingia kaburini hutakuja kumjua Lizaboni
Kuna bandiko lako humu kuhusu Ester Bulaya kutembea na waume za watu. Hivyo wewe unajua kuanzia siri za watu, ukawa, ccm, ikulu, nk.Mkuu, potezea. Kwa sasa tupo kwenye mjadala wa Luhwavi. Ukiwa na kazi ya kunisaka mimi hakika utaumia sana kwa maana mpaka unaingia kaburini hutakuja kumjua Lizaboni
Yeye ni Mungu makada wasimpinge? Acha figisu figisu za kusaka tonge.Wadau amani iwe kwenu,
Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.
Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.
Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.
Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.
Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.
Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.
Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.
Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.
Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.
Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?
Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Mkuu lumumba sasa hali siyo shwari tenaHa ha ha ni wewe Lizaboni ama ni mwingine. Sio wewe uliyokuwa unabeza kuwamba hakuna mgogoro wa aina yoyote Lumumba, kazi kushabikia mambo ya wale wa Ufipa?. Dah huyu bundi aliyetua sasa inabidi tufahamu katumwa na nani maana kachanganya magamba mwanzo mwisho
Lumumba nyumba ya nyasi inateketea sasaPiga ua ana back-up ya JK usimu-underrate kihivyo. Kama umesikiliza hotuba ya mpendwa wetu alipohutubia wakurugenzi wapya alikuwa akiwajibu hawa. JPM naye si haba Ndugu yangu. Atatuongoza Penda usipende. Niishie hapo