gogo la shamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 6,669
- 2,165
kwa hiyo na huyo aliyotoa hayo maneno watamgwajima?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
CCM ni tofauti na vyama vingine, vina utaratibu. Kuna vikao vya ndani na kwa vile unasema ushahidi upo kwa nini asiulizwe au kuhijiwa huko na kupewa adhabu au onyo kwa mujibu aa kanuni? Au uantaka kusema CCM ndio imekutuma yenyewe, kwamba labda inamuogopa face kwa face. Bado hujaiva kumbe umeteleza ndugu yangu, nilidhani kadha umeiva kindakidnaki. Haya mambo ya makumbano, tetesi, fitna mitandaoni sio ya CCMNi jukumu langu kuyaweka hadharani madudu yote yanayofanyika chamani bila kujali yanafanywa na nani
Mhh, bundi ameingia nyumba ya jirani. Ngoja tusubiri hiyo Julai 23, 2016Mi nahisi watu watachapana makonde siku hiyo,tusubiri tuone.
Kama umetumwa shauri yako. Ila hapa JF hata Rais wetu anapata habari. Wahusika wamesikia na hatua zitafhukuliwaCCM ni tofauti na vyama vingine, vina utaratibu. Kuna vikao vya ndani na kwa vile unasema ushahidi upo kwa nini asiulizwe au kuhijiwa huko na kupewa adhabu au onyo kwa mujibu aa kanuni? Au uantaka kusema CCM ndio imekutuma yenyewe, kwamba labda inamuogopa face kwa face. Bado hujaiva kumbe umeteleza ndugu yangu, nilidhani kadha umeiva kindakidnaki. Haya mambo ya makumbano, tetesi, fitna mitandaoni sio ya CCM
Jibu swali kwanza wacha kumbwelambwela
Hiyo ndiyo tabia ya manyang'au mzoga unapoisha, wanaanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe na ole wako mdomo uwe na harufu ya damu...!
Hivi huu ujasiri wa kuwatetea wezi mnautoa wapi?
mkuu pokea like.. wewe level nyingine..Hahahahahaaaaaaa! Ni kazi ya mikono yangu hiyo Mkuu. Hutapata mahala pengine nje ya hapa JF. Lizaboni ni wa level nyingine Mkuu
Hata mimi namshangaaWewe huyo huyo uliwahi kupinga kwamba hakuna kitu kama hicho, sasa unatuletea hii taarifa ili tufanye nini?
Upuuzi wa hivi ndio unaodhibitisha kuwa yeyote mwenye akili timamu hawezi kuwa ndani ya ccm. Yaani kwa kuwa umegundua kuwa esitena tetena ni mwenzako siyo hao unaowaita misukule umemuomba msamaha! Lakini kitu kilekile alichoandika ukidhani kuwa kimeandikwa na hao 'usiowapenda' unajibu utumbo. Kwa tabia hizi ni lini mtaweka maslahi ya taifa letu mbele?!Sorry mkuu. Nilidhani hawa misukule
Mi nadhani nenda chimbo tena katafute alichokuwa akifanya ktk ziara yake ya mikoani. Siyo icho ulichokileta hapa na ziara ilikuwa ya wazi na wanaccm anayefuatilia siasa ndani ya ccm anajua alichokuwa akifanya mzee Luhawavi, tuache MajunguWadau amani iwe kwenu,
Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.
Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.
Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.
Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.
Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.
Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.
Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.
Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.
Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.
Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?
Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Huyo Lizabon atueleze ni nani aligharimia kazi ya kukusanya hizo tetesi!Lizaboni leo umeonesha ujinga wa hali ya juu, unakuja na tetesi za kuwqchafua viongozi wa Chama na kuleta mitafuruku, ndio siasa za Chama mitandaoni? Au unatumika?