Kindoo cha lita 10 kikijaa msosi nina uwezo wa kula na kumaliza msos peke yangu.ushauri please.

Kindoo cha lita 10 kikijaa msosi nina uwezo wa kula na kumaliza msos peke yangu.ushauri please.

Sio kweli japokuwa tumbo ni elastic bag lakini volume ya ndoo ndogo is way beyond stomach's holding capacity ambayo ina range kati ya 1-4 litres of food
 
Duu, umenikumbusha wakati niko O-Level kule Tanga (TTS), jamaa walibishana kama kuna mtu anaweza maliza mikate 10. Msukuma mmoja toka Magu, Masanzakona, kijiji cha Gininiga akadai yeye anaweza. Ikaamuriwa kuwa akiweza kuila yote hamna deni ila, akishindwa kuimaliza mikate hiyo kumi basi anapaswa kulipa mikate hiyo pamoja na ile aloibakiza. Jamaa alituacha hoi kwa kuomba chai ya rangi kikombe cha nusu lita, alipoletewa alianza kama ifuatavyo.....Jamaa aliipiga ile mikate mikavumikavu wa kwanza hadi wa 8, akashushia na funda la chai.......jamaa aliyenunua ile mikate kuona hivyo akaamua kuipora ile 2 ilobaki ili asipate hasara....

agha ,agha,
 
mkuu inategemeana unakula chakula gani bana? hembu jaribu kula ugali maharage tena dona harafu njoo na feed back.
usije ukawa unatafuna chips au kula vitu lain laini.
 
mkuu;ukiona umemaliza andaa na kaburi mapema usitupe tabu siye!
 
Aiseeee?! Hapo ushauri wakitabu hakuna ila nakushauri utafute shamba kama heka tano na uwe unalima mwenyewe kwa jembe la mkono ili ukitendee haki hicho chakula
 
Duh, sijui nikupe pole au, maana sijajua kama ni ugonjwa au ndo uwezo wako wa kula. But hopefully utapata ushauri mzuri.
 
Huo ni uwezo wako Mkuu wa kumenyuka
sasa Ushauriwe nini tena ?
Maana mtu akisema usile hivyo ni wazi
utakaa na njaa sasa huoni tena utajitesa.

ningekuwa naenda toi sawa, nisingejisumbua kuomba nishauliwe.
 
Habari madoctor wa jf .mimi nina uwezo wa kumaliza chakula chenye ujazo wa kindo lita kumi,je! linaweza likawa tatizo lolote tumbon mwangu?.halafu cha ajabu sipati haja kubwa nina mwezi sasa...naomba ushaur.......

Hiyo ni kawaida tu hata Punda anaweza......tena yeye unamuongezea na ndoo ya maji!
 
Habari madoctor wa jf .mimi nina uwezo wa kumaliza chakula chenye ujazo wa kindo lita kumi,je! linaweza likawa tatizo lolote tumbon mwangu?.halafu cha ajabu sipati haja kubwa nina mwezi sasa...naomba ushaur.......

Mkuu hiyo ni kali sana, tafuta kiongozi wa dini unayoabudu akuombee mana nahisi kuna mtu anakula hicho chakula sio wewe. Pole sana mkuu
 
Hivi hujiulizi hicho chakula chote hicho kinaenda wapi kama hupati choo?
 
Hyo ni business opportunity tu mkuu,

Unaweza kutengeneza pesa nzuri sana kwa kula kwako huko na ukatoka kwenye umasikini soon..........
 
Back
Top Bottom