Salim tevez
JF-Expert Member
- Apr 21, 2016
- 394
- 182
Mkapa na Kikwete vipi?Lowasa na Sumaye vipi?
Nikisema Nduga ni taahira watu watakasirika former PMs so what? Si acha sheria ichukue mkondo wake? Kwa huyu kilaza ndugai yeye kazi yake ni kulinda watu alio karibu nao tu maslahi ya nchi zero! I command Curses against Ndugai!! Hili ni jipu baya kuliko yote!!Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.
----
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.
Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.
"Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe," amesema Lijualikali.
Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.
"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesemaNdugai.
Chanzo: Mwananchi
Tatizo uelewa wako ni mdg,Sililiza wewe nyumbu!
Hivi Sumaye na Lowassa unajua kwamba waliwahi kuwa mawaziri wakuu? Umejihoji na kuona ni kwa kiasi gani kwa nafasi zao wanahusika na haya?
Sasa kabla hujamgusa Mkapa na Kikwete fukuza kwanza Lowasaa na Sumaye ili ukitupa jiwe lisikurudie.
Wote wapotezwe, bila kujali itikadi ya sasa au zamani! Wa sasa na wazamani, wote wapotezwe! Wa richmond, dowans escrow; na waliouza nyumba za serikali kwa vei chee, wote wapotezwe tu. Tumechoka sasa tunasema basi, imetosha!Wote tu waliohusika washtakiwe kama ni wa MACCM au waliohamia Chadema. Kama walihusika kwa namna moja au nyingine basi hakuna jinsi.
Hapo mtoto wa mkulima Pinda hachomoki, Warioba pia hachomoki. Acha washtakiwe hatia au hapana mahakama ndo itaamua..Usikwepe hoja.
Mkapa.
Kikwete
Sumaye
Lowasa.
Je upo tayari hiyo team yote ishtakiwe?