High Vampire
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 2,915
- 2,134
nchi inaendeshwa kwa utaratibu wake ukikataa amri ya polisi upigwe tu sasa wakufanye nini aombe msamaha kwa lipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu unaitafuta burn, watu km huyo pimbi hapo juu wanatia kichefu chefu kwa kauli zao lakini ni vyema kuwapuuza
i have liked your post simply because of that statement in red there.
Hivi mkuu umeambiwa usifanye hivi wewe unafanya tu hivi nini kitatokea siku zote kiongozi anayesimama kwenye haki huwa hapendwi na akipendwa uje anafata matakwa ya anaowaongoza kitu ambacho ni makosa mbona polisi wetu wanakufa Kitengo cha sheria na haki za binadamu mbona huwa hawaongei leo hii kuwaambia polisi wanaokiuka sheria wawajibishwe amefanya kosa ila angesema polisi wauliwe mungefurahi tena ninaomba naye mkuu wa JWTZ naye aseme ukivunja sheria achukuliwe hatua kali africa demokrasia bado haijakua kulingana na nchi za ulaya pinda ni kiongozi shupavu hata waliomchagua hawakukosea kabisa
wanaojiita wanaharakati wa LHRC ni makada wa chadema niliwaona kwenye ITV ni wachagga, je unategemea watatumia weledi kujua kama mbunge akisema bungeni anashtakiwa au maamuzi yake ataongozwa ubavicha?
Soma hii hapa toka Tanzania Daima 31/07/2013 inaweza kukusaidia
UAMUZI wa Kituo cha Haki za Binadamu wa kumshitaki mahakamani Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kauli yake ya kuagiza wananchi wapigwe, imelitikisa taifa kiasi cha kuisukuma ofisi ya Bunge kumkingia kifua.
Huku idadi kubwa ya taasisi na wanasheria mashuhuri wakiungana na kituo hicho katika kumfungulia Waziri Mkuu Pinda mashitaka yanayotarajiwa kufunguliwa kesho jijini Dar es Salaam, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema jana kuwa hawezi kushitakiwa popote kutokana na kuwa na kinga ya kibunge inayomlinda.
Katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, Ndugai alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama, au mahali pengine nje ya Bunge.
Ninashangaa sana wanasheria hawa, tena ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, wameacha kabisa kufuata sheria, sasa naona wanafanya siasa, wanatafuta umaarufu tu na mahakama haitaweza kusikiliza kesi hiyo, alisema Ndugai.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndugai, umepingwa na wanasheria wengi waliohojiwa wakisema kuwa tamko la Pinda linavuka mipaka ya kinga za kibunge, na hivyo anaweza kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili.
Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya kufuatilia mwenendo wa Bunge, Marcus Albany pamoja na kukipongeza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa hatua hiyo, alisema tamko la Waziri Mkuu Pinda ni la hatari na lenye madhara makubwa kwa usalama wa nchi.
Albany alisema waziri mkuu anapaswa kuongezewa mashitaka kwa sababu kauli yake inagusa kosa jingine kwa kulitangazia taifa kuwa serikali iliyoko madarakani imechoka.
Waziri Mkuu hakusema piga tu peke yake, bali alisema pia serikali imechoka, hili nalo ni kosa jingine kwa Waziri Mkuu kulitangazia Bunge kuwa serikali imechoka halafu hataki kujiuzulu, hivyo ashitakiwe tu, alisema.
Mkurugenzi huyo alisema wataungana nao kituo hicho katika mashitaka hayo kwa sababu yana uzito mkubwa na athari kwa taifa ikiwa hakutachukuliwa hatua dhidi ya kiongozi huyo kwa sababu yanaweza kuleta maafa makubwa.
Mwanasheria wa kituo hicho, Harold Sungusia alisema utetezi wa Ndugai umejaa siasa zaidi na ametafsiri kimakosa kifungu hicho cha katiba kinachompa kinga mbunge.
Pinda hataepuka kikombe hiki, ni lazima wafike mahakamani ili mahakama ndiyo iseme kama Pinda alikosea au la.
Sisi tulijua kuwa watajiegemeza katika kipengele hicho cha kinga ya Bunge, lakini tunaenda mahakamani kuiomba mahakama ituambie kama kinga dhidi ya Bunge inamlinda mtu anayevunja katiba, tunataka mahakama ituambie kama mtu anayesema watu wapigwe ni sahihi au la, alisema Sungusia.
Alisema katiba ndiyo sheria mama ambayo Waziri Mkuu Pinda aliivunja kwa tamko lake la hatari na linaloweza kusababisha vurugu na umwagaji wa damu. Hivyo hawatarudi nyuma kumfikisha mahakamani.
Aliongeza kwamba kipengele cha katiba alichoshikilia Ndugai bado kinasisitiza kuwa bila kuathiri katiba, na Waziri Mkuu Pinda hakuvunja kanuni za Bunge tu, alivunja katiba aliyoapa kuilinda, na hivyo kipengele ambacho Bunge kinangangania kipo kinyume cha katiba, na katiba inasisitiza bila kuathiri.
Chukulia kuwa ikatokea siku moja mbunge ama kiongozi mkubwa kabisa akasema wanawake wote wabakwe, asichukuliwe hatua kwa kuwa alisemea bungeni?
Ikitokea waziri akaamuru watu wauawe asishitakiwe kwa kigezo kuwa alisemea bungeni? Tunataka mahakama ndio itoe tafsiri ya kifungu hicho, alisema.
Mwanasheria mwingine maarufu ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na dhamana aliyonayo serikalini, alisema kuwa sheria ya haki na wajibu inayotekelezwa na mahakama ya mwaka 1994, inatoa mwanya kwa Waziri Mkuu kushitakiwa hata kwa alichokisema bungeni.
Hii ni kwa kutumia madaraka ya Mahakama Kuu ya kutengua uamuzi unaolalamikiwa, ili mamlaka husika itoe amri nini kifanyike au mahakama ilazimishe jambo fulani lisifanyike (Prerogative of certiorari, mandamus et Prohibimus), alisema mwanasheria huyo.
Alisema Pinda alikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13(2) inayosema: Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la kibaguzi ama wa dhahiri au taathira yake.
Kifungu cha nne cha ibara hiyo hiyo kinasema ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi. Pinda alitoa kauli hiyo akiwa anatekeleza kazi yake kama kiongozi wa serikali bungeni.
Katiba Ibara ya 13 (6) (e) inaonya kuwa ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha. Pia Ibara ya 16 ya Katiba inasema kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na pia heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake binafsi, alisema.
Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma aliyetaka kujua serikali inavyoshughulikia tuhuma za vyombo vya dola kutuhumiwa kuwapiga wananchi kama ilivyotokea Mtwara na kwingineko, Pinda alijibu:
Ni lile lile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu. Hakuna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndiye jeuri zaidi, watakupiga tu. Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine, maana tumechoka.
Tamko hilo lililoshangiliwa na wabunge karibu wote wa CCM huku wale wa upinzani, wakitikisa vichwa vyao kwa masikitiko lilizua malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania wa kada mbalimbali, na wengine kwenda mbali zaidi wakimtaka kiongozi huyo kujiuzulu.
Ikiwa atafikishwa mahakamani, itakuwa tukio la kwanza katika historia ya Tanzania kwa Waziri Mkuu kushitakiwa kutokana na matamshi yake bungeni, ama akiwa nje ya Bunge.
Dude ,you either need to go back to your english class or stop commenting in english..no disrespect
am not sure of what you are talking about, though i cant say am compintent in that language but at least am far away from you given my background and where i used to spend before.
Duhhh,
yaani mtu umemuona kwenye tv kisha ukajua kuwa ni mchagga?
Kweli bange ni mbaya, kama sio bange vitakuwa ni vitu vingine tu vya kimila kama laana, kubemendwa na makuzi mabaya
Hapana kuna kitu ujakielewa ndugu ebu pitia ile ibara ya 100 ya katiba utajua kinacho maanishwa"kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu ktk bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote ktk jamuhuri ya muhungano au ktk mahakama au MAHALI PENGINEPO NJE YA BUNGE."ndugu kama mbunge akifanya jambo kinyume na sheria bac atashitakiwa na kuhazibiwa kwa mujibu wa sheria kanunu na taratibu za bunge na c vinginevyo ndio maana ya ibara ya 100 ya katibaKinga haina mipaka..??? Yaani hata mtu akiamua ampige spika au yeyote yule akiwa ndani ya bunge bado atakuwa na kinga..??
what is that even supposed to mean?
ENGLISH
- :rip: