king'amuzi cha STar TImes hovyoooo..

king'amuzi cha STar TImes hovyoooo..

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
awali kilikuwa kikikamata shwari kabisa lakini baada ya hali ya hewa kubadilika, king'amuzi cha TBC/star time kinarusha station zote kwa kukwaruza mithili ya CD au video tape iliyokwaruzika.shida tupu!
 
Nilitaka niachane na hawa Easy TV nije huko kumbe nako ni hivyo hivyo, huku Easy TV wao ni kama wanaamua siku fulani nusu ya channels zionekana na siku fulani zionekane na mikwaruso, yani tabu tupu, sijui wakizima hiyo Terrestrial television sijui itakuaje.
 
King'amuzi kipi Bomba jamani? mimi hawa startimes/tbc inaonekama ni king'amuzi cha kisiasa zaidi maana sipendi kuangalia TBC, Channel ten, na akina sibuka sitaki kabisa. Nataka kuangalia ITV, star tv angalau unaweza kupata habari nzuri. wanawalazimisha watu kuangalia hilo li TBC hata kama hawataki we angalia hata usipolipia TBC inaonekana na ndipo watu wanapoiona TBC kuwa sio competitive product.
 
Star times ni product ya Tido Mhando.. Sijui Mshana Clement (Mtendaji Mkuu mpya wa TBC) amekuja na nini jipya!
Star times fake!
 
King'amuzi kipi Bomba jamani? mimi hawa startimes/tbc inaonekama ni king'amuzi cha kisiasa zaidi maana sipendi kuangalia TBC, Channel ten, na akina sibuka sitaki kabisa. Nataka kuangalia ITV, star tv angalau unaweza kupata habari nzuri. wanawalazimisha watu kuangalia hilo li TBC hata kama hawataki we angalia hata usipolipia TBC inaonekana na ndipo watu wanapoiona TBC kuwa sio competitive product.

sibuka wanatatizo gani mbona mimi naona hawa ndiyo wameirudishia kihai
 
awali kilikuwa kikikamata shwari kabisa lakini baada ya hali ya hewa kubadilika, king'amuzi cha TBC/star time kinarusha station zote kwa kukwaruza mithili ya CD au video tape iliyokwaruzika.shida tupu!
Ulitegemea nini kwenye kitu ya kichina hiyo?
 
awafai kabisa tena ni wahuni tena na mpango wa kurudisha wanirudishie pesa zangu
 
Jaribu kuwaita mafundi wao, yawezekana ni suala la kuelekeza antenna sehemu nzuri zaidi yenye kukamata signal.Mie nimekuwa natumia king`amuzi hicho toka mwaka jana sijapata matatizo.
 
awali kilikuwa kikikamata shwari kabisa lakini baada ya hali ya hewa kubadilika, king'amuzi cha TBC/star time kinarusha station zote kwa kukwaruza mithili ya CD au video tape iliyokwaruzika.shida tupu!

Mwenyewe nimekubwa na tatizo hilo hilo nataka niwarudishie tu maana sioni faida ya kulipia 9000/= alafu picha zina nata.
 
Kusema kweli mimi ndio nimekinunua wiki ile ya pasaka; yaani hata signal tu hakuna; hivi nimeamua kukirudisha wanirudishie pesa yangu sitaki tena.
 
awali kilikuwa kikikamata shwari kabisa lakini baada ya hali ya hewa kubadilika, king'amuzi cha TBC/star time kinarusha station zote kwa kukwaruza mithili ya CD au video tape iliyokwaruzika.shida tupu!
Usiseme hivyo bwana, wengine kinatusaidia kuona mashindano ya club bingwa ulaya kupitia KBC1 na mara mojamoja ligi ya uingereza kupitia Sibuka, kina umhimu wake ukilinganisha na gharama yake, ukiona kinakuzingua unachagua dstv kilichobora zaidi au ting cha agape, ile mie sijui permaformance yake ikoje.
 
Ingawa mimi si msemaji wa Star Times, lakini inaonekana wote wenye malalamiko mna matatizo ya Antenna. Niliwahi kuwa na matatizo kama yenu nikawa nikiwasumbua customer care wao kwa sana tu, baadaye nikagundua matatizo yako kwangu, waya wa antenna umechomoka kwenye juu. Niliporekebisha reception ikarudi kama kwanza. Jaribuni kutazama antenna zenu vizuri, kuna uwezekano mkubwa kasoro ipo hapo.
 
hivi kukirudisha inawezekana? nataka wanipe hela yangu niangalie ustaarabu mwingine
 
awali kilikuwa kikikamata shwari kabisa lakini baada ya hali ya hewa kubadilika, king'amuzi cha tbc/star time kinarusha station zote kwa kukwaruza mithili ya cd au video tape iliyokwaruzika.shida tupu!

hivi vingamuzi sina uhakika na performance yake. Nimenunua ting ambayo itv na channel ten zinapatikana, baada ya muda nikakosa signal. Bado nawasiliana nao kuona tatizo ni nini, lakini mwanzo nilipata picha bomba.
 
hivi kukirudisha inawezekana? Nataka wanipe hela yangu niangalie ustaarabu mwingine

kanunue kingamuzi cha ufufuo na uzima ujue wachawi wako ni kinanani na utatokaje na laanza za wazazi wetu mateso yao tuyavuaje!!
 
kanunue kingamuzi cha ufufuo na uzima ujue wachawi wako ni kinanani na utatokaje na laanza za wazazi wetu mateso yao tuyavuaje!!

hicho ndo kipi sasa? kina BBA?
 
Back
Top Bottom