sangkipsigis
Member
- Dec 24, 2008
- 16
- 2
Duh! Mbunge kwa mistari umenikuna. Nakufananisha na wabunge wenzako akina Shibuda na Mudhihiri! Ni hayo tu!TUNACHOTAKIWA Watanzania wote kwa pamoja ni kuamua je, tunachotaka kuweka mbele ni UTANZANIA na UAFRIKA wetu au kabila, dini, rangi, jinsia, usomi, vyeo, kazi, mali au ukoo wetu ?
Kama tumeamua kumpa MUNGU kilicho cha Kaizari sawa!!!
Kama tumeamua kwamba mpanda fahali wawili hawezi kupasuka msamba basi tuendelee na kupanda fahali wawili!
Kama tumeamua kwamba kujenga ufa ni kwa kuongeza ufa mwingine tufanye hivyo!
Kama tumeamua kwamba gauni au suruali mpya hupatikana kwa kushona kiraka juu ya kraka tuendelee vivyo hivyo!
Kama tumeamua kwamba akumulikaye mchana usiku hatakuchoma bali atakumwagia maji ya baridi kwanini tuogope maji ya baridi?
Kama akili ni nywele na kila askofu na sheikh ana mvi na sio nywele nyeusi na tumezipenda mvi zisizo na hekima wala busara kwanini tusizipende!!!
Kama tunadhani fataki hawezi kuwepo kwenye majengo ya makanisa na misikiti tuendelee kuruhusu hata wenda nusu uchi kuja kuswali.
Kama hatujui asiyekutaka au anayekutakia baya hawezi kukwambia toka au hawezi bayana bin bayana kukulaani ngoja asubihi ipishe mchana na jioni ipishe usiku.
Niliwahi kuwaambia mkasome kitabu kinaitwa the root of all evil. Kama hamjui vita vingi vya wenyewe kwa wenyewe vina mkono wa Roman Catholic Church na sasa Tanzania ndipo inapolekea nyie subirini. Kingunge analosema ni kweli na hajakosea hata kidogo tunahitaji watu wenye ushupavu kama huo kunyooshea kidole Tabia kama hii.
Na tukiiachie Tanzania inaelekea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe
Mimi nadhani tumsaidie mzee wetu huyu kwa kumshauri astaafu; kwa kweli hali aliyofikia sasa ni ile ya kukaa nursing home au kupata palliative care tu!!!
Lazima akubali kwamba kila jambo na wakati wake, na kila binadamu ana life span... is has already passed the productive stage na sasa anaelekea destructive stage
I still dont know why media inaendelea kumpa nafasi wakati wakijua wazi kwamba inaweza kuwa counter-productive kwa kingunge na CCM
Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.
Kingunge alisema ni vizuri kanisa likaelewa kuwa lenyewe sio chama cha siasa na kwamba, halina uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi.
Alifafanua kwamba, wakati anazungumzia waraka huo bungeni hakuwa anataka uhasama na kanisa kwa kuwa anaheshimu imani, ila alikuwa akitoa angalizo kwa kuwa dini haiongozi nchi kama serikali.
Alisisitiza kuwa dini si chombo cha kuunganisha watu, bali kuwatenganisha ndiyo maana kila mtu ana dini yake, lakini serikali ni moja, hivyo nchi yenye dini nyingi haiwezi kuunganishwa na dini bali siasa.
Mwaka 1992, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Malawi walitoa waraka kama huu wa kwetu - uliolenga kero za watu (kuboresha huduma za jamii, mgawanyo mzuri wa raslimali za nchi, umaskini, uhuru wa kutoa mawazo, haki za binadamu nk) - na kwa vile ilikuwa mara ya kwanza kupinga hadharani upungufu uliokuwepo katika utawala wa Dr Kamuzu Banda, maaskofu hao waliwekwa chini ya ulinzi na kuitwa wajieleze mbele ya Rais.
Hali ilikuwa tete sana na hata printing press iliyochapa waraka huo ilichomwa moto mara moja!
Wakati huohuo chama tawala (Malawi Congress Party - MCP) kilifanya mkutano wa siri namna ya ama kuwafukuza maaskofu hao nchini au kuwafanya wapotee wasionekane tena bila watu kujua wako wapi. Baadhi ya walikuwa viongozi wa Kanisa na wanachama wa MCP walikana dini hadharani kwa kusema maaskofu wamemdhalilisha Rais wao na hivyo wao wenyewe hawana sababu ya kuendelea kusali kwenye Kanisa ovu namna hiyo.
Maaksofu walitungiwa kila aina ya ubaya lakini kwa vile haki na ukweli husimama mpaka mwisho, wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 1994, chama tawala MCP kilianguka vibaya sana na United Democtatic Front (UDF) kikawa madarakani. Baada ya Dr Banda kuangushwa maaskofu waliombwa wafungue kesi ya kutishiwa kuuawa na Dr Banda lakini walisema wameshamsamehe na hivyo kesi yake kufutwa.
Baada ya Dr Banda kufariki, viongozi waliokana dini hadharani walirudi tena kuomba radhi kanisani kwa kusema walichokisema hakikuwa kimetoka moyoni mwao bali ilikuwa kulinda maslahi yao ya kisiasa tu!
Tanzania tunaelekea kwenye njia ya namna hiyo na hakika haki na ukweli kuhusu waraka huo vitasimama hadi mwisho! Kama kweli nia ya waraka ni kumchagua Rais Mkatoliki au Mkristo au kuleta udini na kinachosemwa dhidi ya Kanisa Katoliki ndiyo kero halisi za Watanzania, basi mwisho wa yote Mungu mwenyewe ataamua ukweli uko wapi!
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu
Nimemuona na kumsikiliza huyu mzee wetu kwa kweli kimawazo/kifikra amekwisha kweli, kama mtu unavyozeeka kasi ya nywele inavyopukutika kichwani iko sawia na kupungua kwa fikra basi mzee wetu tumsamehe kwa kweli, hana HOOJA.
DESPITE THE ABOVE FACT!our gvt will still need ''the vingunges,and the likes''.........I fully support your argument, brain aging....
Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.