Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Mnao mdharau Mzee Kingunge hamjui kitu na mpo kama bendera fuata upepo! Kingunge ni mzee makini sana na mnaofurahia jambo hili mtakuja jutia siku moja!
mbona hata viongozi wakuu wa ccm hawazungumzii tena ishu ya urais now wanadili na wabunge na madiwani
 
Mtu huhitaji kuwa na darubini kuona kwamba mchakato wa CCM ulikuwa wa kihuni na usio wa kidemokrasia.

Hao 33 waliokatwa walikatwa kwa vigezo gani? Walipigiwa kura?

Au walikatwa kwa uamuzi wa watu flani flani tu kwamba huyu na yule hawafai?

Licha ya kwamba Kingunge anaonyesha ni mnafiki lakini kwenye hoja yake ya msingi ana hoja.
 
Kama wenyewe hawajitendei haki unadhani watatenda haki kwa wengine jiulize! !?
Hapo jibu lake ni kuwa kwa wengine wanawafunga magoli ya mikono kwa kwenda mbele, kama ilivyo nukuu ya Nape kule pande ya Mwanza.
 
Sasa aone utamu wa kuvuruga taratibu na mchakato.

Kingunge ulishiriki kuvuruga mchakato wa katiba pendekezwa... Sasa usilalamike, muosha uoshwa.

Huyu kikongwe anapovuruga wananchi wengine anaona raha, yeye akivurugwa ana anza kulalamika. Atulie aone raha ya kuvurugwa.
 
Kingunge ni mnafiki mkubwa kwanza mwaka 2005 alikuwa kwenye kamati ya maadili lakini aliondolewa baada ya kuonyesha upendeleo wa waziwazi kwa JK lakini mwaka huo huo taratibu za kupiga kura zilibdilishwa kiasicha kumshangaza hata katibu mkuu Mang'ula lakini hakusema chochote kingunge alitaka kuwaaminisha watanzania bila yeye hakuna mtu anayewez kuwa rais ccm matokeo yake ameumbuka kingunge mwenyewe ni fisadi nani hajui kampuni ya mke wake ya parking ilipewa kazi wakati ilikuwa haijasajiliwa hata brela, nani hajui kampuni ya kukusanya ushuru ubungo ilivyokuwa inaiibia serikali na nani hajui motto wake anafanya biashara ya madawa ya kulevya kwa sababuameshaingia kwenye ufisadi ndio maana hawezi kupinga ufisadi,mwaka 1995 mtu aliyekuwa na nguvu alikuwa malecela lowasa hakuwa na nguvu yoyote ndio maana Nerere alitishia kurudish kadi mwissho ajue wakai wake umepita nio maana alishindwa hata kupata ujumbe wa halmashauri kuu kwenye uchaguzi
 
wanasiasa wengi wanchi hii bara na visiwani wapinzani ukiangalia historia yao wanatoka ccm
 
Makubwa haya, sasa ni dhahiri CCM vipande vipande.
It is very true Ntobi.

Ingawa walipotoka Dodoma walijifariji kwa kusema wanatoka Dodoma wakiwa more stronger kuliko walivyoenda.

Purely hayo ni maneno ya kujifariji sawa sawa na mgonjwa mahututi anayeendelea kuishi kwa kusaidiwa na mitambo ya kupumulia ya oxygen, akijipa matumaini ya kuishi miaka kadhaa ya mbele ambapo kiuhasia ni kuwa madaktari wakiamua tu kuzima mitambo hiyo ndiyo inakuwa the end of the story.
 
Huyu Kingunge aache double standard. Kwenye Mchakato wa Katiba alikwa tayari kukubaliana na CCM kuwaburuza Watanzania, leo hii kuburuzwa kunamhusu mtu wake Lowassa anaona CCM inafanya vibaya kuburuza mambo...Mkuki kwa nguruwe sio?

Kwanza kama alikuwa na nia ya kumsafisha Lowassa, kwa nini asubiri hadi wakati wa kugombea Uraisi, si angeanza kufanya hivyo mapema ili Lowassa angalau arudishwe kwenye Baraza la Mawaziri mapema kabla ya haya mambo ya uchaguzi mkuu?
 
Bado naamini wafuasi wa Lowassa hawana nguvuya kumtisha mwenyekiti wao na hawana ubavu wa kupiga kura za maruhani. Kama wangeweza basi wangeanzia kumpitisha mgombea dhaifu. Huo ubavu hawana kabisa.
 
Leo Mzee Kingunge kaongea na Vyombo vya Habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.

Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba - kukata majina ya wagombe.

Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.

Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.

Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.

attachment.php

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa Habari - Julai 15, 2015

Kingunge amewapongeza sana kina Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba ya Chama.

Kingunge anadai CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani.

Kwa mujibu wa Kingunge, kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine. Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya ila mimi nitasema.

Kingunge anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.

Anasema Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu; na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo.

"Nawaheshimu sana Mzee Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini nasikitika waliotoa michango ya kutotoa haki kwenye Kamati Kuu. Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6," alisema Kingunge.

"Tulipofika NEC - wajumbe wakasema mbona Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulikuwa tested baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 6,” aliongeza Kingunge.

"Mimi na Mwalimu tulishangaa kuona Lowassa anakubalika kiasi kile, Wajumbe wa Kamati Kuu walikuwa kimya na kushindwa kutetea mapendekezo yao. Mwalimu na Mimi ikabidi tuingilie kati na kusaida K'Kuu, tulifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa NEC na wagombea wakaanza kujieleza," aliendelea kuongeza.

Kingunge ameendelea kudai kuwa, wote wakati huo walikubaliana kwamba NEC ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo ya Kamati Kuu.

"Safari hii tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi, lakini haikutumika busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na “KITENGO”. KITENGO kilitoa maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki yake ya msingi ndani ya Chama.

"Kuna watu wananiuliza kwamba Lowassa Fisadi, na wewe mzee unamuunga mkono, sasa ningependa kusema hivi:

"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.

"Lowassa sio kwanza kuwajibika kisiasa, ktk awamu ya kwanza ya Mwalimu - kuna viongozi wa kisiasa waliuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.

"Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.

"Yote haya yalipangwa na 'KITENGO' kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” aliendelea mzee Kingunge.

Kwa mujibu wa Kingunge, Wilaya ya Monduli ni moja ya wilaya ambayo mambo ya Chama yanaenda vizuri sana, na Kinana alimsifu Lowasa kwa hilo kuwa amekitumikia chama.

Kingunge anadai Lowassa amekuwa mtendaji mzuri hata serikalini, kila sehemu aliyopitia alionyesha namna alivyoweza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Anadai mradi wa maji wa Ziwa Victoria, walishindwa wakoloni lakini limewezekana chini yake Lowassa akiwa waziri wa maji.

Amesema Lowassa kila alipoenda amefanya vizuri, na huu mchakato huu wa juzi ndani ya CCM umeonyesha wazi Lowassa anapendwa na watu.

"Zipo hadithi za kijinga kwamba watu wanaojitokeza wamepewa pesa, ni mawazo ya watu waliofilisika. Watu wanamlilia Lowassa hawamjui, hizo zote pesa zote anatoa wapi? Ana kiwanda cha pesa - hata angekuwa Bakheresa asingeweza!” alisema mzee Kingunge.

Mzee Kingunge alisema Lowassa ana kila sifa ya kuwa Rais na mwenyekiti wa Chama, mwingine yeyote inabidi ajifunze sana haya. Akasisitiza kuwa 'Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu.

"Yalitokokea Dodoma yametia doa kubwa ktk historia ya Chama chetu chenye kuheshimika sana nje na nchi kiujumla. Nchi ili itengamae lazima chama kinachoongoza kijiendeshe kwa misingi ya haki na demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa. Yaliyotokea Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki - wagombea walipaswa kusikilizwa kwenye Kamati kuu, walivunjiwa heshima na kunyimwa haki…” alisema mzee huyo.

"Chama kilichofanya maamuzi ya Dodoma hakikuwa chama kinachozungumziwa kwenye Katiba. Nawaomba viongozi wetu warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM. Kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.” alisema mkongwe huyo ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa mzee Kingunge, pamoja na haya yote lakini Chama lazima kiendelee. Amesema CCM imempata mgombea, ndugu Magufuli, maneno yake ya leo hayamhusu yeye, yeye hakuwepo ktk 'KITENGO' cha kuharibu mambo.

Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.

Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.

Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.

Mzee huyo amedai Lowassa pia aliwashinda wote waliomtaka kuvua gamba na akaendelea kubaki ndani ya Chama.

Kingunge ameulizwa wakati wa Richmond alikuwa mbunge lakini hakuonekana kumtetea Lowassa, kwanini? Amedai 'Vitu vingine havipaswi kusema hadharani, niliona mambo yameharibika, nikakaa na Lowassa nikamshauri awajibike kisiasa.’

Ameulizwa kama ana mpango wa kurudisha kadi ya Chama kuonyesha kutokuridhishwa na uvunjifu wa katiba ya Chama; akajibu 'Siku nikitaka kurudisha kadi yangu nitawaambia, mimi kadi yangu namba 8 na nilihusika ktk kuunda chama hiki, nikifikia maamuzi nitasema.’

Mwisho amemalizia kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”

Asanteni
Mzee kingunge,anataka nin sasa!Magufuli anakubalika zaid ya huyo amtakae yeye!
 
Malinyingi naona unaandika vitu vya ajabu. Ukweli ni Ukweli tu na unatabaki kuwa ukweli tu. Lowassa ni Fisadi kabisa lakini bado ni mwanaCCM muaminifu kwa chama chake. CCM ilipaswa kufuata kanuni, taratibu na katiba yake katika kumwondoa Lowassa na sio kufanya uhuni kama ule.

Kuhusu Zitto ni kweli ni Msaliti kwa CHADEMA dhambi mbaya zaidi katika uaminifu lakini bado kanuni, taratibu na Katiba ya CHADEMA ilitumika kumfukuza.

Alichokisema Mzee Kingunge ndio ukweli wenyewe, na utabaki hivyo hivyo siku zote. Kama humpendi Mzee Kingunge hilo ni sawa, lakini jaribu kuupenda hata ukweli wake.

Una akili kuliko Shein
 
Last edited by a moderator:
Mwakyembe: (Kwenye Richmond saga bungeni) ... ombeni kanuni zitenguliwe ili tuwasilishe upya taarifa yetu ili tuseme na siri tuliyoificha ili kuikoa serikali isiporomoke yote..."

Kingunge:"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu..."

 
Kingunge is just retiring the amount of money received from EL.

Kama anasema wananchi wamedharauliwa....mbona hakuwa mstari wa mbele kutetea maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba? (Double standard)

Wanasiasa ni waongo sana....anafanya yote haya kumridhisha EL kuwa wapo pamoja ( moyoni hayupo hivyo)

Naupenda msemo huu " kunya anye kuku akinya bata kahara"......
 
Huyu mzee sije kuwa hii yote ni mwanzo wa kampeni mpya? Lowasa labda anataka kugombea kupitia chama tofauti na CCM na huu ndio wanzo wakumsafisha, haiwezekani kwa mwanasiasa mzoefu kama kigunge kuamua kufa na Lowasa. tumeona kwa kina Sophia walivyorudi mbio, Tusubiri soon tutasikia EL anapeperusha bendera ya ACT!
 
Mtu huhitaji kuwa na darubini kuona kwamba mchakato wa CCM ulikuwa wa kihuni na usio wa kidemokrasia.

Hao 33 waliokatwa walikatwa kwa vigezo gani? Walipigiwa kura?

Au walikatwa kwa uamuzi wa watu flani flani tu kwamba huyu na yule hawafai?

Licha ya kwamba Kingunge anaonyesha ni mnafiki lakini kwenye hoja yake ya msingi ana hoja.


Kwenye hatua ya kwanza huwa hamna kupiga kura majina yote yanachukuliwa na kuangaliwa moja baada ya jingine na wale wote wenye tabia mbovu mbovu na ambao Tume ya maadili inaona hawafai huwa majina yao hayarudi, wale ambao majina yanarudi ndio hupigiwa kura sasa, nilivyoelewa mimi!
 
Sasa aone utamu wa kuvuruga taratibu na mchakato.

Kingunge ulishiriki kuvuruga mchakato wa katiba pendekezwa... Sasa usilalamike, muosha uoshwa.

Kweli kabisa....kula tano
 
Back
Top Bottom