Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kuna watu wanasema ccm inakufa mwaka. Lakini hawajui nini kinachoiweka ccm hai, imara na ambacho kinachowaunganisha viongozi wa ccm. Uhai, uimara na umoja wa ccm unasababishwa na UFISADI. Bila ufisadi wa viongozi wa ccm, hakuna uimara tena. Kupiga vita ufisadi ni kuiua ccm.
 
anayedhani kuwa chama cha Mapinduzi hakiongozwi kihuni anasahau, aliyofanyiwa Lowasa ya ukosefu wa heshima na kudharauliwa wameshafanyiwa watu wengi, Kolimba (late), Mzee Jumbe, Mzee Moyo, Mansour Y Himid, Prof. Kighoma Malima (late), sasa Mzee Kingunge asubiri kugeuzwa jina na yeye, uhuni na uharamia uendelee
 
Mchaka mchaka chinja aliselema alija Magufuri njoo Mwanza tunakusubiri kwa hamu kubwa sana njoo bana njoo nyumbani bana bibi anaumwa njoo njooo huku bana
 
Haya mengine ni mazungumzo baada ya habari,hivi mnafahamu kwamba nyumbani kwa magufuli chato kwa mwaka sasa panalindwa na wanajeshi Wa jwtz! Nani aliamrisha apewe huo ulinzi kama si amiri jeshi mkuu?

Magufuli alifiwa na binti jk aliacha ziara ya ulaya anakokupenda akaenda chato ,mawaziri wangapi wamefiwa hajaenda zaidi ya kuwapa pole tu,kiufupi jk alimuandaa magufuli na jaji
Ramadhani ambae kilichomcost ni nafasi yake na msimamo Wa tume ya katiba
 
sawa Mzee Kingunge mbona mchakato wa katiba haukufuata taratibu haukusema??
 
Niliamini na nitaendelea kuamini kuwa Lowassa hafai na hakufaa kuwa mgombea wa CCM hata kama mimi si mwanachama wala si mpenzi wa CCM. Niliamini pia kuwa jina la Lowassa litakatwa hata tano bora asingefika. Ndicho kilichotokea. Kwanini niliamini hivyo? Kwanza alikuwa tayari ana afya mbovu. Pili alikuwa anatumia njia haramu kusaka uraisi wa nchi. Tatu ana visasi jambo ambalo niliamini kuwa hata kama Kikwete hawakukutana barabarani lakini suala la nchi lazima lipewe kipaumbele kuliko urafiki. Nne, nchi hii isingekuwa salama kwa Loawassa kuwa rais na lakini kubwa zaidi CCM ingekuwa chama cha upinzani kwa asilimia 90% niliamini hivyo. Tano, Lowassa alikuwa anatumia vitisho vingi kuwatisha watu wa maamuzi. Hili lilikuwa kosa.
KURA LIKE NYINGINE TENA,
Mkuu Hata mimi nilikuwa naamini haya uliyoyaandika japo kutokana na ushabiki mwingi kuna wakati nilikuwa nafikiri huenda kuna kitu labda wengine wanaona mimi sioni mpaka napinga hivi. Baada ya kutafakari nikaona kuwa niko sahihi!
 
kwa hiyo mama yako angepewa pesa angefanya hivyo hivyo kama kingunge ?au angetumia njia nyengine ku justify..

Muulize kwanza zile nilizompa mama yako ali justify vipi. Labda wewe ndiyo tunda la justification!
 
Hata bunge la katiba ccm walivuruga,ni chama cha watu fulani mifukoni
 
bora ujiongeze mapemaaaaa. kwani lowassa ndio ana hati miliki ya akili zako! tooootooooo:Cry::Cry::Cry:
 
Kama Kingunge asingekua na mgombea angeheshimika sana lakini kwa sasa atadharaulika sana hakuna atakaye msikiliza, huyu ni mnafiki.

Yeye alihusika sana kuweka utaratibu mbovu wa kuingia CCM alishauri kwa JK enzi hizo kwamba ili kua Mwanachama lazima mtu asome miezi 3 yeye na JK walikua miungu mtu tena alikua mnoko sana kuwasema vibaya wenzake kwa JK. Enzi zimebadilika Ubungo haitarudi tena mikononi mwake atulie wakati umepita, alisaidia sana kujenga makundi ndani ya CCM kwa maslahi binafsi.

Kamati ndogo ya maadili ile ya watu 5 ndiyo inafanya kazi ya kushauri lakini kamati ya Usalama na maadili inaruhusiwa kupunguza kwa sababu inaongozwa na Mwenyekiti wa Chama, kwa hiyo hakuna uhalali wa kusema hayo, lugha nzuri ya kumwambia huyu Mzee ni kwamba aache kuropoka muda wake umekwisha.
 
Leo Mzee Kingunge kaongea na Vyombo vya Habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.

Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba - kukata majina ya wagombe.

Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.

Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.

Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.

attachment.php

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa Habari - Julai 15, 2015

Kingunge amewapongeza sana kina Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba ya Chama.

Kingunge anadai CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani.

Kwa mujibu wa Kingunge, kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine. Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya ila mimi nitasema.

Kingunge anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.

Anasema Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu; na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo.

"Nawaheshimu sana Mzee Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini nasikitika waliotoa michango ya kutotoa haki kwenye Kamati Kuu. Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6," alisema Kingunge.

"Tulipofika NEC - wajumbe wakasema mbona Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulikuwa tested baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 6,” aliongeza Kingunge.

"Mimi na Mwalimu tulishangaa kuona Lowassa anakubalika kiasi kile, Wajumbe wa Kamati Kuu walikuwa kimya na kushindwa kutetea mapendekezo yao. Mwalimu na Mimi ikabidi tuingilie kati na kusaida K'Kuu, tulifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa NEC na wagombea wakaanza kujieleza," aliendelea kuongeza.

Kingunge ameendelea kudai kuwa, wote wakati huo walikubaliana kwamba NEC ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo ya Kamati Kuu.

"Safari hii tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi, lakini haikutumika busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na “KITENGO”. KITENGO kilitoa maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki yake ya msingi ndani ya Chama.

"Kuna watu wananiuliza kwamba Lowassa Fisadi, na wewe mzee unamuunga mkono, sasa ningependa kusema hivi:

"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.

"Lowassa sio kwanza kuwajibika kisiasa, ktk awamu ya kwanza ya Mwalimu - kuna viongozi wa kisiasa waliuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.

"Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.

"Yote haya yalipangwa na 'KITENGO' kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” aliendelea mzee Kingunge.

Kwa mujibu wa Kingunge, Wilaya ya Monduli ni moja ya wilaya ambayo mambo ya Chama yanaenda vizuri sana, na Kinana alimsifu Lowasa kwa hilo kuwa amekitumikia chama.

Kingunge anadai Lowassa amekuwa mtendaji mzuri hata serikalini, kila sehemu aliyopitia alionyesha namna alivyoweza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Anadai mradi wa maji wa Ziwa Victoria, walishindwa wakoloni lakini limewezekana chini yake Lowassa akiwa waziri wa maji.

Amesema Lowassa kila alipoenda amefanya vizuri, na huu mchakato huu wa juzi ndani ya CCM umeonyesha wazi Lowassa anapendwa na watu.

"Zipo hadithi za kijinga kwamba watu wanaojitokeza wamepewa pesa, ni mawazo ya watu waliofilisika. Watu wanamlilia Lowassa hawamjui, hizo zote pesa zote anatoa wapi? Ana kiwanda cha pesa - hata angekuwa Bakheresa asingeweza!” alisema mzee Kingunge.

Mzee Kingunge alisema Lowassa ana kila sifa ya kuwa Rais na mwenyekiti wa Chama, mwingine yeyote inabidi ajifunze sana haya. Akasisitiza kuwa 'Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu.

"Yalitokokea Dodoma yametia doa kubwa ktk historia ya Chama chetu chenye kuheshimika sana nje na nchi kiujumla. Nchi ili itengamae lazima chama kinachoongoza kijiendeshe kwa misingi ya haki na demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa. Yaliyotokea Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki - wagombea walipaswa kusikilizwa kwenye Kamati kuu, walivunjiwa heshima na kunyimwa haki…” alisema mzee huyo.

"Chama kilichofanya maamuzi ya Dodoma hakikuwa chama kinachozungumziwa kwenye Katiba. Nawaomba viongozi wetu warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM. Kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.” alisema mkongwe huyo ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa mzee Kingunge, pamoja na haya yote lakini Chama lazima kiendelee. Amesema CCM imempata mgombea, ndugu Magufuli, maneno yake ya leo hayamhusu yeye, yeye hakuwepo ktk 'KITENGO' cha kuharibu mambo.

Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.

Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.

Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.

Mzee huyo amedai Lowassa pia aliwashinda wote waliomtaka kuvua gamba na akaendelea kubaki ndani ya Chama.

Kingunge ameulizwa wakati wa Richmond alikuwa mbunge lakini hakuonekana kumtetea Lowassa, kwanini? Amedai 'Vitu vingine havipaswi kusema hadharani, niliona mambo yameharibika, nikakaa na Lowassa nikamshauri awajibike kisiasa.’

Ameulizwa kama ana mpango wa kurudisha kadi ya Chama kuonyesha kutokuridhishwa na uvunjifu wa katiba ya Chama; akajibu 'Siku nikitaka kurudisha kadi yangu nitawaambia, mimi kadi yangu namba 8 na nilihusika ktk kuunda chama hiki, nikifikia maamuzi nitasema.’

Mwisho amemalizia kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”

Asanteni

Sometyms the end justify the means. Kwa kukiuka hizo taratibu tumeweza kumpata mgombea asie na makundi wala si fisadi kama maamvi. Hata kama mapungufu si kama ya edo au membe. I pray to God awe na speed ile ile na in three years nchi itapata mwelekeo.
 
Haya mengine ni mazungumzo baada ya habari,hivi mnafahamu kwamba nyumbani kwa magufuli chato kwa mwaka sasa panalindwa na wanajeshi Wa jwtz! Nani aliamrisha apewe huo ulinzi kama si amiri jeshi mkuu?

Magufuli alifiwa na binti jk aliacha ziara ya ulaya anakokupenda akaenda chato ,mawaziri wangapi wamefiwa hajaenda zaidi ya kuwapa pole tu,kiufupi jk alimuandaa magufuli na jaji
Ramadhani ambae kilichomcost ni nafasi yake na msimamo Wa tume ya katiba

Jk hajawahi kumtaka MAGUFULI ....MAGUFULI amekuwa akipewa ulinzi tangu wakati wa Mkapa ..ni kawaida ..kwa PSU- Kitengo cha ulinzi wa viongozi wa wanaofanya security risk assessment kwa viongozi NA watu wengine muhimu ...NA ikionekana wazir I au kiongozi huzika Ana maadui basi ni jukumu la Kitengo kuagiza ulinzi stahiki ...level ziko Kama nne kwa kuangalia tishio .......NA eneo husika
MAGUFULI ni Kati ya mawaziri ambao wana maadui NA wana ulinzi ....wazi au wa Siri ..

Eneo Kama chato kuna Wimbi kubwa la wahamiaji haramu NA ujambazi kadiri DSO NA OCD wanavoweza kuona wanaweza kutoa ulinzi kwenye maeneo muhimu ..kwa kupitia chombo chochote cha ulinzi NA usalama ...Mfano mabank,Nyumba za Ibada...Nyumba za viongozi NA watu wengine maarufu wilaya kadiri ya ripoti ya usalama wa eneo husika ....

Kikatiba hata Mimi NA wewe tunaweza kulindwa Kama maisha yetu yanatushiwa ......,kuna wakati Kitengo kilitoa walinzi kumlinda Reginald Mengi kwa KUWA aliropoti ametishiwa kuuliwa NA Alkarim wa CTN ..ugomvi wa kuinesha mpira ..Hadi mengi akaweka TV ya bure Mnazi Mmmoja ....Augustine Mrema aliridhika NA ripoti ya usalama aliyopewa wa tishio kwa bwana mengi NA akamshauri rais mwinyi aruhusu mengi apewe ulinzi wa state
 
mtu makini aliemptisha mkapa 1995 badala ya jakaya au karume 2000 badala ya bilali. kazoea kufanyia wenzake zengwe safari hii kisu cha mazingaombwe kimemkata anaruka ruka kama bisi kweye kikaango. wamekatwa watu zaidi ya 30 lowassa ni kama wanachama wengine. kaaa kimya babu wa maslahi
 
Unajua haya majitu siku zote tunasema wawe wanaweka sheria na taratibu zitakazotoa haki kwa wote. Wao siku zote wanadhani kuwa wayafanyayo ni kwa ajili ya kuwanyima haki wapinzani, matokeo yake ndiyo haya. Yalimkuta Sumaye, Salim nk, leo yamemuangukia Laigwanan. Bado yataenda kupitisha katiba mbovu yakidhani ni kuwakomoa wapinzani, matokeo yake yanakuwa ya kwanza kujeruhiwa nayo. Shame upon you ------.
 
Bado sijaelewa kuhusu yule Jaji Augustino Ramadhani ambaye tuliaminishwa kwamba hana kashfa je ni ithibati gani zilizotumika kumdhalilisha kiasi hiki? Na wale waliomshawishi kuchukuwa fomu wanajionaje?

Jaji hadhi yake imeshuka sana na hiki ni kiburi na uroho wa madaraka alionao kutoitambuwa hadhi ya Jaji. Hili ndio jinga kuliko wote.


Tatizo kubwa linaanzia katika mfumo wa upatikanaji/uteuzi wa hawa majaji unafikiri wakiombwa wajipake kinyesi hata kama wanaona unafikiri watakataa!!?.Mfumo mmbovu huo.
 
Hata Kingunge mwenyewe ni batili. Mtu gani haamini wala biblia takatifu wala Quran tukufu. Tunajua kwa nini anashabikia hiyo kambi sababu ni kwamba mwanaye Kinjekitile ni msafirisha madawa ya kulevya mkubwa. Na katika wagombea ambao wangemsaidia wasimkamate mwanae ni Lowassa tu kwa sababu naye ni Fisadi.
hee!as of now huyo msafirisaji wa madawa yupo jela au uraiani?
 
Katikati ya Maneno ya huyu Mzee Edo hatoki CCM anachotaka Tingatinga akapige magoti ili kuonyesha nguvu yake na yeye ahakikishiwe maslahi yake hizi ni siasa chafu
 
Back
Top Bottom