Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

 
Binafsi najisemea kuwa watanzania weng hatujui matukio na hatuchukui muda wetu kujisomea na kufuatilia mambo. Ndo maana tukio hili linachukuliwa kirahisi sana na linamaelezo meng ya tofauti tofauti na mepesi. Ukisikiliza shuhuda mmoja mmoja utaamini haya niandikayo pia ukifuatilia comment za watu. Mtu anachukulia bunduki n kama manati na mtu anachukulia mwalifu hasa wa kutumia silaha kama kibaka wa mfukoni.

Mtu anaona kama askari kama si watu ila wajinga flani na wazembe nyakati zote. Ila nature ya askari na majesh yote yaliyo kwenye sare rasmi huwa n watu wa lawama sana na ni target rahisi sana maana wanaonekana na kufahamika kirahisi tofauti na wasiona na sare.
Kilichowakuta askari wa uingereza. Ufaransa na marekan pale iraq nadhan wajuvi wa mamabo watakuwa wanaelewa nn kilikuwa kinawaponza.

Yote kwa yote tujifunze kuviheshmu vyombo vyetu vya ulinz na usalama maana naamin sote tunaopiga kelele mitandaon tungepewa silaha alafu ndo tuwe katka utekelezaji wa kazi ile asilimia kubwa wangekimbia maana ogopa sana bunduki ambayo milio yake ukiisikia unajua umeelekezewa wewe mtutu wake. Pili eneo mapambano huwa linatisha zaid ya vile tumeona kwenye video. Pia tukumbuke wakat mtu unapambana wakati huo unakuwa na familia tena unaitegemea nayo inakutegemea zaid.

Nihitimishe kwakusema kama hujawahi shuhudia maganda ya risasi yakidondoka karibu ya mwili wako kamwe huwezi jua meng kuhusu matukio ya utumiaji wa silaha. Na kama hujawahi kuwa mhanga wa kutekwa kwa kutumia silaha huwezi jua hofu inayokuwa mioyon mwa watu walio na uhai na roho moja.
Tuombee aman nchi yetu tuombe matukio kama haya yasijitokeze katka nchi yetu.
 
Alivopora silaha akawaua hao police aliowapora silaha.? Hao walioporwa walikuwa wangapi na wameuawa wangapi.? Jumla ni Vifo vingapi kujumlisha na wale wanne waliouawa wakati wa kushambuliana.?
 
Unayajua mazingira yaliyopelekea wao kuporwa hizo silaha?

Vipi kama hao askari walikuwa ambushed na huyo jamaa akafanikiwa kuwaua au kuwadhuru na hivyo kuweza kuzichukua silaha walizokuwa nazo kiurahisi zaidi?

Ni rahisi sana kukosoa ukiwa umekaa mbali na eneo la tukio tena baada ya kupita masaa tele kuliko ungekuwepo hapo huku ukishuhudia tukio in real time.
 
Inawezekana hilo pia
Ila Gaidi kaacha kushambulia Ubalozi na wananchi anawaambia ondokeni pia kuongea na yule mtoto na kuwaambia madereva waondoke na magari yao
Ugaidi upo ila hii sio mbinu za kigaidi labda iwe mbinu mpya...
Mkuu ugaid n mpana sana na usijiwekee mpaka katika mambo nyeti kama haya. Gaid ama ugaid haujawah taki kikubwa ila kama lililotokea. Kwa wakati wako jitahid kusoma sheria ya ugaidi pia kujifunza viashiria vya ugaid namna ugaid unavyopenya.pia na malengo ya magaidi.
 
Nipe majibu yako baada ya kuchunguza
Ameshuhudia ila mengne yanamaswali. Maana tulichokiona kwenye video na anachokisema kunasehemu vinakinzana na hii n kwa kawaida kwa binadamu kutaka kuonekana wameshuhudia kutoka mwanzo mpaka mwisho
 
Alivopora silaha akawaua hao police aliowapora silaha.? Hao walioporwa walikuwa wangapi na wameuawa wangapi.? Jumla ni Vifo vingapi kujumlisha na wale wanne waliouawa wakati wa kushambuliana.?
Mjuba ata kufuatilia huwezi..unachosha watu
 
Hata Kama alidhurumiwa kitendo cha kushambulia polisi na kubeba silaha ya kivita alijiweka kwenye nafasi ya kushambuliwa pia

Angeenda kushitakiwa wapi, wakati polisi ndio huko wanakaa na mahabusu zaidi ya miezi miwili bila kuwapeleka mahakamani? Hao polisi sio ndio hao wanapiga raia wema kwa kuagizwa na watawala majizi ya kura?
 
Hata kama madai yako ni kweli, je kuna haja ya kuchukua hatua za kipumbavu kama alivyochukua mwenzako huyu unayejitahidi kumtetea? Jicho kwa jicho wameliteketeza gaidi la kisomali
 
Mjuba ata kufuatilia huwezi..unachosha watu
Siwachoshaje watu wakati bado cjapewa majibu ya maswali yangu.? Ingekuwa mtu amenijibu lkn bado nikaendelea kuuliza hapo ndo ungesema nachosha watu
 

Polisi wamejengewa hii tabia ya dhuluma na watawala waliopo madarakani, kama hawa hawa polisi ndio wanaotumika na watawala waliopo madarakani ili kupora chaguzi, unategemea kuna wa kumzuia mwenzake? Kinachofanyika kwa polisi na watawala hawa ni kile waswahili wasemacho, nilinde kwa jua, nikulinde kwa mvua. Hapo polisi wanahakikisha ccm wanaingia madarakani kwa kupora chaguzi, kisha ccm wakishaingia madarakani wanawaachia polisi wale rushwa na kupora wananchi.
 
Ameshuhudia ila mengne yanamaswali. Maana tulichokiona kwenye video na anachokisema kunasehemu vinakinzana na hii n kwa kawaida kwa binadamu kutaka kuonekana wameshuhudia kutoka mwanzo mpaka mwisho
Wabongo tunaupiga mwingi kwenye kutoa ushahidi
 
kweli usilolijua ni kama usiku wa giza, kuna mama mmoja nimemsikia anasema jamaa ALIKUA ANAONGEA KIISLAMU, sijui ndio lugha gani hiyo!!!? Anyways ya Mungu ni mengi.
 
Mkuu wacha kutetea mapolisi...! Jamaa yuko kwenye cross fire lakini yanamkosa yanapiga chini, mengine yapo kwenye range kabisa jamaa anatembea wala hajifichi na yanamkosa! Risasi kibao zinapigwa kama hawana mafunzo πŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈπŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈπŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈπŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…