Ni tukio la kushangaza na lenye maswali mengi kwa sasa hivi hakuna ajuae Ukweli ngoja tusubiri taarifa ya jeshi la polisi.
Mpaka muda huu tayari ndugu wa Bwana Hamza wamechukulia wako polisi kwa mahojiano zaidi.
Lakini tujiulize
1. Hamza ni nani ?
2. Ni raia wa Nchi gani ?
3. Anafanya Kazi gani ?
4. Kama tukio hili tutaliweka kwenye kundi la Ugaidi tujiulize kwanini shumbulio lake liliwalenga Askari polisi pekee licha kuwa na nafasi ya kuwadhuru raia waliokuwepo karibu nae mfano kwenye Daladala.
4. Ukitazama vizuri baadhi ya video utaona jamaa alikuwa anashambulia na kukwepa (swali) mafunzo haya aliyapata wapi au tuseme ameiga kwenye Movie??
......................
Huo ni Upande mmoja wa maswali lakini Kuna upande mwingine umejaa tetesi kwamba huyu Bwana Hamza ana mgodi huku Chunya mkoani Mbeya ambao waliachiwa na Marehemu Baba yao. Tetesi hizi zinadai kwamba siku ya tukio Bwana Hamza alikuwa kwenye mipango ya kufanya Biashara ya Madini na suala hili Kuna maafisa wa jeshi la polisi walikuwa wanalijua sasa basi Kuna kitu cha ajabu Sana kikatokea na kukwamisha hiyo biashara. Ni kitu gani hicho ngoja kwanza jeshi la Polisi limalize Kazi yake May be litatueleza ukweli narudia tena May be.
**********
REJEA.
Nenda kwenye Post za Millard Ayo (Instagram) Kuna Dereva tax anaefanya shughuli zake karibu na nyumbani kwa Akina Hamza amekiri ni kweli Hamza na ndugu zake wengine waliachiwa Mgodi huku Chunya mkoani Mbeya na Marehemu Baba yao.
Lakini pia Kuna kipande cha ujumbe amekipost Le Mutuz nitakiweka hapa ili uunganishe matukio.
Swali la Mwisho. Hamza ni kichaa au ana tatizo la Akili ??
Siku chache zilizopita Kuna watu walikamatwa na Madini feki huko Dar es laam. Please hii nayo usiiweke mbali ukianza kuunganisha matukio
View attachment 1908534