Je TIDDO MHANDO wa BBC ndiye huyu anayedhalilishwa na akina Lowasa hapa TBC 1? Je si alifanya vizuri tu kule BBC, nini amepewa hapa mpaka amekuwa kama Zuzu? Sasa hivi TBC 1 hata kule DSTV inaonyesha ovyo tu, inakatakata mpaka aibu. Ukifungulia KBTV kwenye DSTV iko clear sana! Tatizo ni uroho na kuhemea misaada, vinginevyo Tido angekuwa na akili ni vyema astaafu, kuliko aibu hii anayo jitia kwa kulamba miguu ya kina Lowasa na wenzake.
Hivyo kutembea nje, kusoma nje, kufanya mashirika ya kimataifa is one, na kuwa na moyo wa uzalendo ni kingine....tusimpokee mtu kwa CV yake. Kama CV yake nzuri, aombe kazi pale BOT, akawasaidie kuplan uchumi upya, lakini sio kwenye siasa ambako unakaa kikao kimoja na wasanii kama akina Hadija Kopa, halafu utegemee kutumia PHD yako vizuri....