KINSHASA ARENA :DR CONGO ikijenga Uwanja mkubwa wa ndani Afrika Mashariki na kati

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,764
Reaction score
3,230
Wakati huku serikali ikiwa bado inajifkiria,nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaendelea na Ujenzi wa Arena kubwa Afrika Mashariki na Kati.

Arena hiyo itakuwa ikiitwa Kinshasa Arena,na itakuwa na uwezo wa kuchukua watu 20,000.
Ujenzi huo ulianza mwaka 2023 unatarajiwa kukamilika mwaka huu.

Kongo inazidi kujipambanua.
images-2.jpeg

Ujenzi ukiendelea
images-1.jpeg

Muonekano wa mwisho itakavyokuwa
 
Kupanga ni kuchagua.
Kipande cha nchi kimekaliwa na majeshi ya kigeni wenyewe mko bize kufikiria arena kubwa ya kufanyia burudani.
 
Hauwezi kufanya vyote kwa wakati mmoja...
Now Kongo inapiga hatua ,uchumi unakua kwa kasi.
 
Ni kweli huwezi kufanya vyote kwa wakati mmoja, lakini ilipaswa kipaumbele kuwekwa kwenye ulinzi wa mipaka ya nchi.
Haiwezekani kijitu kinapora ardhi ya nchi yenu nyi mko bize kujenga kumbi za starehe, wakati huo huo mnaomba majeshi ya kikanda yaje yapigane kwa niaba yenu.
Hiyo ngumu bro.
 
Mkakati wa mda mrefu unahitajika,
1. Kufufua uchumi uchumi ni jambo la kwanza
2.Kuonesha matumizi ya fedha zinazopatikana kutokana na rasilimali zao
3. Wananchi wajionee faida ya amani na rasilimali zao ni zipi
4. Hii inarudisha morali ya watu ,hata ukisema unaenda vitani,unapata watu

Angalia mfano wa Azberijan ilivyorudisha ardhi yake baada ya miaka 10+ tangia washindwe vita
 
Huwezi kuendesha miradi ya kufufua uchumi wakati mko vitani.
Kabla ya chochote kipaumbele cha kwanza ni kupigana mpaka kukomboa nchi.
Linchi likubwa na watu zaidi ya milioni 100 wanasumbuliwa na kanchi ka watu milioni 6.
Kwakuwa kipaumbele chenu ni starehe
 
1.Korea Kusini mpaka leo hii wapo kwenye Vita na Korea kaskazini....na wamepiga hatua kuliko nchi yoyote Afrika
2. Azberijan imepiga maendeleo makubwa licha ya sehemu kubwa ya nchi yao ilikuwa chini ya Armenia
3.Japan ni ya nne kwa uchumi duniani licha ya kanakwamba kuna sehemu ya ardhi yao inakaliwa kimabavu na Urusi

Mifano ni ipo mingi sana...

Vita vinahitaji fedha ; Nchi inajenga miundombinu ya kuzalisha pesa...
Wakati wewe unawaza ni starehe tu,wenzako wanaona fursa ya kuzalisha fedha.
 
Huwezi kuendesha miradi ya kufufua uchumi wakati mko vitani.
Kabla ya chochote kipaumbele cha kwanza ni kupigana mpaka kukomboa nchi.
Linchi likubwa na watu zaidi ya milioni 100 wanasumbuliwa na kanchi ka watu milioni 6.
Kwakuwa kipaumbele chenu ni starehe
Sisi bana ya Congo pedeshee, yenye tunakula bata- mambo ya malisasi hatutakangi. Tunataka bajeshi ba inchi ingine baje baipiganie Congo, sisi tutabalipa madolaa/mafaranga.
 
Msigwa na Bashite wakiiona hii taarifa wataenda kumshawishi mama yao naye ajenge, halafu wanaujenga kwa gharama mara kumi yake. Na CAG akikakugua mahesabu na kuugundua huo ufisadi, hakuna watakacho fanywa.

Zaidi watapongezwa tu kwa kula vizuri kwa urefu wa kamba yao.
 
Back
Top Bottom