Pre GE2025 Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais ajae baada ya Samia lazima awe Mkiristo,hua tunakawaida ya kupokezana
 
Mnatuharibia nchi kwa ramli zenu hizi. SSH kakwambieni hatogombea 2025? Huyu Mwinyi ana tofauti gani, ukizingatia kule Zanzibar kwanza ndio ajamaliza vipindi vyake viwili kama ilivyo ada ya CCM.

Kimsingi hiki chama changu kimechoka kuongoza nchi. Ufisadi, ubabaishaji wa viongozi na mbaya zaidi unafiki wa wanachama wake kujipendeka kwa kusema uongo ili wapate teuzi kunakitafuna chama.
 
Mnatuharibia nchi kwa ramli zenu hizi.
Hizi sio ramli, ni trends readings, kusoma mielekeo, karibu ujifunze kusoma mielekeo uone ni mielekeo gani watu kama sisi tuliwawekea humu na ikaja kutokea.
SSH kakwambieni hatogombea 2025?
SSH hahitaji kumwambia mtu yoyote kuwa atagombea au hagombei 2025, kwasababu hata akipoupata urais, hakumwambia mtu yoyote kuwa anautaka urais wa JMT, ni imetokea tuu SSH akawa rais wetu ile March 17, 2021 lakini trends za SSH atakuwa rais wetu, watu wa trends, tuliziweka humu toka 2017!. Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020
Huyu Mwinyi ana tofauti gani, ukizingatia kule Zanzibar kwanza ndio ajamaliza vipindi vyake viwili kama ilivyo ada ya CCM.
Ni kweli utaratibu wa CCM ni rais kushika madaraka vipindi viwili, ila it's not fast and hard rules, no utaratibu tuu wa CCM, kipindi cha urais kwa mujibu wa katiba zote mbili ya JMT na ya ZNZ, urais ni miaka 5, anaweza kugombea kipindi cha pili lakini sio lazima, Ali Hasan Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kimoja tuu, akafuatiwa na Idris Abdul Wakil alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kimoja!, hivyo urais wa vipindi viwili sio lazima!.

Hata JPM, angekuwa anasoma jf na kuufuata ushauri wa humu, saa hizi angekuwepo!, watu tulimshauri humu asigombee kipindi cha pili na badala yake ampishe Samia, ni mwaka 2017 kwenye bandiko hili Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” Kisha 2020 kwenye bandiko hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Hivyo usiite hizi ni ramli hizi sio ramli na kwa taarifa yako mabandiko kama haya ndio mabandiko ya kusaidia nchi, na kuwasaidia viongozi wetu kujiandaa kisaikolojia kwa yajayo. Huwezi jua kama JPM angeusikiliza ushauri wa humu ile 2020 kuwa ampishe tuu Samia, you never know labda saa hizi angekuwepo!. Ndio maana nilipo isikia sauti hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke nikaileta ili kumsikilizisha mtu ili...

Siku zote nasisitiza humu kuwa kauli zinaumba!. Karibu utembelee hapa kuangalia baadhi ya hizi kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

P
 
Ndio mumepanga? Mistake kutuvurugia uchumi Kwa kuokoteza watu.

Samia kesha set momentom nzuri kabisa ya uelekeo wa Nchi Kwa Mageuzi aliyoyafanya kuanzia kwenye uchumi hadi Huduma za jamii.
 
Ngoja tuone 🙏🙏
 
Ukisoma post hii unaweza kudhani Dr. Mwinyi ni changamoto, kumbe wapinzani Wa Makonda Wa najaribu kutumia njia nyingi kutisha Mama. Kwa ufupi Dr. Mwinyi hatagombea, Makonda ndiye mwenezi wetu na atawacharaza Sana 2025. Upinzani jipangeni kupata jimbo hata moja itakuwa kama Ngamia kupenya kwenye sindano
 
Kivipi tena hili mbona liliibukia Bungeni?😆
Hapana, kwa mara ya kwanza bomb 💣 hili alilitegua Mbowe akiwa nje ya Nchi.

Baada ya uwasilishaji wake ndiyo likaenda Bungeni ambapo wakaanza kusema Mbowe mbaguzi kuleta Uzanzibari na Utanganyika.

Ila ni jambo lilitegwa Kimkakati sana bila Mama Kujua anawekewa Miiba kuelekea 2025
 
Mama Dkt Samia hana shida kabisa, ni muadilifu, mzalendo, mwaminifu, mchapa kazi, muungwana, mfis nchi, mpenda nchi, mwenye hofu ya Mungu, ni rais wetu mpaka 2050!
 
Mama Dkt Samia hana shida kabisa, ni muadilifu, mzalendo, mwaminifu, mchapa kazi, muungwana, mfis nchi, mpenda nchi, mwenye hofu ya Mungu, ni rais wetu mpaka 2050!
We ChawaWaMama , angalizo uchawa usizidi ukageuka kufuru, YULE YEYE AWAYE, akakasirika aka...
Kumpenda Mama na kumkubali ni jambo moja na kumpangia mpangaji ni jambo jingine!, hii joke ya mpaka 2050 is not a good joke!, it carries karmic consequences, kumpenda kwenu Mama kusimponze kama mlivyo mponza yule!.
P
 

[emoji897][emoji897]
 

Unajua Vijana tunajisahau Sana. Yaani mtu unakuwa chawa mpaka unayemfanyia uchawa ananuna.
 
Mwamba anatosha Sana. Tatizo lake 1 Tu. Hajasota ktk maisha yake, kakulia na kuishi kwenye maisha bora, so mashaka ni hayo
Kwenye kinyang'anyiro cha mgombea mwenza wa JPM, mwaka 2015 waliwahi kuchuana vikali na SSH. Kwa hiyo kama asingeshindwa na Samia, sasa hivi ndiye angekuwa Rais wa JMT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…