Angalizo kwa Wanabodi na Mode
Bandiko hili ni C&P kutoka kwa mwana JF fulani.
Kwasababu mwandishi ni member wetu humu na humu hajaileta, naomba ikitokea ameileta humu, then futa hili bandiko langu.
Nime C&P kwasababu mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kuandika humu kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 could be Dr. Hussein Mwinyi, kupitia bandiko hili
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Hivyo hoja kama hii inapotolewa na mwajeiefu mwenzetu, mwandamizi kama huyu, hivyo nimejikuta ni muhimu kuisambaza.
Paskali.
(Mwanzo wa kunukuu Barua ya...)
Kwa kiasi kikubwa, siasa za Tanzania zimejikita zaidi kwenye chaguzi, hususan uchaguzi mkuu. Kwamba vyama vya siasa hutumia muda mwingi kujiandaa na chaguzi kiasi kwamba kuna dhana kwamba haviwatumikii wananchi vya kutosha kutokana na hilo.
Lakini lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Na katika nchi za kidemokrasia, kushika dola kunawezekana kwa njia moja tu, yaani uchaguzi mkuu. Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kwa vyama vya siasa kujipanga vema kwa ajili ya chaguzi.
Na kwa chama tawala, kisipofanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya chaguzi zijazo, nafasi yake kama chama kinachoshika dola inakuwa hatarini.
Ni katika mazingira hayo ndio maana kumekuwa na maongezi mengi kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 japo bado miaka miwili hivi kabla ya uchaguzi huo. Na japo kuna chaguzi za serikali za mitaa mwakani, maongezi mengi ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba kuna jitihada zinafanyika huko Zanzibar kumwezesha Dkt Hussein Mwinyi kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2025.
Si tayari CCM “ina mgombea wake” 2025?
Naam. kwa mujibu wa utaratibu usio rasmi huko CCM, rais aliyepo madarakani anakuwa automatically mgombea pekee wa urais mwaka katika uchaguzi utakaomuingiza awamu ya pili ya urais wake.
Ilikuwa hivyo kwa Mkapa mwaka 2000, Jk 2010 na Magufuli 2020. Na inatarajiwa iwe hivyo kwa Mama Samia 2025.
Hadi wakati makala hii inaandikwa haijafahamika rasmi kwanini kuna mpango huo amba sio tu utapelekea “kuukoroga utaratibu huo usio rasmi wa Rais aliyepo madarakani kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo ili akamilishe ngwe zote mbili” bali pia utakuwa upinzani baina ya wanasiasa wawili kutoka Zanzibar.
Maandalizi yameanza
Taarifa zinaeleza kwamba tangu Zanzibar ijiunge na Tanganyika mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna kipindi ambapo upande huo wa Muungano umepokea fedha nyingi kutoka serikali ya Muungano kama kipindi hiki cha utawala wa Mama Samia.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa sehemu ya fedha hizo zimekuwa zikitumiwa na wanamkakati wa mpango huo wa kumwezesha Dkt Mwinyi kuwa mgombea mwaka 2025.
Licha ya ukweli kuwa maandalizi ya uchaguzi wowote hule huhitaji fedha za kutosha, yaaminika kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 utatawaliwa na matumizi makubwa ya fedha hasa kutokana na ukweli kwamba wanasiasa wengi wamepoteza mvuto machoni mwa wananchi na njia pekee ya “kupendeka” ni kumwaga fedha.
Mama Samia anawarahisishia kazi wapinzani wake ikiwa ni pamoja na mwanasiasa huyo wa Zanzibar
Kuna matukio mawili makubwa ambayo yanatarajiwa “kumsumbua” Mama Samia kati ya sasa na uchaguzi mwaka 2025. La kwanza ni suala la mkataba wa bandari ambalo japo “kwa nje ya CCM” linaonekana kama lilikuwa lina mwafaka miongoni mwa wana-CCM, ukweli ni kwamba sio tu lilizua mgawanyiko wakati wa mjadala bali pia limeacha makovu ambayo yanaweza “kukwanguliwa” pindi kampeni za urais zitaposhika kasi.
La pili ni hili la “Mama Samia kujichoma msumari mwenyewe” kwa kumteua Bashite kuwa katika mwenezi wa chama hicho, huku akifahamu fika kuwa kada huyo anachukiwa na wengi ndani na nje ya chama hicho.
Japo Mama Samia anatarajia kuwa Bashite atamsaidia kukabiliana na “wapinzani wake”, nguvu za kada huyo huko nyuma zilitegemea zaidi staili ya uongozi wa kibabe wa marehemu Magufuli, ambayo ni tofauti na satili ya uongozi wa Mama Samia, unless aamue kubadilika.
Hitimisho
Kuna msemo kuwa kwenye siasa, wiki moja ni sawa na uhai mzima (lifetime). Na kwa hakika, kati ya sasa Novemba 2023 hadi Oktoba 2025 ni takriban miaka miwili, na mengi yanaweza kutokea aidha kuimarisha dhamira ya mwanasiasa yeyote mwenye ndoto za kumpiku Mama Samia au urais wa Mama Samia ukaimarika zaidi kiasi kwamba yeyote mwenye ndoto za kum-challenge atakuwa anapoteza muda wake. (mwisho wa kunukuu)
Mwana if fulani.
C&P by Paskali
Update 1
Mchango very objective
Hizi sio ramli, ni trends readings, kusoma mielekeo, karibu ujifunze kusoma mielekeo uone ni mielekeo gani watu kama sisi tuliwawekea humu na ikaja kutokea.
SSH hahitaji kumwambia mtu yoyote kuwa atagombea au hagombei 2025, kwasababu hata akipoupata urais, hakumwambia mtu yoyote kuwa anautaka urais wa JMT, ni imetokea tuu SSH akawa rais wetu ile March 17, 2021 lakini trends za SSH atakuwa rais wetu, watu wa trends, tuliziweka humu toka 2017!.
Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020
Ni kweli utaratibu wa CCM ni rais kushika madaraka vipindi viwili, ila it's not fast and hard rules, no utaratibu tuu wa CCM, kipindi cha urais kwa mujibu wa katiba zote mbili ya JMT na ya ZNZ, urais ni miaka 5, anaweza kugombea kipindi cha pili lakini sio lazima, Ali Hasan Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kimoja tuu, akafuatiwa na Idris Abdul Wakil alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kimoja!, hivyo urais wa vipindi viwili sio lazima!.
Hata JPM, angekuwa anasoma jf na kuufuata ushauri wa humu, saa hizi angekuwepo!, watu tulimshauri humu asigombee kipindi cha pili na badala yake ampishe Samia, ni mwaka 2017 kwenye bandiko hili
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
Kisha 2020 kwenye bandiko hili
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Hivyo usiite hizi ni ramli hizi sio ramli na kwa taarifa yako mabandiko kama haya ndio mabandiko ya kusaidia nchi, na kuwasaidia viongozi wetu kujiandaa kisaikolojia kwa yajayo. Huwezi jua kama JPM angeusikiliza ushauri wa humu ile 2020 kuwa ampishe tuu Samia, you never know labda saa hizi angekuwepo!. Ndio maana nilipo isikia sauti hii
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke nikaileta ili kumsikilizisha mtu ili...
Siku zote nasisitiza humu kuwa kauli zinaumba!. Karibu utembelee hapa kuangalia baadhi ya hizi kauli umba
"Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
Amber light Mama alee wajukuze kwa Abduli?