Uchaguzi 2020 Kinyerezi, Segerea: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. Magufuli

Uchaguzi 2020 Kinyerezi, Segerea: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. Magufuli

Amelibagua Jimbo lake sehemu zenye madiwani wapinzani amewanyima maendeleo,hizi Jamii zinazotoka nchi jirani ni wabaguzi Sana na wakabila kiasili
Umesema kweli mkuu kimanga na kinyerezi wamepitia kipindi kigumu ila naye safari hii ana hali ngumu sidhani kama atatoboa maana hata kuupata ubunge ilikuwa bahati baada ya majina ya wabunge wote wa ukawa kuwepo kwenye ballot paper licha ya kutangazwa mtatiro kuwa ndiye mpeperusha bendera ya ukawa
 
Naona Kumbilamoto kaamua kuchomoa betri walichokuwa wanafanya upinzani
Kumbilamoto naye tunayajua mambo yake hapo Vingunguti na wafanyabiashara ya mbuzi. Unamuangalia unaona tu jinsi alivyo falafala unamtunzia heshima tu.
 
Ali
Umesema kweli mkuu kimanga na kinyerezi wamepitia kipindi kigumu ila naye safari hii ana hali ngumu sidhani kama atatoboa maana hata kuupata ubunge ilikuwa bahati baada ya majina ya wabunge wote wa ukawa kuwepo kwenye ballot paper licha ya kutangazwa mtatiro kuwa ndiye mpeperusha bendera ya ukawa
Alidanganywa na jiwe eti usipeleke maendeleo mitaa ya wapinzani Hali wote ni watu wake,kakumbuka shuka anajifanya ana kwangua barabara Hadi mitaani.Ajiandae kuisoma namba, atapigiwa kura na mitaa aliyoipendelea,mitaa aliyoisomesha namba asitegemee kupata kura
 
Ilani ipenyi akilini bila uongo mwingiii,Uchonganishi,ubaguzi,kufokea,na mademu .hii nini hiii
 
Amesema vijana wanateseka kwa kukosa ajira wenfine wamemaliza vyuo vikuu hawana ajira hivyo anataka ndani ya miaka mitano akipewa tenauraisi suala la ajira alishughulikie kwa nguvu zote. Amesema kama wameweza kujenga flyover hawezi kushindwa kuleta ajira kwa vijana.
Ni vizuri kama anatambua hili.
 
Rais hayupo consistency anapoelezea suala la kutatua changamoto za ajira....leo nimemsikiliza akisema kwamba endapo atachaguliwa tena basi tatizo la ajira litakuwa historia ......

Wakati sasa tunatega sikio atatatuaje ilihali yeye ndiye aliyefukuza kazi watu hovyo na kuuwa sekta binafsi ......

Ghafla akahama Mara oooh tuna gesi, tuna madini, tuna ndege tuna wanawake wazuri na wanaume wazuri..... Dah, nilichoka

Kitengo cha madaktari waliopo kwenye msafara wa rais itoshe kusema kwamba kuna tatizo kwa mgombea na kuna jambo halipo sawa .

Aidha wanaogopa kumwambia ukweli au mgombea hautaki ukweli huo,

28/10 watz wana jambo la kufanya.
 
CHADEMA Mgombea wao mnene Duh, ...
1602503376163.png




 
Huyu Magu yeye kazi yake kujenga tu madaraja reli na miundombinu mingine Tundu Lissu ukiwa Rais mteue awe waziri Wa ujenzi
Hata kuwa Waziri wa Ujenzi hafai kabisa maana alipokuwa Waziri wa Wizara hiyo ndo alikatisha kandarasi 3000 za ujenzi wa barabara na kuitia Serikali hasara kubwa bila kuwajibishwa. Haijulikani katika maisha yake amefanikiwa kwa lipi maana licha ya maneno mengi, sifa na ngonjera nyingi amepwaya kabisa kwenye nafasi ya Urais na itakuwa kilio na kusaga meno akipewa miaka mingine 5. Amekuwa mtu wa kubebwa tu kutoka nafasi moja hadi nyingine bila kuacha legacy ndo maana hata mafanikio yake kama mwalimu pia hayajulikani wala akiwa Mbunge labda anajulijana huko kwao tu.
 
Kiukweli Leo baba kajichanganya tunajua mazuri aliyofanya ni mengi lakini anatoa hotuba kama vile anamlaumu aliyekuwa madarakani kwa awamu inayoisha wakati ni yeye mwenyewe!!, Mara vitambulisho vitasaidia wajasiriamali wadogo kupata mikopo bila riba, how comes!! Vitambulisho havina ata majina wala picture ya MTU,
Na Yale maneno aliyoyasema kuhusu mgombea wa upinzani mhhh ingekuwa ni mpinzani ndo kayasema kuhusu mgombea wa ccm nahisi angeitwa kwenye kamati ya maadili,
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk John Pombe Magufuli leo anaendelea na kampeni zake katika jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo atanadi Sera na ilani za Chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, 28, 2020



=========
Hotuba ya Dkt Magufuli akiwa Segerea


Tunawashukuru viongozi wote wa dini kwa kuwa mstari wa mbele kuliombea Taifa hili pia namshurukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai.

Dkt Magufuli amesema kuwa aliekuwa Meya wa Dar es salaam kwa tiketi ya CHADEMA na kuhamia CCM amesema kuwa alipokuwa kwenye nafasi ya Umeya kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwakwamisha wana Dar es salaam, hivyo Magufuli amewataka wananchi wajifunze kitu kutoka katika hotuba ya aliekuwa Meya na wasirudie makosa.

Magufuli amesema anaijua vyema Dar es salaam kwa kuwa maeishi miaka mingi sana Dar es salaam tangu akiwa anasoma chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo anafahamu matatizo ya Dar es salaam hata ya wale wanaoishi mazingira magumu katika wilaya zote za Dar es salaam.

Amesema kuwa malengo yake yalikuwa ni kuzibadili wilaya zote za Dar es salaam kwa ujumla wake lakini walimchagua na kuwa kama wamemfunga miguu kwa kuchagua upande mwingine, hawakumpa uhuru wa kufanya kazi lakini leo mabadiliko yamepatikana lakini yamepatikana kwa tabu sana kwa kuwa wakwamishaji waliwaweka wao.

Anasema hata ile stendi ya Mbezi Luisi ilichukua miaka kadhaa kumpata mkandarasi lmpaka ikabidi aingilie kati kwa kulazimisha, amesema anajua wana Segerea wana UKonga wana Ilala wamejifunza vya kutosha, hivyo anaomba wampe kura za kutosha na wamchagulie wabunge na madiwani wa CCM halafu waje wamuulize ndani ya miaka mitano kitu gani kimekwama kukitekeleza.

Amesema anamshukuru baba wa taifa kwa kulijengea taifa la Tanzania utaifa na kabla alipigania uhuru na tukawa huru na kisha kufanya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania, na leo tunaendelea katika utaratibu huo na tupo huru lakini amesema kuwa huru kitaifa ni jambo moja lakini kuwa huru kiuchumi ni jambo lingine.

Dkt Magufuli amesema amefanya kazi na Mzee Mkapa kwa miaka yote kumi na anafahamu kwa nini barabara hazikuwa na lami, amesema watu walikuwa wanasafiri mpaka siku tano njiani na walianza kupanga mipango ya kutatua matatizo hayo.

Amesema yeye hakujua kuwa atakujua kuwa Rais na wala hakutegemea kuja kuwa Rais na hivyo Urais ameupata bila kutumwa na mtu bila kuhonga ndio maana kauli mbiu yake ilikuwa hapa kazi tu maana kazi hiyo alipewa na Mungu kama sadaka ya kuwafanyia kazi watanzania na walipoingia changamoto zilikuwepo.

Walipoingia tu kuna maeneo yakiuwa hayana amani, ukienda Bukoba ulikuwa huwezi kusafiri mpaka usindikizwe na polisi na sasa amekomesha na mabo yameanza kuwa mazuri kwa kukomesha vitendo vya kijamzazi.

Amesema la kwanza alipoingia madarakani ilikuwa ni kuhahakisha wanajenga amani na utulivu wa nchi hii maana bila amani hakuna jamboo unaweza kulifanaya. na ndio maana anaomba miaka mingine mitano ili akakomeshe kabisa changamoto zilizokuwa zimebakia.

Amesema katika utafiti uliofanya na benki ya dunia ulisema jiji la Dar es salaam lilikuwa linapoteza bilioni nne kwa sababu ya foleni na ndio maana wakaona lazima walifanyie mkakati wa kulitatua kama ujenzi wa barabara za juu kama Ulaya na daraja la Kwa Mfugale na wataendela kuona miradi inafumka zaidi.

Amesema wajasiriamali walikuwa wanasumbuliwa na wanamgambo kwa kunyang'anywa bidhaa zao na kufukuzwa kwenye maeneo ya biashara na hivyo yeye akaona atatue tatizo hilo kwa kuanzisha vitambulisho vya mjasiriamali na kuviita vitambulishi vya Rais kwa kuwa hakuna atakae vinyanyasa na wao kwa gharama ya 20,000/= wakawa huru kufanya biashara ndani ya mipaka ya Tanzania.

Amesema hiyo gharama ya elfu ishirini ni kutokana na gharama za utengenezaji wa vitambulisho hivyo, amesema pia wana mpango wa kuanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali kupitia vitambulisho hivyo kwa wajasiriamali kuunda vikundi.

Amesema yeye huwa anaumia sana kuona wazee na wakina mama wanasumbuliwa, huwa akiona mama anasumbuliwa anamkumbuka mama yake ambaye ni mgonjwa kitandani.

Amesema vijana wanateseka kwa kukosa ajira wenfine wamemaliza vyuo vikuu hawana ajira hivyo anataka ndani ya miaka mitano akipewa tenauraisi suala la ajira alishughulikie kwa nguvu zote. Amesema kama wameweza kujenga flyover hawezi kushindwa kuleta ajira kwa vijana.

Anachekesha kweli!!! Je, wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi kwanini hakukamilisha ujenzi wa barabara badala yake anang'ang'ania flyovers. Kitakachoweza kuondoa foleni ni kujenga barabara za pembezoni (feeder roads) sio flyovers. Hili ndilo litakuwa suluhisho sahihi kabisa kwa tatizo la foleni Dar es Salaam. Nyote ni mashahidi kwamba, pamoja na kujenga flyovers, bado tatizo la foleni ni kubwa sana. Na kwa kuwa hakuna namna ya kuweza kujenga feeder roads kutokana na ukweli kuwa maeneo mengi ambako barabara hizo zingepita tayari yamejengwa majengo makubwa, tatizo la foleni Dar litaendelea kuwepo milele. Acheni kudanganywa na kuchekelea kama mazuzu.
 
anatia huruma hana mvuto kabisa
Mwambie baba yako akagombee ana mvuto labda ,Magu kidume haitaji mvuto kuingia Ikulu 28Oct ndio utajua kijani kina nguvu kuliko vyama vyovyote.
Hivi kwa akili yako kabisa unadhani kijani hakitoboi 🤣🤣🤣 karagabao utaona sasa hao wapiga kelele watatuma salamu za ushindi wenyewe tena ndo watakuwa mstar wa kwanza.Shida wengi wenu mmeshuhudia chaguzi hizi karibuni hamjazishudia zile zingine sasa hivi hakuna washindani kuna wapinzani wa maendeleo bado siku sio nyingi utablo..mapigo.
 
Mwambie baba yako akagombee ana mvuto labda ,Magu kidume haitaji mvuto kuingia Ikulu 28Oct ndio utajua kijani kina nguvu kuliko vyama vyovyote.
Hivi kwa akili yako kabisa unadhani kijani hakitoboi 🤣🤣🤣 karagabao utaona sasa hao wapiga kelele watatuma salamu za ushindi wenyewe tena ndo watakuwa mstar wa kwanza.Shida wengi wenu mmeshuhudia chaguzi hizi karibuni hamjazishudia zile zingine sasa hivi hakuna washindani kuna wapinzani wa maendeleo bado siku sio nyingi utablo..mapigo.
magu hana mvuto ,mama yako mi ndo namtaka ana mvuto
 
Back
Top Bottom