Uchaguzi 2020 Kinyerezi, Segerea: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. Magufuli

Amelibagua Jimbo lake sehemu zenye madiwani wapinzani amewanyima maendeleo,hizi Jamii zinazotoka nchi jirani ni wabaguzi Sana na wakabila kiasili
Umesema kweli mkuu kimanga na kinyerezi wamepitia kipindi kigumu ila naye safari hii ana hali ngumu sidhani kama atatoboa maana hata kuupata ubunge ilikuwa bahati baada ya majina ya wabunge wote wa ukawa kuwepo kwenye ballot paper licha ya kutangazwa mtatiro kuwa ndiye mpeperusha bendera ya ukawa
 
Naona Kumbilamoto kaamua kuchomoa betri walichokuwa wanafanya upinzani
Kumbilamoto naye tunayajua mambo yake hapo Vingunguti na wafanyabiashara ya mbuzi. Unamuangalia unaona tu jinsi alivyo falafala unamtunzia heshima tu.
 
Naona Kumbilamoto kaamua kuchomoa betri walichokuwa wanafanya upinzani
mkuu kumbe sisi Kawe tunakosa ma lami kama kule anapokaa shilole Majohe kwa upuuzi huu wa jamaa pinga pinga f.c
 
Ali Alidanganywa na jiwe eti usipeleke maendeleo mitaa ya wapinzani Hali wote ni watu wake,kakumbuka shuka anajifanya ana kwangua barabara Hadi mitaani.Ajiandae kuisoma namba, atapigiwa kura na mitaa aliyoipendelea,mitaa aliyoisomesha namba asitegemee kupata kura
 
Ilani ipenyi akilini bila uongo mwingiii,Uchonganishi,ubaguzi,kufokea,na mademu .hii nini hiii
 
Ni vizuri kama anatambua hili.
 
Rais hayupo consistency anapoelezea suala la kutatua changamoto za ajira....leo nimemsikiliza akisema kwamba endapo atachaguliwa tena basi tatizo la ajira litakuwa historia ......

Wakati sasa tunatega sikio atatatuaje ilihali yeye ndiye aliyefukuza kazi watu hovyo na kuuwa sekta binafsi ......

Ghafla akahama Mara oooh tuna gesi, tuna madini, tuna ndege tuna wanawake wazuri na wanaume wazuri..... Dah, nilichoka

Kitengo cha madaktari waliopo kwenye msafara wa rais itoshe kusema kwamba kuna tatizo kwa mgombea na kuna jambo halipo sawa .

Aidha wanaogopa kumwambia ukweli au mgombea hautaki ukweli huo,

28/10 watz wana jambo la kufanya.
 
Huyu Magu yeye kazi yake kujenga tu madaraja reli na miundombinu mingine Tundu Lissu ukiwa Rais mteue awe waziri Wa ujenzi
Hata kuwa Waziri wa Ujenzi hafai kabisa maana alipokuwa Waziri wa Wizara hiyo ndo alikatisha kandarasi 3000 za ujenzi wa barabara na kuitia Serikali hasara kubwa bila kuwajibishwa. Haijulikani katika maisha yake amefanikiwa kwa lipi maana licha ya maneno mengi, sifa na ngonjera nyingi amepwaya kabisa kwenye nafasi ya Urais na itakuwa kilio na kusaga meno akipewa miaka mingine 5. Amekuwa mtu wa kubebwa tu kutoka nafasi moja hadi nyingine bila kuacha legacy ndo maana hata mafanikio yake kama mwalimu pia hayajulikani wala akiwa Mbunge labda anajulijana huko kwao tu.
 
Kiukweli Leo baba kajichanganya tunajua mazuri aliyofanya ni mengi lakini anatoa hotuba kama vile anamlaumu aliyekuwa madarakani kwa awamu inayoisha wakati ni yeye mwenyewe!!, Mara vitambulisho vitasaidia wajasiriamali wadogo kupata mikopo bila riba, how comes!! Vitambulisho havina ata majina wala picture ya MTU,
Na Yale maneno aliyoyasema kuhusu mgombea wa upinzani mhhh ingekuwa ni mpinzani ndo kayasema kuhusu mgombea wa ccm nahisi angeitwa kwenye kamati ya maadili,
 
Anachekesha kweli!!! Je, wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi kwanini hakukamilisha ujenzi wa barabara badala yake anang'ang'ania flyovers. Kitakachoweza kuondoa foleni ni kujenga barabara za pembezoni (feeder roads) sio flyovers. Hili ndilo litakuwa suluhisho sahihi kabisa kwa tatizo la foleni Dar es Salaam. Nyote ni mashahidi kwamba, pamoja na kujenga flyovers, bado tatizo la foleni ni kubwa sana. Na kwa kuwa hakuna namna ya kuweza kujenga feeder roads kutokana na ukweli kuwa maeneo mengi ambako barabara hizo zingepita tayari yamejengwa majengo makubwa, tatizo la foleni Dar litaendelea kuwepo milele. Acheni kudanganywa na kuchekelea kama mazuzu.
 
anatia huruma hana mvuto kabisa
Mwambie baba yako akagombee ana mvuto labda ,Magu kidume haitaji mvuto kuingia Ikulu 28Oct ndio utajua kijani kina nguvu kuliko vyama vyovyote.
Hivi kwa akili yako kabisa unadhani kijani hakitoboi 🤣🤣🤣 karagabao utaona sasa hao wapiga kelele watatuma salamu za ushindi wenyewe tena ndo watakuwa mstar wa kwanza.Shida wengi wenu mmeshuhudia chaguzi hizi karibuni hamjazishudia zile zingine sasa hivi hakuna washindani kuna wapinzani wa maendeleo bado siku sio nyingi utablo..mapigo.
 
magu hana mvuto ,mama yako mi ndo namtaka ana mvuto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…