Kinyozi, mchomeleaji, bodaboda, mama ntilie,n.k. hulaza wastan elfu 10 kwa siku, mhitimu unaeogopa kuchekwa endelea kukaa nyumbani

Kinyozi, mchomeleaji, bodaboda, mama ntilie,n.k. hulaza wastan elfu 10 kwa siku, mhitimu unaeogopa kuchekwa endelea kukaa nyumbani

Shida sio kufanya hizo kazi ila shida ni kwamba wengi wanaofanya hivyo ulivyovitaja ni wale ambao walituacha shule na usikute tuliwabeza iwe moja kwa moja au sio moja kwa moja pia jamii ilitupatia ufalme na kutuona sisi ndio wamaana na tulio na akilli ila hao wengine walishaonekana malooser tayari.

Sasa jaribu kuvaa viatu vya kijana wa namna hiyo ambae mtaa ulimpa ufalme na akaonekana yeye ni mwenye akili na kuonesha ikiwa na matarajio makubwa sana Kwake then arudi na degree yake akaanze kushinda salon moja na kijana ambae alionekana looser baada ya kufeli.

Tafakari hapo kwa uzuri sana then nadhani utapata picha kwamba hawa vijana sio kwamba hawatamani kufanya kazi za namna hiyo ila shida ni kwamba wanahofia jamii ambayo iliwaamini na kuwa na matarajio makubwa juu yao then Kesho iwakute kwenye kazi zile zile ambazo zinafanywa na wale ambao walionekana hawana akili.

Hiki kitu kinawaumiza sana vijana kwenye akili hadi moyo ila wanakua hawana jinsi.

But ili kuwasaidia hawa vijana ni kuwashauri tu kwamba wakishamaliza vyuo wasirudi kwenye maeneo ambayo wamekulia bali watoke na waende wakatafute maisha kwenye mikoa mingine huko hakuna anaewajua kwahiyo watakua na uwezo wakujichanganya na kufanya kazi za aina yoyote ili watafute mitaji ya kuanzisha vya kwao.

Na hii inaonekana kwenye baadhi ya mikoa ambayo nimepata kukaa kwa mfano...

Ukienda Dodoma utakutana na vijana wengi wa bodaboda ni degree holders wale wengi kiasili sio wa mkoa ule ila wameamua kubakia pale waendeleze gurudumu la maisha pia nimeona hata Iringa maeneo ya mkwawa pale bodaboda wengi ni degree holders so wapo ambao wanatoka kwenye comfort zone zao na kujitafutia kilocal katika maeneo ambayo hawajulikani sana ingawa hata maeneo hayo pia wakishajulikana kwamba wako na degree halafu wanafanya hivyo bado wanawashangaa na kuwafanya vijana hawa wakose kujiamini.

Daslam ndio utakuta vijana wengi wanatoka mikoani kuja kusoma na wakimaliza chuo wanaongoza kujitafuta kilocal na wanaongoza kufanya vizuri na wengi wananyanyuka kiuchumi ila hawa ambao ni wazawa wa Dar huwakuti kwenye hizo shughuli kwa maana bado mentality yao iko kwenye watanionaje washkaji niliomaliza nao na kadhalika.
well noted, nimeongezea hii
 
The issue is not all about making money

Wewe unawaza tu Ila hauangalii mbele zaidi

Kuna degree holder wengi wamekufa kwa ajali za bodaboda

So think twice

Kama shida ni hela watu wasingesoma kabisa
You can't win the game if you're too afraid to play,

Huna kazi na upo broke, You need to work your way up or stay stuck waiting huku umri unaenda.

Risk ya kupata ajali kwenye vyombo vya moto sio kwa boda boda tu, watu wengi wa aina tofauti hupata ajali kila siku, wengi zaidi kuzidi boda boda, hao boda boda wanaopata ajali kwa kiasi kikubwa huwa ni speed kali na vilevi kama ilivyo kwa watu wengine wanaopata ajali na ni vitu unavyoweza kujitahidi kucontroll, na bado asilimia ya bodaboda wanaopata ajali ni ndogo ukiwaweka kwenye kundi la bodaboda wote.

Jaribu kuangalia positive side zaidi, bodaboda anaweza kupewa mkataba wa mwaka na nusu kila siku anaingiza elf 10 na akimaliza mkataba anapewa chombo kipato kinaongezeka anajichanga anaongeza chombo kingine, hii ni biashara tayari na fursa kwa watu wengine wakiwemo wahitimu kupata ajira.
 
Kama mtu atataka afanye biashara kisa amekosa kazi namhurumia sana... fanya biashara kwa moyo wako sio kwasababu umekwama kwingine. Biashara sio ya kila mtu. Kuwalazimisha vijana wote kuuza vitumbua na kuendesha bodaboda ni kufeli kama taifa. Serikali iweke sheria na sera nzuri ili wafanyabiashara wawe na mazingira mazuri kuweza kubuni miradi itakayotoa ajira kwa vijana. Yale mabilioni yanayotumika kwenye mradi wa BBT yangeelekezwa kukuza mitaji ya wakulima vijana ingeweza kusaidia kuajiri wenzao wengi
 
Kwa msomi mwenye busara uliye mtaani, ni wakati wa kujichanganya, usiangalie makunyanzi. Kuna dada aliyemaliza chuo, aliuza uji kwenye chupa na sasa ametulia ,biashara yake iko poa.
 
You need to tell degree holder /graduates to be job oriented and not money oriented.

Unapozungumzia 10k kwa siku

Nikwambie kuna watu wanalaza zaidi ya 10k uliyoandika hapo juu kupitia boda boda.

Watu sio kwamba wanadharau kuendesha boda au kuwa mama ntilie

Itapendeza ikiwa kila MTU atafanya kitu anachopenda na anachokimudu vzr.

Don't be fooled with politics being a bodaboda rider is not a job
Kama wewe ni msomi basi hio degree, masters, n.k ni ya karatasi tu, it’s too bad it didn’t come with real-world insight. You can easily solve 100 - 5 = 95 but you cant understand that 95 applicants will be left without a job when there are only 5 available, hao 95 wanaotoswa ni bora warudi kwenye mishe zao huku wanaendelea kuapply ajira au warudi nyumbani wanashinda kuapply ajira ambazo hazina guarantee ?
 
Mbele na nyuma hakuna kitu Ila kuna wewe.
 
Wewe umesoma lakini hujaelimika, unaweza kujibu 100 -5 = 95 lakini huwezi kufikiria wahitimu 100 waliosomea udaktari wakiitwa kujaza nafasi 5, ni 95 watakosa
Hata wakati wanasoma walilifahamu hilo, hivyo watavuta subira.
Hawawezi kutelekeza ndoto zao ili wakachomelee vyuma.
Wangetaka hayo wangeenda VETA kama wewe ulivyofanya baada ya kufeli kidato cha nne!
 
kuna mama ntilie wanafanya mauzo ya milioni 3 kila siku.

ukitoa jumapili ambapo wanapumzika, kwa mwezi wanafanya mauzo ya zaidi ya milioni 60.

tembelea kariakoo utazame tu mauzo ya mama ntilie mtaa wa manyema na mitaa mingineyo

mama ntilie wanakuja kazini na gari kabisa.
Huyo si mama ntilie tena
 
Shida wasomi wa bongo ni wakufaulu mitihani tu Hawana maajabu Kama kweli mtu umeelimika si lazima afanye hizo kazi sijui bodaboda
 
kuna mama ntilie wanafanya mauzo ya milioni 3 kila siku.

ukitoa jumapili ambapo wanapumzika, kwa mwezi wanafanya mauzo ya zaidi ya milioni 60.

tembelea kariakoo utazame tu mauzo ya mama ntilie mtaa wa manyema na mitaa mingineyo

mama ntilie wanakuja kazini na gari kabisa.

Acheni kumdanganya watu.
 
Kama wewe ni msomi basi hio degree, masters, n.k ni ya karatasi tu, it’s too bad it didn’t come with real-world insight. You can easily solve 100 - 5 = 95 but you cant understand that 95 applicants will be left without a job when there are only 5 available, hao 95 wanaotoswa ni bora warudi kwenye mishe zao huku wanaendelea kuapply ajira au warudi nyumbani wanashinda kuapply ajira ambazo hazina guarantee ?

Acha kulazimisha watu waishi maisha yako. Kukosa kazi isipelekee kukata tamaa na kufanya kazi ambazo hujasomea.
 
Hizo ni zile biashara zinazotegemea location.

Kinyozi wa Sinza, wa Dongobesh na wa Mwananyamala Kisiwani hawa ni vinyozi watatu tofauti.

Sawasawa na hizo kazi nyingine ulizosema.

In fact anayejiuza Sinza, atawacheka wenzake kwanini hawajiuzi kwakua ana constant market. Wakati anayejiuza Dongobesh atakua anajuta, na mnunuzi atakua na amani kununua Sinza kuliko Dongobesh au Mwananyamala Kisiwani.

You have to understand
 
Back
Top Bottom