Kiongozi anaposema ‘Watu hawali Katiba’, anapotosha kwa faida ya nani

Kiongozi anaposema ‘Watu hawali Katiba’, anapotosha kwa faida ya nani

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kuna viongozi wakiwepo wasomi wengine na PhD zao wanasema wananchi wanataka chakula wanataka maji hawataki Katiba kwa sababu hawatakula katiba. Huu ni upotishaji wa kiwango cha hali ya juu.

Katiba ni mkataba kati ya mtawala na mtawaliwa, ni jumla ya kanuni za msingi zilizoanzishwa na wananchi wenyewe ambazo zinaunda msingi wa kisheria wa sera, shirika au aina nyingine ya chombo cha dola na kwa kawaida huamua jinsi vyombo hivyo vinapaswa kuongozwa.

Sekita ya Elimu kwa mfano, inaendeshwa kwa sera na miongozo ambayo imetungiwa sheria kutokana na katiba, vile vile huwezi kujenga vituo vya Afya bila kuwa na sera bora za Afya ambazo zinatokana na katiba bora, sasa utaitenga vipi Katiba na Elimu, Afya, au Maji.

Najua wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi kulinda vyeo nk, lkn kwa kufanya hivyo hawaitendei haki jamii isiyo na uelewa mpana wa katiba ila laana haitawaacha wote wanaopotosha.
 
Kuna viongozi wakiwepo wasomi wengine na PhD zao wanasema wananchi wanataka chakula wanataka maji hawataki Katiba kwa sababu hawatakula katiba. Huu ni upotishaji wa kiwango cha hali y
Ukiona kiongozi anaetoa lugha kama hii basi tambueni huyu ni mufilisi na asie na faida tena ktk hata ngazi ya kijiji!
Kwa ufupi amefikia ukomo wa kuishi
 
Wote wanaosema hivyo ni walinda vyeo hawana lolote na wanafanya hivyo makusudi ili kupotosha,huwezi kusikia hio kauli kutoka kwa mwanachi wa kawaida.

Tuchukulie mfano katiba ikasema wazee wote kuanzia miaka 60 na kuendelea pamoja na vijana wasio na kipato wanapaswa kulipwa fedha za kujikimu kila mwisho wa mwezi,Je sio chakula hicho?
 
Back
Top Bottom