Charamba
Member
- Aug 12, 2022
- 7
- 12
1.0 UTANGULIZI
KIONGOZI Ni mtu mwenye dhamana ya kusimamia kundi fulani la watu yeye akiwa mstari wa mbele kama muwakilishi wa kundi hilo katika jambo fulani. Kiongozi hupatikana kwa namna mbalimbali kama vile kuchaguliwa, kuteuliwa au kurithi. Kuna aina kuu mbili za viongozi ambazo ni kwanza Kiongozi Bora na pili ni Kiongozi ni yule Kiongozi asiye Bora. Kwa nchini Tanzania kuna aina zote hizi mbili za Viongozi yaani kuna Viongozi waliobora na pia kuna wale Viongozi wasio bora.
1.1 KIONGOZI BORA NA SIFA ZAKE
Siyo kila kiongozi anaweza kuitwa kiongozi bora bali kunazo sifa zinazoweza kumfanya kiongozi kuwa kiongozi bora miongoni mwa sifa za kiongozi bora japo kwa uchache ni kama zifuatazo;
(i) kiongozi bora ni yule anayepatikana kutokana na ridhaa ya anowaongoza. Hapa ni juu ya utaratibu na mchakato mzima ambavyo kiongozi hupatikana mpaka kushika nafasi hiyo ya uongozi. Kwa maana hiyo kiongozi bora anapaswa awe yule anaeshika nafasi hiyo ya uongozi kwa ridhaa ya anaowaongoza, hakuna namna kiongozi anaweza kuwa bora kama anaowaongoza hawajalidhia kiongozi huyo kuwaongoza.
(ii) Kiongozi bora ni yule mwenyedira ya maendeleo kwa muda ambao atakuwa Kiongozi. Bila shaka ni ukweli uliowazi kwamba hakuna Nyumba inaweza kujengwa bila ya kuwepo kwa ramani ya Nyumba hiyo basi ukweli huo pia unatumik katika masuala ya uongozi kwani ili Kiongozi kuongozakwa mafanikio anapaswa kuwa na dira na maono juu ya kile anachokiongoza.
(iii) kiongozi bora ni yule anayeoongoza kwa kuzingatia sheria na misingi ya haki na usawa. Ukweli ni kwamba hakuna sharia dunianiinaruhusu vitendo vilivyo kinyume na haki. Kwa mfano kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,
Ibara ya 13(1) “Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria”
kwa maana hiyo kiongozi anapaswa kuwaongoza watu kwa kufuata sheria na misingi ya haki na usawa na hapo ndipo kiongozi huyo ataitw kiongozi bora.
(iv) Kiongozi bora ni yule anayetanguliza masilahi ya anaowaongoza na umma kwa ujumla na siyo masilahi yake binafsi. Kwa kuzingatia hili kiongozi hapaswi kujihusisha na vitendo vya wizi, rushwa, ufisadi au kujilimbikizia mali za Umma. Kwa kufanya hivyo kiongozi huyo ataitwa kiongozi bora.
2.0 AINA YA VIONGOZI WA TANZANIA KWA SASA
Ukweli ni kwamba Tanzania kwa sasa ina viongozi bora kwa kiasi chake lakin kwa sehemu kubwa viongozi wengi wa Tanzania siyo viongozi bora kwa sababu ya wanayoyafanya wengi wao hayaaksi Uongozi bora. Mfano wa mambo yanayofanywa na viongozi wa Tanzania ambayo yanawakosesha kuwa Viongozi bora ni kama vile Wizi, kujihusisha na vitendo vya rushwa, kutowajibika, kutokubali kukosolewa, matumizi mabaya ya mali za umma na mengine mengi kama hayo. Mambo hayo yote mengi hufanywa na viongozi wengi wa Tanzania kitu ambacho kinatoa sababu ya kusema Tanzania haina Viongozi bora wengi.
2.1 NINI SABABU YA KUWEPO KWA VIONGOZI WENGI WASIO BORA TANZANIA KWA SASA
Kunazo sababu mbalimbali ambazo zimepelekea kuwepo kwa viongozi wengi wasio bora na miongoni mwa sababu hizo japo kwa uchache ni kama zifuatazo;
(i) Kutokuwepo kwa namna bora ya kuwaandaa viongozi bora mapema tangu wakiwa na umri mdogo na badala yake kutarajia kupata viongozi bora wakati wameshakuwa watu wazima tayari.
(ii) Kutokuwepo kwa Sera Endelevu za maendeleo kwa Viongozi wan chi na badala yake kila Kiongozi huja na sera zake.
(iii) Ufinyu wa nafasi ya wanaoongozwa kuwakosoa Viongozi wao kutokan na yale wanayoyafanya katika uongozaji wao.
(iv) Kuwepo kwa mtazamo hasi kwa wanaoongozwa kuwaona Viongozi wao kama watu wakutisha na wa kuogopwa.
3.0 NINI KIFANYIKE KAMA MCHAKATO WA KUWAPATA VIONGOZI BORA TANZANIA KWA MIAKA 25 IJAYO
Kama tulivyokwishaona hapo awali kwamba ni rahisi kupata kiongozi lakini kumpata Kiongozi bora ni mchakato wa muda mrefu hivyo kwa Tanzania kuwapata viongozi bora kwa miaka 25 ijayo inapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kufanikisha jambo hilo. Na miongoni yanayopaswa kufanywa ni kama yafuatayo japo ni kwa uchache;
(i) Kuanza na kizazi kichanga cha sasa kwa kuwafundisha kuhusu misingi ya Uongozi bora, hapa tunaweza kulejelea maneno ya biblia “mlee mtoto katika mjia impasayo naye hatoiacha hata atakapokuwa mkubwa” maandiko haya yanatufundisha kuwa mtotoanapaswa kulelewa katika njia iliyo sahihi ilia je kuwa mtu mzima mwema. Ndivyo hivyo pia Tanzania inapaswa sasa kuanza kuwalea watoto wa Kitanzania katika misingi ya Uongozi bora kwa sababu watoto wa leo ndio viongozi wa kesho hivyo tutakuwa na viongozi bora kesho. Na hili linaweza kufanyika kwa kuwekwa katika mitaala ya elimu kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu.
(ii) Serikali ianze utaratibu wa kuwepo kwa sera endelevu za maendeleo ambazo viongozi watapaswa kuzitimiza. Tanzania tuitakayo yenye viongozi bora itafikiwa kama Serikali itakuja na utaratibu wa kuunda sera ambazo zitakuwa endelevu ambazo kila kiongozi atakayekuwa anashika madaraka ya uongozi anakabidhiwa ili azitimizekwa kipindi atakachokuwa kiongozi, hii itasidia kuwa na maendeleo endelevu ya nchi na pia itarahisisha kuwatathimini Viongozi utendakazi wao
(iii) Kusiwepo na utenguzi wa kihorera wa Viongozi hususani Viongozi wanaoteuliwa. Hapa ni kwamba kwa wale Viongozi wanaoteuliwa kama vile Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wengineo wasiwe wanatenguliwa hovyo kwani utenguzi wa kihorera unapeleke Viongozi kuwa wezi na kujilimbikizia mali za umma kwani wanakaa muda wote wanajua muda wowote naweza kutenguliwa hivyo anaamua kuvuna haraka ili akitenguliwa asione hasara. Kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza uaminifu wa Viongozi na itasaidia kuwa na Viongozi bora kwa kesho.
(iv) Kuundwe vyombo maalumu vilivyo huru vitakavyokuwa na jukumu la kufatilia, kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi mbalimbali nchini, Hii itasaidia kuongeza uadilifu wa Viongozi, hivyo kuwa na Viongozi bora kwa kesho.
(v) Mfumo na mchakato wa kuwapata viongozi unapaswa kuwa huru na wa haki, Hapa ni juu ya maswala ya uchaguzi kwa mfano Tume Ya Uchaguzi inapaswa iwe huru isiingiliwe kwa namna yoyote kwa kufanya hivyo kutasaidiakupunguza na kuondoa kabisa vitendo vya udanganyifu katika chaguzi, hivyo kupata Viongozi bora kwa kesho.
4.0 HITIMISHO
Kwa kuhitimisha ni kwamba ili Tanzania kuyafikia maendeleo ya kweli katika Nyanja mbalimbali kuna haja ya Serikali kuchukua hatua za makusudi juu ya kutekeleza haya ambayo yameelezwa katika andiko hili kwa upeo na maono yangu ili kufanikisha kuifikia Tanzania Tuitakayo.
Nawasilisha kwa unyenyekevu,
Mimi, Boniphace Julius Charamba.
12/06/2024.

Upvote
123