SI KWELI Kiongozi mkuu mpya Alireza Arafi wa Iran ameuawa

SI KWELI Kiongozi mkuu mpya Alireza Arafi wa Iran ameuawa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa zinazosema kiongozi mkuu mpya wa Iran Bwana Alireza Arafi ameuwawa.

Ngoja tusubiri tuone kama itakuwa ni kweli.
1772701718723.png
 
Tunachokijua
Jeshi la Israel (IDF) lilithibitisha kumuua Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran, katika shambulio kubwa la anga lililofanywa mjini Tehran, na hivyo kumaliza utawala wake uliodumu kwa miongo kadhaa. Iran pia ilikiri kifo chake na kutangaza mipango ya uongozi wa muda.

Kufuatia kifo cha Ali Khamenei kilichodaiwa kusababishwa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel, Iran ilimtaja Alireza Arafi kuwa Kiongozi Mkuu wa muda. Arafi ni mwanazuoni wa juu wa kidini mwenye uhusiano mkubwa na taasisi za kidini na kisiasa za Iran, na aliwahi kushika nyadhifa muhimu ikiwemo katika Baraza la Guardian Council.

Madai

Kumekuwapo na taarifa inayosmbazwa mtandaoni kuwa kiongozi mpya wa Iran Alireza Arafi ameuawa.

Je, ni upi uhalisia wa Taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli, kwani hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichothibitisha au kutoa taarifa hiyo. Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa madai hayo yanatokana zaidi na uvumi wa mitandaoni kuliko taarifa za mamlaka au vyombo vya habari vinavyoaminika.

Hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran, serikali za kigeni, au mashirika makubwa ya habari ya kimataifa kuhusu madai ya kifo hicho.

Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa Arafi aliteuliwa kuongoza baraza la uongozi wa muda wa Iran kufuatia kifo cha kiongozi mkuu wa muda mrefu, Ayatollah Ali Khamenei.​
Si ulisema ameuwawa na ukashangilia hapa kuwa Rais Pezeshkian kawahishwa ahera. Hahahah mpaka unatia huruma, mpotoshaji mkuu JF.
Hakuna Aliyesema hayo wewe endelea tu kujifariji Maana Magaidi huko Iran wanauliwa sana akiwemo Gaidi Ayatollah Ali Khamenei
 
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na Mojtaba Khamenei aliyechukua mikoba ya Ayatollah Ali Khamenei inasemekana wamefyekelewa mbali na kuangamizwa na majeshi hodari ya Israel.
Si wewe ndio ulipost huu ujinga sasa unakana nini hapa?
Hakuna Aliyesema hayo wewe endelea tu kujifariji Maana Magaidi huko Iran wanauliwa sana akiwemo Gaidi Ayatollah Ali Khamenei
 
Si wewe ndio ulipost huu ujinga sasa unakana nini hapa?
Ulivyo mjinga hata hujui maana ya Neno Inasemekana mikubwa Gaidi Ayatollah Ali Khamenei aliangamizwa bila huruma na Majeshi hodari ya Israel!!
 
Back
Top Bottom