Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei atiliashaka mazungumzo ya nyuklia ya Marekani

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametiliashaka kwamba mazungumzo ya nyuklia ya Marekani yataleta mwafaka, akisema kuwa taifa hilo limetoa masharti mengi na ya kukerankuhusu kurutubisha urani.

Hatujui iwapo yatasababisha mafanikio yoyote. Hatujui kitakachotokea, Ayatollah Ali Khamenei alisema.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema wiki iliyopita kwamba Iran walikuwa na“aina ya” ya makubaliano kufuatia duru nne za mazungumzo yaliyopatanishwa na Oman tangu tarehe 12 Aprili.

Lakini kabla ya kufanyika kwa duru nyengine ya mazungumzo yanayotarawa wikendi hii, , Mpatanishi Mkuu wa Iran amekataa madai ya mwenzake wa Marekani kwamba italazimika kujitolea kuacha kuzalisha urani iliyorutubishwa, ambayo inaweza kutumika kutengeneza mafuta ya kinu cha kuzalisha umeme lakini pia silaha za nyuklia.

Trump, ambaye aliiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani katika muhula wake wa kwanza madarakani, ameionya Iran kuwa inaweza kukabiliwa na mashambulizi ya kijeshi kutoka Israel na Marekani iwapo mazungumzo hayo hayatafanikiwa.

Iran inasisitiza kuwa shughuli zake za nyuklia ni za amani kabisa na kamwe haitatafuta kutengeneza au kupata silaha za nyuklia.

Hata hivyo, imekiuka vikwazo vilivyowekwa na mkataba uliopo wa nyuklia ili kulemaza vikwazo vya Marekani vilivyorejeshwa miaka saba iliyopita, na imekusanya madini ya urani yenye thamani kubwa kutengeneza mabomu kadhaa
 
Hapa Trump akij8changanya atapigika kama ngoma kashindwa na kikundi cha wa houthi aje kumuweza iran 🇮🇷
 
Muda ukifika utajionea wenzako wanavyopanua midomo kwa juhudi na kupayuka .."free Iranians"...!
Kama walishindwa kuanzia 1980-1988 kipindi Iran Ina jeshi dhaifu la mapinduzi wataweza sasa hivi Iran ikiwa na jeshi imara!?
Acha vichekesho wewe.
 
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametiliashaka kwamba mazungumzo ya nyuklia ya Marekani yataleta mwafaka, akisema kuwa taifa hilo limetoa masharti mengi na ya kukerankuhusu kurutubisha urani.

Hatujui iwapo yatasababisha mafanikio yoyote. Hatujui kitakachotokea, Ayatollah Ali Khamenei alisema.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema wiki iliyopita kwamba Iran walikuwa na“aina ya” ya makubaliano kufuatia duru nne za mazungumzo yaliyopatanishwa na Oman tangu tarehe 12 Aprili.

Lakini kabla ya kufanyika kwa duru nyengine ya mazungumzo yanayotarawa wikendi hii, , Mpatanishi Mkuu wa Iran amekataa madai ya mwenzake wa Marekani kwamba italazimika kujitolea kuacha kuzalisha urani iliyorutubishwa, ambayo inaweza kutumika kutengeneza mafuta ya kinu cha kuzalisha umeme lakini pia silaha za nyuklia.

Trump, ambaye aliiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani katika muhula wake wa kwanza madarakani, ameionya Iran kuwa inaweza kukabiliwa na mashambulizi ya kijeshi kutoka Israel na Marekani iwapo mazungumzo hayo hayatafanikiwa.

Iran inasisitiza kuwa shughuli zake za nyuklia ni za amani kabisa na kamwe haitatafuta kutengeneza au kupata silaha za nyuklia.

Hata hivyo, imekiuka vikwazo vilivyowekwa na mkataba uliopo wa nyuklia ili kulemaza vikwazo vya Marekani vilivyorejeshwa miaka saba iliyopita, na imekusanya madini ya urani yenye thamani kubwa kutengeneza mabomu kadhaa
Huyo Israel anapewa Hizbollah apapatuane nao.
Huyo Marekani kambi anazozitegemea middle east zitashughulikiwa na Houthi kabla hata Iran haijaanza retaliation.
Hakuna mwenye ubavu kwa Iran hapo.
 
Umenena mkuu
 
Umenena mkuu
Watu huongea kwa mitazamo mifupi sana.
Iran ukiitizama unaweza ukaiona nchi nyepesi ila Iran ni taifa lile tena gumu sana.
Nchi ina vikwazo vya kiuchumi miaka zaidi ya 40 ila imefanikiwa kuwa middle income country na ina maendeleo hadi ya teknolojia na viwanda.
Nchi imehimili vita ya miaka nane ikiwa na jeshi changa la mapinduzi.
Sio hivyo tu imeunda hadi vikundi vya kiasi na kuvifadhili kivita mathalan Hizbollah.
Hiyo nchi bado unaiona ni nyepesi!??
 
Back
Top Bottom