Kiongozi Mwandamizi wa CHADEMA akutana na Kikwete, Kinana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Kiongozi Mwandamizi wa CHADEMA akutana na Kikwete, Kinana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

DaveSave

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Posts
440
Reaction score
638
Jitihada za kumaliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, zinaendelea “nyuma ya pazia,” ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amekutana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani.

Haijaweza kufahamika kama jitihada hizo ni za Mnyika binafsi au zina baraka ya chama hicho, ambacho kwenye mitandao ya kijamii kimetanabaisha kuwa hakitaki suluhu yoyote kuhusiana na kesi hiyo.

Taarifa hizo zinaeleza kwamba kimsingi Mama Samia Suluhu aliridhia ombi la kuachiwa kwa Mheshimiwa Mbowe na ilitarajiwa aachiwe kwa “nolle prosequi” (tamko la nia ya kutoendelea na mashtaka) ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) lakini “yaliyojiri kabla, wakati na baada ya mkutano wa vyama vya siasa huko Dodoma” yalipelekea mpango huo kukwama.

Licha ya jitihada hizo za Mnyika, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman nae aliwasilisha maombi ya Chadema kwa Mama Samia, na akashauri Mheshimiwa Mbowe aachiwe bila masharti yoyote.

Uamuzi wa Chadema kususia mkutano huo wa vyama vya siasa huko Dodoma ambao ulifunguliwa na Mama Samia, inatajwa kuwa moja ya sababu zilizopelekea kukwama kwa mpango huo wa kumwachia Mheshimiwa Mbowe.

Taarifa hizi zinakinzana na kauli zinazoongewa na viongozi na wafuasi wa chama hicho kuwa “hawako tayari kuomba Mheshimiwa Mbowe aachiwe” kwa sababu wanaamini kuwa hana hatia na mashtaka dhidi yake ni ya kutungwa.

Yawezekana tofauti hizo kati ya “kinachoendelea faraghani” na “kinachoongelewa hadharani” zikawa ni mkakati wa Chadema hasa ikizingatiwa kuwa wafuasi wengi wa chama hicho hawaafiki kabisa wazo la kuomba Mheshimiwa Mbowe aachiwe. Moja ya sababu zinazochangia “msimamo huo mkali” ni shinikizo la “wanaharakati wa mtandaoni” ambao wanapinga vikali siasa za maridhiano kati ya chama tawala CCM na vyama vya upinzani.

Hata hivyo, suala hilo la kesi ya Mbowe “limevamiwa” pia na kundi moja ndani ya CCM linalompinga Mama Samia, na ambalo linaiona kesi hiyo dhidi ya Mheshimiwa Mbowe kuwa yenye manufaa kwa kundi hilo kwa sababu inatoa taswira mbaya kuhusu Mama Samia.

Nihitimishe kwa kutanabaisha kuwa haitokuwa jambo la kushangaza endapo Mheshimiwa Mnyika atakanusha taarifa hizi kwa sababu “zinaweza kumletea tabu” katika chama chake.

Jumanne njema
 
Jitihada za kumaliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, zinaendelea “nyuma ya pazia,” ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho...
Vipi ikiwa Samia akiwa ndiye kawatuma , Kikwete , Kinana na Mtunga uongo wa kesi hiyo aliyeshirikiana na Magufuli na baadaye Samia kumweka selo Mbowe anayeitwa Diwani Athumani ILI KUMUANGUKIA MNYIKA ASHAWISHI CHADEMA IKUBALI MBOWE AACHIWE ?

Na je ikiwa Mnyika akiwaeleza hao akina kikwete na kundi lake msimamo wa Chadema kwamba Serikali ndio imuombe radhi Mbowe kwa kesi ya uongo na ya kutunga kishamba kabla ya kumuachia utakuwa tayari kuripoti pia ?
 
Jitihada za kumaliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, zinaendelea “nyuma ya pazia,” ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho
CHADEMA wafunike kombe, mwanaharamu aendelee kupumzika.

Kesi hii iliasisiwa Awamu ya 5, na mama Samia alikiri hivyo.
 
Vipi ikiwa Samia akiwa ndiye kawatuma , Kikwete , Kinana na Mtunga uongo wa kesi hiyo aliyeshirikiana na Magufuli na baadaye Samia kumweka selo Mbowe anayeitwa Diwani Athumani ILI KUMUANGUKIA MNYIKA ASHAWISHI CHADEMA IKUBALI MBOWE AACHIWE ?

Na je ikiwa Mnyika akiwaeleza hao akina kikwete na kundi lake msimamo wa Chadema kwamba Serikali ndio imuombe radhi Mbowe kwa kesi ya uongo na ya kutunga kishamba kabla ya kumuachia utakuwa tayari kuripoti pia ?
Serikali HAIDEKEWI wala HAINUNIWI. Chagua kusuka au kunyoa
 
Jitihada za kumaliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, zinaendelea “nyuma ya pazia,” ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika...
Kwahiyo Mbowe hakuachiwa kwa sababu ni Gaidi au kwa sababuChadema hawakuhudhuria mkutano wa ccm?
 
Back
Top Bottom