Kiongozi ni yule ambaye mikono yake haina damu, anapoteuliwa watu hufurahia na kujihisi salama. Usirudie makosa!

Kiongozi ni yule ambaye mikono yake haina damu, anapoteuliwa watu hufurahia na kujihisi salama. Usirudie makosa!

Namwambia rafiki yangu mpita njia kwamba zama zimebadilika, malaika anaetawala sasa ni malaika wa kheri. Watu wanaenda wapendako na wanalala wanapotaka wao. Enzi za kumiliki vikosi na magenge ya wahuni zimepita, hazipo tena.

Nakwambia wewe rafiki yangu mpita njia kwamba, zama za kutishia watu bastola ama kumiminia watu risasi zimesahaulika, kwa sasa tunaendelea kuuguza na kuganga vidonda vya walioumizwa.

Nikupe taarifa tu kwamba, mpaka sasa bado kuna watu wanavilema vya maisha, na wengine hatujui waliko. Familia zao mpaka hazielewi kama waliuwawa au walifukiwa wakiwa hai, au ama walitupwa baharini.

Karibu sana mjini, mji unasisimka kwa hofu, sio furaha tena. Usione wanakenua meno ukajua wanafuraha, hapana, wana maumivu makali sana. Sijajua wale walioporwa ardhi na minyukano iliyokuwa inasimamiwa na kinjekitile ngwale enzi za mkwawa?

Tafadhali ukishika mic kwa mara ya kwanza omba msamaha, wala usione aibu. Uungwana ni vitendo, hata mbingu zitakuelewa sana! Rip all innocent.

Mkuu kama mhusika anasoma hapa umempa ushauri mzuri, Hii ni second chance ya kurekebisha mambo yote ya nyuma! Kazi ni kwake, yetu macho!
 
Lime korogeka chamani
Lime korogeka Tiss kwani huko ndipo alipo vuruga zaidi kwakupora protocol za utendaji wakati wanaelewana na dingi yake kabla dingi Jiwe hajamtema hivyo kisasi Bado kipo

Ukweli Kuna Mkorogo
Huku Gsm anatazama Kwa mbali
Duuh
 
20231026_063101.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda uta sema
Kigogo ataibika upya!!!
Kwanza ameshaanza mawasiliano na Mange iweje alicho sema kimekuwa kweli?!!!

Zakuambiwa changanya na za Mange[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
hivi mange yupo
 
Back
Top Bottom