Kiongozi wa Al Qaeda, Ayman al Zawahiri auawa kwa shambulio la drone lililofanywa na Marekani

Kiongozi wa Al Qaeda, Ayman al Zawahiri auawa kwa shambulio la drone lililofanywa na Marekani

Al qaeda hivi karibuni limepotrza umaarufu wake na sidhani kama ni threat sana kama tunavyo aminishwa?
Wameshalitumia lishamaliza Kazi yake wamelidump,wakaanzisha jingine la ISIS na ISIL nayo yanapotea, hii njia ya ugaidi naona awaitumii tena. Naona wanataka kumchapa Iran kupitia kundi la Taliban.
 
Operesheni ya kukabiliana na ugaidi nchini Afghanistan imemuua kiongozi wa kundi la al- Qaeda, Ayman al-Zawahiri, Rais Joe Biden amethibitisha.

Vinasema kwamba aliuawa katika shambulio la ndege isiyo kuwa na rubani lililotekelezwa na CIA katika mji mkuu wa Kabul siku ya Jumapili.

Bw Biden alisema Zawahiri "amechonga mkondo wa mauaji na ghasia dhidi ya raia wa Marekani".

"Sasa haki imepatikana na kiongozi huyu wa kigaidi hayupo tena," aliongeza.

Maafisa walisema Zawahiri alikuwa kwenye balkoni ya nyumba wakati ndege isiyo na rubani ilipomrushia makombora mawili.

Wanafamilia wengine walikuwepo, lakini hawakujeruhiwa na ni Zawahiri pekee aliyeuawa, waliongeza.

Bw Biden alisema ametoa kibali cha mwisho cha "mashambulizi ya usahihi" dhidi ya kiongozi huyo wa al-Qaeda mwenye umri wa miaka 71 baada ya miezi kadhaa ya kupanga.

Kuuawa kwake kutaleta kufungwa kwa familia za wahasiriwa wa mashambulio ya 2001, Bw Biden alisema.

"Haijalishi itachukua muda gani, haijalishi utajificha wapi, ikiwa wewe ni tishio kwa watu wetu, Marekani itakupata na kukuondoa," alisema Bw Biden na kuongeza kuwa "hatutawahi kusita kutetea taifa letu na watu wake".

Bw Biden alisema Zawahiri pia alipanga vitendo vingine vya vurugu, ikiwa ni pamoja na shambulio la kujitoa mhanga kwa meli ya kivita ya USS Cole huko Aden mnamo Oktoba 2000 ambayo iliua mabaharia 17 wa Marekani.

Chombo cha habari cha CBC News kimesema kwamba vyanzo vitatu vimethibitisha mauaji hayo ya kiongozi huyo wa al-Qaeda. Chombho cha Habari cha New York Times, Washington Post na CNN vimenukuu vyanzo visivyojulikana vikimtambua muathiriwa.

Afisa mmoja mkuu amezungumza kuhusu operesheni iliofanikiwa dhidi ya malengo muhimu nchini Afghanistan.

Operesheni hiyo ilifanyika wikendi iliopita na hakukuwa na raia waliojeruhiwa, maafisa hao walisema.

Wakati huohuo, msemaji wa Taliban aliripoti kwamba shambulizi la ndege ya marekani isio na rubani lilifanyika siku ya Jumapili katika eneo la makaazi ya watu mjini Kabul.

Alieleza kuwa ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kimataifa.

"Vitendo kama hivyo ni marudio ya uzoefu uliofeli wa miaka 20 iliyopita na ni kinyume na maslahi ya Marekani, Afghanistan na kanda," msemaji huyo aliongeza.

Hili limekuwa pigo kubwa sana kwa wavaa kobazi wakiongozwa na Bwana Utam na STRUGGLE MAN
 
Haijalishi itachukua muda gani, haijalishi utajificha wapi, ikiwa wewe ni tishio kwa watu wetu, Marekani itakupata na kukuondoa," alisema Bw Biden na kuongeza kuwa "hatutawahi kusita kutetea taifa letu na watu wake".
kauli ya kibabe sana hii
 
US Wakiamua Jambo Lao Hata Miaka 50, Mpaka Litimie Haijalishi Gharama
Amewindwa Mpaka Ameuwawa
... nimeshangaa sana! Tangu Osama auwawe 2011 hadi leo (11 years) wanaendelea kumsaka mrithi wake hawakati tamaa! Jamaa wakikuamulia lazima wakuue aisee; hata zipite tawala ngapi as long as uko kwenye list yao lazima maamuzi yatekelezwe no matter how long it will take! Dah!
 
Al-Zawahiri.JPG
Kiongozi wa Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri ameuawa na ndege ambayo haina rubani ‘drone’ mali ya CIA katika Mji wa Kabul Nchini Afghanistan.

Rais wa Marekani, Joe Biden amesema haki imetendeka na gaidi Al-Zawahiri ameuawa, akidai hilo ni pigo kubwa kwa kundi hilo kwa kuwa ndiye aliyekuwa akishikilia madaraka ya Osama bin Laden aliyeuawa 2011.

Biden amesema shambulizi hilo limemuua mtu mmoja tun a halikuwa na madhara kwa watu wengine

=========================

Al-Qaeda leader Ayman al-Zawahiri killed in US drone strike


US President Joe Biden says ‘justice has been delivered’ after al-Qaeda leader located and killed in Kabul, Afghanistan.

Al-Qaeda leader Ayman al-Zawahiri has been killed in a CIA drone strike in Afghanistan’s capital, Kabul, United States President Joe Biden has said.

Al-Zawahiri was killed on Sunday in the biggest blow to the group since its founder Osama bin Laden was killed in 2011.

“Justice has been delivered and this terrorist leader is no more,” Biden said in a special televised address from outside the White House.

Intelligence had located al-Zawahiri’s family in Kabul earlier this year, Biden said, adding that no members of the family or civilians had been killed in the attack.

An Egyptian surgeon with a $25m reward on his head, al-Zawahiri helped coordinate the September 11, 2001 attacks on the US that killed nearly 3,000 people.

Earlier, US officials speaking on the condition of anonymity told reporters earlier that the CIA carried out a drone attack in Kabul using two missiles.

Al-Zawahiri was on his balcony at the time, they said.

“It’s a significant blow,” Colin Clarke, research director at the Soufan Group, a global security firm, told Al Jazeera, adding that his presence in Kabul was also interesting in what it suggested about his relationship with the Taliban.

“It tells us he’s gotten far more comfortable over the past years since the Taliban took over,” Clarke said.

The Taliban confirmed the attack in Kabul, and condemned it as a “violation of international principles”.

In a statement, US Secretary of State Antony Blinken said al-Zawahiri’s presence in Kabul “grossly violated the Doha Agreement and repeated assurances to the world that they would not allow Afghan territory to be used by terrorists to threaten the security of other countries”.

Washington and the Taliban signed the deal in 2020 paving the way for the withdrawal of US-led foreign forces in return for a guarantee from the Taliban not to allow groups such as al-Qaeda and ISIL (ISIS) to operate on Afghan soil. The US forces withdrew just before an August 31 deadline in what turned out to be a chaotic exercise.

Blinken said that by allowing al Qaeda shelter in Afghanistan, the Taliban had also “betrayed” the Afghan people and “their own stated desire for recognition from and normalization with the international community”.

Source: Aljazeera
 
Magaidi hawako salama kila mahali, ukiona ligaidi ambalo halijauliwa si kwamba ni lijanja na lina uwezo wa kujificha ila jua Marekani hajaona ulazima wa kuliua kwa wakati huo. Muda ukifika ni shaba basi.

Tunasubiri watakayemchagua naye awekwe kwenye orodha ya watafutwaji
Alzawhri alishajisahau kabisa. Angebakia tu milimani huko kwenye triibral tarrain na makabila ya Pashto ambao ni Talenan. Sasa yeye kaenda kujichanganya mjini Kabul halafu alikuwa akipunga hewa kwenye Balcony mizinga miwili ya drones " ninja hell fire". Ila mmarekani noma. Wameleta hofu Sana kwa magaidi. Na siku hizi magaidi wakitembea macho Yao Kila mara yanaangalia juu utadhani kuku anayekunywa maji.
 
Back
Top Bottom