Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 7,748
- 10,288
Kwa nini wasimkamate mchana?👇
Katibu wa Kanda ya Victoria, ndugu Zacharia Thomas Obadi, amekamatwa na watu waliofika nyumbani kwake saa nane usiku na kuanza kugonga mlango.
Hata hivyo, mlango haukufunguliwa hadi ilipofika saa tisa usiku, ndipo walipokuja na Mwenyekiti wa mtaa na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Inadaiwa kuwa mmoja wa askari hao anafahamika katika mtaa wa Kahama.
Zacharia amechukuliwa kwa kutumia gari aina ya Land Cruiser, na watu hao wameondoka naye. Hadi sasa, tunahitaji kufahamu alipo na hali yake.
Soma Pia: Mwenyekiti wa Vijana kanda ya Victoria, Fred Masele anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za Uchochezi
Tumepokea Taarifa toka kwa wanafamilia, Tumuombee ndugu yetu Zacharia awe salama akiwa mikononi mwa polisi.