Kiongozi wa CHADEMA kanda ya Victoria, Zacharia Obadi akamatwa na polisi usiku wa manane

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
​

Kwa nini wasimkamate mchana?πŸ‘‡

Katibu wa Kanda ya Victoria, ndugu Zacharia Thomas Obadi, amekamatwa na watu waliofika nyumbani kwake saa nane usiku na kuanza kugonga mlango.

Hata hivyo, mlango haukufunguliwa hadi ilipofika saa tisa usiku, ndipo walipokuja na Mwenyekiti wa mtaa na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Inadaiwa kuwa mmoja wa askari hao anafahamika katika mtaa wa Kahama.

Zacharia amechukuliwa kwa kutumia gari aina ya Land Cruiser, na watu hao wameondoka naye. Hadi sasa, tunahitaji kufahamu alipo na hali yake.

Soma Pia: Mwenyekiti wa Vijana kanda ya Victoria, Fred Masele anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za Uchochezi

Tumepokea Taarifa toka kwa wanafamilia, Tumuombee ndugu yetu Zacharia awe salama akiwa mikononi mwa polisi.
 
Yes,
ikiwa anashukiwa kwa uhalifu au ukikuaji wa sheria za nchi ni muhimu akatiwa nguvuni.

Bilashaka yoyote,
muungwana ni miongoni mwa wale vijana mamluki waliokua wamehifadhiwa hoteli flani hivi pale Nairobi na kale kabibi kadrama, kwaajili ya kuzalisha uongo, porojo, na uzushi baada ya kushiriki ghasia, uharibifu na maafa ya Oct 2025.

Na wote waliokua wamehifadhiwa Nairobi,
wakikanyaga ardhi ya Tanzania tu lazima watiwe nguvuni kwasababu hawana adabu hao πŸ’
 
Na hapo watu wanaimba wimbo wa maridhiano, hiki ni kituko kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…