Nimeshangaa sana kusoma taarifa kuwa kiongozi huyo anatarajia kutoa hotuba leo Ijumaa wakati wa sala ya Ijumaa kwani anajiweka katika hatari ya kushambuliwa na majeshi ya Israel kama ilivyokuwa kwa viongozi wakuu wa Hesbolah na Hamasi(asijiamini sana kiulinzi, lolote laweza tokeo)
Bado inaweza isiwe leo, ila hapaswi kuendelea kufanya hivi kwa siku za usoni kwani wanaweza kumla kichwa( Netanyau ni mental case).
Nieleweki kabisa kuwa Siwapendi wa Israel kwasababu moja kubwa: kuwaonea wapalestina na kuwaua hovyo kama wanaua kuku au panya. Hawana ubinadamu kabisa na wanajiona wao ni binadamu wa daraja la juu kulinganisha na wapalestina wanaowaona kama sio binadamu.
Kwa msingi huo, nisingependa kuona Israel anafanikiwa katika vita yake na Iran na ndio maana namtahadharisha Ayatollah asijaribu kujianika maana Israel huwa hawajali nini kitatokea baadae(hawapimi maamuzi yao) la muhimu kwao ni kutaka kuonyesha dunia kuwa wao ni bora kivita katika hilo eneo lote la Mashariki ya Kati.
Kwahiyo, hawatasiita kumshambulia Ayatollah kwa kushitukiza sambamba na kushambuliwa vituo vya kijeshi na nuclear facilities za muajemi pamoja na kushambulia raia kwa kushambulua mfululizo kuhakikisha Iran hapati muda wa kujipanga.
Mpaka sasa Israel ameshaona uwezo wa Iran na hatari iliyopo kuingia nae vitani. Hivyo, njia pekee ya kupambana nae ni kuanzisha mashambulizi ya non stop (full blown war) jambo ambalo linaweza kuwafanga Iran watumie unconventional weapons kama vile sila za nyuklia na hii ndio hatari ambayo mmarekani ameshaiona.
Kwa kifupi, Israel alijaa sana kiburi hasa baada ya kuua viongozi wa Hamasi na Hesbolah huku Iran akiwa katulia, ila sasa kiburi hicho mbele ya Iran hakitavumiliwa na unaweza kuwa ni mwanzo wa janga la kibinadamu katika hilo eneo, na dunia ikizembea, tunaweza shuhudia vita ya tatu ya dunia kiutani utani tu.
Muda utaongea.
NB: Kuingia katika vita au kuendelea kupigana vita wakati kiongozi wa juu wa nchi ameuwawa au kujeruhiwa, ni disadvantage kubwa sana na ni advantage kubwa sana kwa adui na Israel huenda anapanga kufanya jambo kama hili akijua faida ya kufanya hivyo.
Mkuu, hisia zako zinaeleweka sana. Kwamba Wapalestina wanaonewa na kunyanyaswa sana inaeleweka. Na inafahamika vizuri kuwa Wapalestina wako Waislamu na Wakristo pia. Na kwamba Wapalestina wengi ni watu wa kawaida wenye malengo ya maendeleo katika mazingira ya kisasaninajulikana.
TATIZO KUBWA ni kuwa suala la kupigania uhuru na haki za Wapalestina LIMETEKWA na vikundi vya Waislamu wenye msimamo mkali wa Jihad (
Radical Islamists). Vikundi hivyo kama
HAMAS na
Hezbollah lengo lao kuu rasmi ni kuiangamiza Israel, Wayahudi wote na watu wote wasio wa imani ya kali Kiislamu. Kisha kuhakikisha Mashariki ya Kati inaongozwa na utawala wa Sharia pekee. Ndio maana IRAN inajihusisha sana na suala la Wapalestina.
Katika hali itakayokushangaza pia ni kuwa, Wayahudi wenye msimamo mkali kama Benjamin Netanyahu na serikali anayoiongoza, wanapenda sana tawala za hao Radical Islamists huko Palestine na Lebanon kwa sababu nao hawataki amani. Hawataki
a two state solution. Wanataka vita kwa sababu lengo lao ni kuwafurusha Wapalestina wawaachie ardhi yote ya Palestina, Israel ibakie kuwa taifa moja tu. Kisha waangamize utawala wa Ayatollah wa Iran na miundombinu yake ya Nuclear. Kisha wahakikishe hakuna jirani anayewaletea fyoko Israel. Yote hayo kwa msaada wa watu wa Marekani. Kuna wakati serikali ya Netanyahu iliunga mkono ushindi wa HAMAS dhidi ya PLO katika uchaguzi huko Gaza.
IRAN ina mkono katika harakati zote za kusimika na kuimarisha makundi ya kigaidi yenye ajenda ya Uislamu wa msimamo mkali (RADICAL ISLAM) duniani kote. Hawataki muafaka (
compromise) kabisa na jamii tofauti zisizozingatia imani yao. Kwao ni suala la muda na fursa katika kukamilisha ajenda yao hiyo kuu.
Wapalestina wanatumiwa na makundi hayo kama
pawn (rehani) tu kufanikisha malengo yao. Hao watu hawajali kama Wapalestina wanaumia au wanaweza kuangamia kabisa. Wao malengo yao ya Uislamu mkali ndiyo muhimu zaidi. Wamejenga na kuimarisha miundombinu yao ya kigaidi/kivita kwenye makazi ya raia huko Ukanda wa Gaza, sehemu za West Bank na sehemu za nchi ya Lebanon. Wamekandamiza kabisa uwezo wa tawala rasmi kufanya kazi kwenye maeneno yao. Kwa namna hiyo wanaipa Israeli uhalali wa kushambulia maeneo ya raia wa Palestina, Lebanon na Iran kwenyewe.
Usishangae kwa nini nchi jirani za kiarabu zinawaogopa wakimbizi wa Kipalestina kuingia nchi zao. Wanaogopa sana kujikuta wameingiza pia au wametengeneza uhalali wa kuwepo hayo makundi yenye RADICAL ISLAM AGENDA yanayojiambatanisha na Wapalestina.
Ni suala gumu lakini lazima liangaliwe kwa undani na mikanganyiko (complexities) yake yote.