Kiongozi wa Iran Ayatollah Khamenei, anafanya kosa kubwa kwa kutangaza wazi mahali na muda wa hotuba yake

ukute ameshakubaliana na Amerika kuwa yeye ndo atolewe kafara๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„.Maana hawa jamaa wanafanya vitu ukitumia tu akili ya darasa la saba B inagoma kuona mantiki ya kumtaarifu adui yako mienendo yako.

Ayatola ataliwa kichwa soon, maana kachoka kukaa kwenye mashimo kama panya.Ngoja wamsafirishe mawinguni๐Ÿค—
 
Mashariki ya kati inawaka moto kwa Sasa...
 
Kama Iran wamemuweka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau kwenye list ya magaidi wanaotakiwa kuliwa kichwa, kwanini nao Israel wasim-target Ayatollah?
Pengine ni kumfanya afikirie namna ambayo ikiwa maamuzi yoyote mabaya kuanzia sasa atakayoyafanya kwa viongozi wa ngazi za juu wa Iran na wewe upo kwenye list yetu.

Ukiangalia na mashambulizi ya siku ya Jumanne ni makubwa na israel mifumo yake ya ulinzi ya anga imeonyesha udhaifu mkubwa sana.

Kwa mawazo yangu nafikiri ni sehemu ya taarifa kuwa hata wewe Netanyahu haupo salama sana.

Tukumbuke pia muanzilshi wa mbinu za kijasusi wa kuua viongozi kwa hapa duniani ni muajemi.
 
Israel lazima atalipiza ila msaada na ulinzi kutoka Marekani,UK lazima uwepo Ili afanikishe hilo.

T14 Armata
Hawezi kushambulia moja kwa moja Iran. Hatoweza.

Na ni kwa sababu kiwango chao cha uchizi ni kama kiwango cha Iran cha uchizi. Na mbaya zaidi na wenzao wana nguvu za kijeshi vilevile.

Si jambo jepesi kumshambulia mshirika mkubwa wa magharibi bila kupepesa macho.
 
We upo huko kazuramimba kigoma kitu pekee unachokiweza kukifanya kwa usahihi kuliko khamenei ni kukamua mafuta ya mawese tu, siku ukiskia Khamenei anakamua mawese ndo umpe ushauri lakini siyo sasa
 
Waisrael hawataki kumuua.
Wakitaka ni dakika moja tu.
Ina maana hujui?

Kama walimuua kiongozi wa Hamas ndani ya Iran tena Hotelini kwake wanashindwaje kumuaa huyu
 
Yeah!.....huenda Israel akalipiza ila katika namna ambayo haitachochea mzozo kuwa mkubwa zaidi.

Ila Iran itakuwa na wakati mgumu Sana kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Israel, hata ADs zao sidhani kama zinaweza kuzuia missiles kama Jericho -3 au ndege za Israel kama F-35/ F-15.

T14 Armata
 
Mkuu hao wayahudi waliopo Iran hawafahamiki?
Kama wanafahamika kwanini wasiondolewe kwa maslahi zaid ya taifa?
 
Watumie tu nuke mchezo uishe.
Dondosha nuke la maana Tel Aviv
 
Mkuu, hisia zako zinaeleweka sana. Kwamba Wapalestina wanaonewa na kunyanyaswa sana inaeleweka. Na inafahamika vizuri kuwa Wapalestina wako Waislamu na Wakristo pia. Na kwamba Wapalestina wengi ni watu wa kawaida wenye malengo ya maendeleo katika mazingira ya kisasaninajulikana.

TATIZO KUBWA ni kuwa suala la kupigania uhuru na haki za Wapalestina LIMETEKWA na vikundi vya Waislamu wenye msimamo mkali wa Jihad (Radical Islamists). Vikundi hivyo kama HAMAS na Hezbollah lengo lao kuu rasmi ni kuiangamiza Israel, Wayahudi wote na watu wote wasio wa imani ya kali Kiislamu. Kisha kuhakikisha Mashariki ya Kati inaongozwa na utawala wa Sharia pekee. Ndio maana IRAN inajihusisha sana na suala la Wapalestina.

Katika hali itakayokushangaza pia ni kuwa, Wayahudi wenye msimamo mkali kama Benjamin Netanyahu na serikali anayoiongoza, wanapenda sana tawala za hao Radical Islamists huko Palestine na Lebanon kwa sababu nao hawataki amani. Hawataki a two state solution. Wanataka vita kwa sababu lengo lao ni kuwafurusha Wapalestina wawaachie ardhi yote ya Palestina, Israel ibakie kuwa taifa moja tu. Kisha waangamize utawala wa Ayatollah wa Iran na miundombinu yake ya Nuclear. Kisha wahakikishe hakuna jirani anayewaletea fyoko Israel. Yote hayo kwa msaada wa watu wa Marekani. Kuna wakati serikali ya Netanyahu iliunga mkono ushindi wa HAMAS dhidi ya PLO katika uchaguzi huko Gaza.

IRAN ina mkono katika harakati zote za kusimika na kuimarisha makundi ya kigaidi yenye ajenda ya Uislamu wa msimamo mkali (RADICAL ISLAM) duniani kote. Hawataki muafaka (compromise) kabisa na jamii tofauti zisizozingatia imani yao. Kwao ni suala la muda na fursa katika kukamilisha ajenda yao hiyo kuu.

Wapalestina wanatumiwa na makundi hayo kama pawn (rehani) tu kufanikisha malengo yao. Hao watu hawajali kama Wapalestina wanaumia au wanaweza kuangamia kabisa. Wao malengo yao ya Uislamu mkali ndiyo muhimu zaidi. Wamejenga na kuimarisha miundombinu yao ya kigaidi/kivita kwenye makazi ya raia huko Ukanda wa Gaza, sehemu za West Bank na sehemu za nchi ya Lebanon. Wamekandamiza kabisa uwezo wa tawala rasmi kufanya kazi kwenye maeneno yao. Kwa namna hiyo wanaipa Israeli uhalali wa kushambulia maeneo ya raia wa Palestina, Lebanon na Iran kwenyewe.

Usishangae kwa nini nchi jirani za kiarabu zinawaogopa wakimbizi wa Kipalestina kuingia nchi zao. Wanaogopa sana kujikuta wameingiza pia au wametengeneza uhalali wa kuwepo hayo makundi yenye RADICAL ISLAM AGENDA yanayojiambatanisha na Wapalestina.

Ni suala gumu lakini lazima liangaliwe kwa undani na mikanganyiko (complexities) yake yote.
 
Tuseme sawa!

Lakini tulizungumzie kwa upande wa pili wa sarafu.

Mashambulizi ya Iran ya juzi yameshambulia base za uwanja wa ndege hizo hizo za Israel.

Swali, Israel ina uhakika gani wa ndege zake kuwa salama kwenye kambi zake dhidi ya Iran?
 
Mkuu hao wayahudi waliopo Iran hawafahamiki?
Kama wanafahamika kwanini wasiondolewe kwa maslahi zaid ya taifa?
Ni sehemu ya raia wake haiwezi kuwaondoa.

Ni kama sisi hatuwezi kuwaondoa wanachi wenye asili ya Tutsi kisa uharamia wa Paul Kagame ijapokuwa wapo ambao wamethibitika walikuwa kwenye madraka makubwa hapa Tz na kukimbilia kwao na kupewa vyeo vikubwa vilevile.
 
Kwahyo unamuonya kwa sababu yeye yuko humu jf? Labda ungesema kwa maoni yako unadhani amekosea apo ntakuelewa sio unamuonya unaanzaje kumuonya mtu hauna contact nae na ujumbe wako hauwez mfikia kwa namna yeyote
 
Ukiona kafa jua wamarekani ndio wamemuua acheni kuwapaisha hao wapuuzi.
 
Sahihi kabisa mkuu, kwa Sasa waisrael wengi wamegeuka kuwa wafuasi wa siasa Kali za mrengo wa kulia.

Zile siasa za wastani za kina Rabbin (Rip), Peres (Rip) kwa kizazi cha Sasa hazina nguvu tena, ila ukweli ni kuwa hawatapata amani ya kudumu na jirani zake kama suala la Palestine lisipopatiwa ufumbuzi wa kudumu, haijalishi nguvu za kijeshi walizonazo wala msaada wanaopewa na Marekani.

zitto junior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ