Kiongozi wa Iran Ayatollah Khamenei, anafanya kosa kubwa kwa kutangaza wazi mahali na muda wa hotuba yake

Hakuna wa kuharibu waisrael , kinachotakiwa palestina wapate uhuru wao wa kutambulika na jerusalem ni mji wao mkuu .


Lebanon , syria na palestine ni vita kwa sababu , huyo jamaa yenu ataka hizo Ardhi mda tu kuunda Great israel.
 
Kama kuna kitu waislamu hawaogopi ni kifo. Huko Gaza umewahi kuona watu wanakimbia nchi yao? wanapigwa wanauliwa lakini wapo hapo hapo.. kufa ukitetea haki yako ni kifo cha kishujaa na hakuna kukimbia na hakuna kujificha
Hwa jamaa hasa jamii ya shia ni wagumu sn, wanavyojiua kweny sikukuu zao kwa kujikata na mapanga.
 
Kuna channel ya Iran
Press tv ni ya Iran
Ye nani na anatofauti gani na waliouwawa au ndo ushabiki maandazi,Israel hajawahi kusita kwenye maamuzi yake only a right time is waited.
Waambie wapige,ile kauli ya Iran kwamba wanataka mashariki ya Kati iwe na amani ya kudumu ina kitu kizito ndani yake,huyo mzee hakosi miaka 70+,kishaishi kamaliza, israel wampige waone nini kitawakumba
 
Press tv ni ya Iran

Waambie wapige,ile kauli ya Iran kwamba wanataka mashariki ya Kati iwe na amani ya kudumu ina kitu kizito ndani yake,huyo mzee hakosi miaka 70+,kishaishi kamaliza, israel wampige waone nini kitawakumba
85 yule aliyeuliwa kweny ajali ya ndege ndiye alikuwa supreme leader ajaye.
 
Ayatollah Khamenei in the building, tumemaliza SWALAT teyari.
Huyo manyaunyau wa israel anaweweseka huko aliko.

Hallelujah!!!
 
Swala ya Ijumaa imeisha na watu wametawanyika tayari hap Tehran. Huyo Israel yuko wapi? Ayatollah kaongoza swala tena uwanjani, tena alitoa taarifa mapema kuwa atatoa hotuba na atakuwepo sehemu hiyo. Na nyuma yake alikuwepo Raisi wa Iran

Vipi Israel imekwama wapi? hiyo si ndio ilikuwa nafasi nzuri ya kuwamaliza kama mlivyokuwa mnajisifia?

Tukiwaambia Israel bila USA ni taifa mfu huwa hamuamini
 
Netanyahu anategemea Air Defence Systems kama Iron Dome na David Sling, Ayatolah anategemea Allah Systems.

Umeona tofauti ya hao Watu wawili mmoja lazima awe mjinga.
 
Mkuu nimependa tahadhari yako ni nzuri na nimecheka sana ulivyosema Netenyau ni mental case jamaa lile jinga sana katika hali ya kawaida linajua Iran iko imara kijeshi na kwa kuwa imewapiga watakua wanajipanga wailipize ila mkuu wao USA anawambia wasubiri kwanza maana ikitokea piga nikupige itakua balaa kubwa...

Kingine umeandika kama Ayatollah tuko nae humu ha ha ha ha .....naamini Iran wameweka ulinzi wote unaotakikana hasa wa Anga na huu wa normall assassnation kwa bullet au bomu sio wajinga jamaa wale wana akili sana.

Kuhusu Vita itakayotokea ni wazi walijiandaa nitawashangaa sana kama watakua hawakujiandaa nikuambie katika watu wajanja kimkakati ( Strategist) basi Waajemi ni No 1, Wanajua ni lini wapi na kwanini afanye uamuzi huu au ule na madhara yake...Sio malofa kivile na ukumbuke wanapambana na US manaa Israel ni mtoto wa mbwa.

Kuhusu Nuclear sijui kama Iran ana Nuclear ( I stand to be corrected) on this, Hivyo wanategemea Long Range Missiles, na Intercontinental Ballistic Missiles ili wapige kule Israel. kwa vyovyote vile kumuua Kiongozi Mkuu wa nchi moja kwa moja ni vita mbaya saanaa..Hata Kule Hamas au Hizbollah walijichanganya sana wakuu wao wakauwawa so Iran kama mkuu wa hizo Proxies zote anachukua tahadhari kubwa katika suala hili.

Mwisho.

Tuombee amani mana hii Dunia hatari za nuclear sasa ziko dhahiri kabisa kutokana na machizi wengi kuwa kwenye Mamlaka makubwa duniani. Mtu kama Netenyau ni chizi kabisa yaani yeye anataka abakie mamlakani kwa gharama zozote hata kama ni kuangamiza dunia.
 
Ayatollah yupo live anatoa hutuba muda huu, haya tunasubiri Israel akafanye yake
Subutu Osegeze ndege zake Iran, kwanza zitapita wapi😄 Jordan, Saud Arabia wanajua wazi kuwacha Air spaces zao ni kutafuta kipigo kutoka Iran. Wameona vipi Israel anacharazwa kama mtoto mdogo wao wakacheze hapo, si ndio wanatafuta balaa
 
Kiongozi kujificha muda wote haileti picha nzuri kwa wafuasi. Baadhi ya wafuasi (akiwemo kiongozi mwenyewe) watatafsiri kama ni woga ama udhaifu.

Vilevile, targeted assassinations huwa hazifanyiki hadharani pekee. Adui akiwa na nia pamoja na taarifa sahihi anaweza kushambulia mtu yeyote mahali popote pale. Kwani kina Nasrallah na Haniyeh waliuawa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara?

Hilo pekee linatosha kuonesha kuwa hata kama kiongozi akijificha, bado usalama wake uko hatarini. Wakati mwingine kuonekana mbele ya public ni salama zaidi kuliko kujificha kwenye handaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…