Simpendi Donald Trump. Ni rais wangu lakini ananichafua sana. Kama Magufuli.
Sipendi kuua watu bila kuwafikisha mahakamani. Mim8 ni mshabiki wa "the rule of law".
Ila, Al-Qaeda waliazimia vita dhidi ya Marekani.
Ubalozi wa Marekani ulipigwa bomu hapo Dar es Salaam yetu.
Watanzanzania waliumia.
Nikisikia Al-Qaeda kauawa, kitu pekee cha kujiuliza ni, huyu Al-Qaeda kweli? Au anasingiziwa tu?
Ikionekana ni Al-Qaeda kweli, hata mimi mtu wa amani ambaye sipendi kuua hata sisimizi katika maisha yangu, siwezi kumhurumia akiuawa na serikali ya Marekani.
Maana leo naweza kumhurumia, wakati kashaweka uuaji katika roho yake, halafu keshi akalipua Dar es Salaam na kuua ndugu zangu.
Nabaki siwezi kupongeza mauaji ya mtu, kwa sababu naamini mtu anaweza kubadilishwa.
Lakini pia, katika ma,ingira ya vita, siwe,i kummtukana mwanajeshi wa Kimarekani, au muongozaji wa jeshi la Marekani, anayesema washenzi wanaotaka kuua watu wauawe tu.
Kwa kweli, nikiamua kuchagua upande, nasema waliotaka kuua watu, wakiwa Wamarekani au Al-Qaeda, wenyewe eamehalalisha kuuawa katika vita.
Sent using
Jamii Forums mobile app