Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kiongozi mpya wa kijeshi wa Madagascar, Kanali Michael Randrianirina, anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa taifa hilo siku ya Ijumaa, Oktoba 17, 2025, licha ya upinzani kutoka kwa Umoja wa Afrika (AU), uliosimamisha uanachama wa nchi hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Andry Rajoelina.
Mapinduzi hayo yalitokana na maandamano ya wananchi waliolalamikia ukosefu wa huduma za msingi kama maji na umeme, ambayo yaligeuka kuwa harakati za kisiasa zilizomalizika kwa jeshi kumng’oa Rais Rajoelina madarakani.
Kanali Randrianirina ametangaza kuwa ataapishwa na Mahakama Kuu ya Katiba kama Rais wa “Msingi Mpya wa Jamhuri ya Madagascar,” akiahidi kuongoza kipindi cha mpito cha hadi Miaka Miwili kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.
Soma Pia: Kiongozi wa Mapinduzi ya Kijeshi Madagascar ajitangaza kuwa Rais
Imeelezwa, Serikali ya mpito itakuwa chini ya usimamizi wa kamati ya kijeshi, huku taasisi zote za serikali zikisitishwa kwa muda, isipokuwa Bunge la Kitaifa.
Kwa upande wake, Rais Rajoelina amekataa kujiuzulu na kusisitiza kuwa bado ndiye kiongozi halali wa nchi, akiwatuhumu wabunge kwa kushirikiana na wanajeshi kupanga njama za mapinduzi.