Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Na sisi wananchi tulioiamini tukaipa kura, sasa tunaamini kuwa imesimama thabiti kulinda maisha yetu. Tupo pamoja na serikali yetu kuwadhibiti wanaotishia maisha yetu LIWALO NA LIWE.

Hivi CCM ilishinda uchaguzi wa mwaka 2010....!?
 
Hapa tunapofikia na swala la Ulimboka si sawa kabisa! Nalaani kupigwa kwake, nalaaani kutekwa kwake! Lakini nalaani ziadi juhudi za kulifanya swala hili ni la kisiasa!! Watu naona kwenye thread kadhaa wanadai wenye silaha ni TISS na Polisi pekeake, hivi huu nao unataka kuitwa ukweli?? wale majambazi nao ni tiss na polisi?

hizi sasa ni siasa za maji taka kwa jambo sensitive kama hili
 
Alafu mnasema eti Tanzania kuna Amani kweli? Haya yetu macho.
 
Najua sisiem watakuwa wa kwanza kulaani.Ombi kwa vyombo vya usalama acheni kutumika vibaya.hilo mnaliweza lakini wahamiaji haramu wizi wa rasilimali za nchi zinakombwa mbele ya macho yenu.

Katika katiba ijayo tuwe na baraza la usalama wa Taifa ambalo halitapatikana kwa kuteuliwa na rais.Liwe na mamlaka ya kumuwajibisha mtu yeyote kuanzia rais kwa kuahatrisha Usalama wetu.

Kuibiwa kwa rasilimali za nchi mchana kweupe kunazua migomo manung`uniko hivyo kuhatarisha usalama wa nchi.
Imefika wakati watanzania tufikilie Tanzania yetu sio mtu au chama.

Matumizi mabaya ya dola yamewapeleka Maraisi wengi Mahakamani.
Washauri wa usalama angalieni Moto na Petrol.Leo watanzania wote wakiandamana kupinga kitendo hiki mtatumia nguvu hivyo kuua Raia.

Kama wakoloni waliwahasi,kuwaua na kuwatendea kila lisilo njem kwa lengo la kulinda masilahi yao lakini walifika sehemu wakarejea kwenye mazungumuzo.

KUTAWALA KWA NGUVU NI GHARAMA SANA CHONDE SERIKALI HAINA PESA
 
Inasikitisha kwa Kweli yaani watawala wamechoka hadi wanajibu hoja kwa kutumia nguvu? tuwaondoe kwa namna yoyote ile.
 
ITV wamethibitisha...

ITV‏@ITVTANZANIA
mwenyekiti wa jumuiya ya madakatari Dr. Stephen Ulimboka ametekwa na kupigwa na watu wasiojulikana na anapelekwa moi
 
serikali yako ya ccm unayoitetea hapa jamvini kila siku ndio inayofanya umafia huu kwa watu wema, wezi waliochota 303bil wameficha uswiss wanawaficha. shame

Kwa hiyo nyie Chadema ndio mnawatetea madaktari? suala hapa sio vyama vya siasa tunaongelea issue ya madaktari wewe unaleta mambo ya Chadema.
 

Sheria itumike. Serikali imefata sheria, kwenye mgogoro inatakiwa uende kwenye vyombo vya sheria, vyombo vya sheria vimesitisha mgomo na vimetowa amri, bado unaleta ukaidi? sasa ataijuwa Serikali ni nini, ingawa yeye kwa gonjwa linalomsumbuwa anaona kuwa hana cha kupoteza, lakini hii itakuwa ni fundisho kwa wengine wajuwe kutumia sheria na kuheshimu mahakama.


Kwa hiyo na hawa waliomteka na kumjeruhi Dkt wamefuata sheria?
 
Sheria itumike. Serikali imefata sheria, kwenye mgogoro inatakiwa uende kwenye vyombo vya sheria, vyombo vya sheria vimesitisha mgomo na vimetowa amri, bado unaleta ukaidi? sasa ataijuwa Serikali ni nini, ingawa yeye kwa gonjwa linalomsumbuwa anaona kuwa hana cha kupoteza, lakini hii itakuwa ni fundisho kwa wengine wajuwe kutumia sheria na kuheshimu mahakama.
wana jf msameheni mtu huyu.
 
Kama habari hii ni ya kweli, Suluhisho la ukweli halitokani na kuteka watu, ni kwa kuwapa madaktari haki yao.

Serikali badala ya kuteka mafisadi inateka wanaodai maslahi yao. Aibu!. Baadhi ya madai ya madaktari ni ya Msingi, wanataka huduma ziboreshwe hospitalini, wanataka wasiwaandikie watu aspirini wakati wanahitaji dawa ya malaria isiyokuwepo.

Haya ni madai ya haki, hayatatatuliwa kwa kuteka watu.

Kuna mtu aliwahi kuuliza hapa Jamvini kwamba usalama wanafanya kazi gani? hii ni moja ya mifano ya kazi zao
 

Sheria itumike. Serikali imefata sheria, kwenye mgogoro inatakiwa uende kwenye vyombo vya sheria, vyombo vya sheria vimesitisha mgomo na vimetowa amri, bado unaleta ukaidi? sasa ataijuwa Serikali ni nini, ingawa yeye kwa gonjwa linalomsumbuwa anaona kuwa hana cha kupoteza, lakini hii itakuwa ni fundisho kwa wengine wajuwe kutumia sheria na kuheshimu mahakama.


Kwa hiyo na hawa waliomteka na kumjeruhi Dkt wamefuata sheria?Ni sheria zipi za Tanzania ziliwahi kusimamiwa kikamilifu bila upendeleo wowote!!!?.
 
Ni mimi naitwa Niambieni Niende. Hii ni mara yangu ya kwanza kujitokeza kwenye hii JF.

Kwa niaba ya wana JF napenda kutoa pole sana kwa wagonjwa wote waliokumbwa, na watakaokumbwa na mgomo huu. Pia pole kwa pande zote mbili zinazopingana yaani Madaktari, Wauguzi na Serikali.

Suala hili haliwahusu tu kama wanao tajwa kama wana CCM au Rais wa Nchi au Wana Chadema, Madaktari na Wagonjwa etc. Bali nyuma ya pazia kuna nguvu za shetani ambaye anachanganya watu wachukiane na kuibuka maovu yote haya.

Hii ni dalili ya mwisho wa Dunia. Zaidi ya hili la mgomo angalieni mfumuko wa wahubiri wa uongo uliopo; amri kumi za Mungu zinavyo vunjwa mfano: kuabudu miungu mingine; sanamu; hakuna heshima kwa wazazi wetu; mauaji; uzinifu umeongezika sana; wizi ni umekuwa sana; ushahidi wa uongo na tamaa.

Imeandikwa 2Petero 3:3-4 "Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho kutakuja na dhihaka za watu wenye kudhihaki wafuatao tamaa za wenyewe ...

Solution: Ni kusameana wenyewe kwa wenyewe na JEMA ZAIDI NI KUMPOKEA YESU NA KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU!

TUACHE MCHEZO NDANI YA UFALME WA GIZA NA TUINGIE UFALME WA MUNGU, NA YOTE YA MIGOMO NA MAKUNDI YATAISHA
 

Na hao madaktari wanaoziiba dawa mahospitali huwaoni?

vip kuhusu wanaoficha dawa msd hadi zinaoza,,,,wanaoihujumu wizara ya afya???wamama walojifungua wanalala chini pale mhimbili(jengo la watoto),,,,sasa mtu ametoka kufanyiwa upasuaji unamlaza chini,,,,jaman does that fair mdau????halafu ngonyani(prof maji)juz kaenda apolloooooooo,,,,,,
 
Back
Top Bottom