namshitu kazeni
Member
- Jan 31, 2012
- 18
- 0
Madaktari please! apparently it is true, at MOI needing CT scan not available BUT his colleagues working out logistics for an outside hospital. very sad
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri...
Wakuu huyu mtu nimekuwa nikimsikia mara nyingi sana kwenye vyombo vya habari,ningefurahi sana kama ningeweza kupewa taarifa zake na cv yake ikiwezekana,kwangu anaonekana kama mtu anayepigania haki fulani ambayo wengi hatujaiujua bado,anakuwa kama Dactari lakini the same time ni mwanaharakati na mtu muhimu sana kwa mapambano yanayoendelea ndani ya taifa letu lililojeruhiwa vibaya!
Ulimboka hawawezi kuwafahamu lakini serikali inawajua. Maana Watekaji walikuwa wakiwasiliana naye kwa kutumia mawasiliano ya simu kwa siku kudhaa. Lakini kwa kuwa serikali ndiyo inayodhibiti hata makampuni ya simu watajitahidi wasijulikane. Watanzania hatuna haja ya kujua majina ya waliohusika lakini tunajua ni mwendelezo wa vitendo vya mauaji vinavyofanywa na serikali. Tawala nyingi kabla ya kuanguka, mara nyingi hufanya mauaji mengi maana humwona kila mtu ni adui. Kwa mambo yanvyokwenda, na jinsi wananchi wengi wanavyozidi kuichukia CCM na serikali, ni lazima tutarajie matendo kama haya kuongezeka katika uwingi na kiwango. Kwa sababu kuna watu huwa wanaamini kuwa unaweza kuzuia kila kitu kwa kutumia nguvu. Mkumbuke hotuba ya JK alipokuwa akijibu kauli ya wapinzani kuwa ni dikteta, alisema, 'mimi dikteta, hamuwajui madikteta? Kama ningekuwa dikteta ungeweza kutamka hata hayo unayotamka na ukaendelea kuwepo? Kama kuna jambo nalaumiwa, hasa ndani ya chama changu ni kuwa mpole mno.' Kwa hiyo si ajabu, wakati mwingine, hata bila amri ya Rais watu wengine wakaamrisha mambo kama haya kwa kisingizio cha mamlaka waliyo nayo kwaajili ya usalama wa Taifa.
Mbona wameharibu sana kufanya hivyo maana sasa hii vita naona inazidi kuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa. Na kwa nini imekuwa ndo njia ya serikali kuziba midomo ya watu wanaokuwa mstari wa mbele kuwa sauti ya wengine? Hivi wanafikiri watazuia watu kugoma kwa vitisho na ubabe kama huo? Ngoja tuone itakuwaje sasa
Usiseme kuwa ni kati ya
serikali au CHADEMA mmojawapo alihusika na kifo cha Wangwe, ukweli ni
kuwa tukubali kuwa au Serikali au ilikuwa ajali ya kawaida.
Nina hakika kama CHADEMA ingekuwa imehusika serikali ya CCM ingefanya
kila iwezekanalo kiitia hatiani CHADEMA ili kuwaonesha wananchi kuwa ni
chama cha mauaji, walishindwa kufanya hivyo kwa kuwa hakukuwa na namna
ya kuihusisha CHADEMA zaidi ya kupiga kelele mitaani.
Na katika hili, kama ni watu tu wasio na uhusiano na serikali ndiyo
waliohusika na uovu huu, masaa 48 hayatapita watakuwa wamekamatwa lakini
hawatakamatwa kwa sababu anayetakiwa kuwakamata ndiye
aliyehusika.
Lazma watu wafe for the greater good so kaa kimya na usikilizie
Usiseme kuwa ni kati ya serikali au CHADEMA mmojawapo alihusika na kifo cha Wangwe, ukweli ni kuwa tukubali kuwa au Serikali au ilikuwa ajali ya kawaida.
Nina hakika kama CHADEMA ingekuwa imehusika serikali ya CCM ingefanya kila iwezekanalo kiitia hatiani CHADEMA ili kuwaonesha wananchi kuwa ni chama cha mauaji, walishindwa kufanya hivyo kwa kuwa hakukuwa na namna ya kuihusisha CHADEMA zaidi ya kupiga kelele mitaani.
Na katika hili, kama ni watu tu wasio na uhusiano na serikali ndiyo waliohusika na uovu huu, masaa 48 hayatapita watakuwa wamekamatwa lakini hawatakamatwa kwa sababu anayetakiwa kuwakamata ndiye aliyehusika.
Ina maana wewe ungekuwa ni miongoni mwa wafanya maamuzi ungefanya maamuzi ya kijinga kama hayo?!
Kuwatisha madaktari mbona jambo dogo sana mkuu wangu!! Hivi unataka kuniambia hufahamu ni kwanini madaktari walikuwa wanaenda kusaini lakini hawafanyi kazi?!
Ina maana hapo inahitaji mtu awe na digrii kufahamu kwamba pamoja na kugoma kwao lakini wanaogopa kupoteza ajira na ndio maana walikuwa wanasaini ili waonekane wamekuja kazini?!
Kuwaatisha ni rahisi tu.....ukiwatimua wale, baada ya mda wote wangerudi kufanya kazi na wala hawakuwa na sababu ya kumteka Ulimboka na kujenga picha ya kijinga kama hiyo!
Sina hakika na ukweli wa habari hii!
Kwa uhusiano alionao na serikali hii, saa sita ya usiku anaenda kufanya 'reconciliation' na 'mtu' wa serikali? Tena peke yake bila viongozi wenzie? Atakuwa wa ajabu basi!
Nimesikia huku mtaani amepatikana eneo la Bunju akiwa hoi, amepigwa haijulinaki, amegongwa haijulikani! Taarifa zilizopo amepelekwa MOI haraka.
Nazidi kufuatilia hili nikipata zaidi nitarudi tena.
Sawa lakini pia umeona hapa chini Ibara ya 30(1) ya Katiba yetu inavyosema
30 -(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
Usiangalie upande mmoja tu wewe!
umeulalia wewe.