Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Yafuatayo yanawezekana kwa harakaharaka;
  1. Yaliyomkuta Ulimboka ni kama yale ya Igunga; ilipata kusdikika kuwa mauaji ya Igunga yalisababishwa na CCM pinzani ndani ya CCM tawala, hivyo bado kuna nafasi ya kuwa huenda yamesababishwa na serikali pinzani ndani ya serikali tawala, ili kuiweka serikali tawala in a hard situation mbele ya jamii...!
  2. Yaliyomkuta Ulimboka huenda yamesababishwa yamesababishwa na serikali baada ya kumuona kama threat katika utawala wao...! Lakini kama ndio hivi, basi binafsi nazidi kudhibitisha jinsi walivyodhaifu katika mikakati, maana hatua ya kumteka mtu na kumuachia akiwa hai, huku wamekwisha muumiza kiasi hiki ni uzembe wa kutupwa...!
  3. Huenda yaliyomkuta Ulimboka ni kama ya watu wengine wengi waliiopata kutekwa na kupigwa na hata kuuawa...! Hii ni kwa sababu naye ni binadamu, na anaweza akawa na vishawishi vya kuweza kumfanya afanyiwe hivyo...!
  4. nk
 
Ulimboka nae hasipate huduma kwa siku tatu kama wenzie wasio madaktari wanavyokosa huduma na kuteseka kwa matendo yake ya kuwashawishi madr wagome na wananchi wakose huduma

kwa nini asipewe huduma na wennzake? hiyo lazima first class. asipopata pale wengi wana private hospitals, so he is in good hands. Naomba Mungu apone haraka.
 
This is so sickening! Hii inaonesha kiwango cha kufikiri cha serikali hii!
 
SERIKALI IPI WEWE zomba?? kesi ya kunguru ukampe mwewe uliona wapi?? halafu nakuchukia wewe na wenzako wote mnaosuport hiki chama cha machangudoa!

Hizo ni chuki binafsi, mimi hazinistui kwa sababu najuwa chuki zenu ni kuwa tu pale wetu anapoweza kufanya vizuri kuliko wenu, huwa hampendi na mnaona vipi huyu katuzidi? hiyo ni roho ya kichawi.
 
Member Array

Join Date : 24th June 2012
Posts : 28
Rep Power : 306
Likes Received 2


Pole Pole dada... semea nafsi yako na waliokutuma!! wengi mnawaua na mtawaua kutokana na upofu mliopatilizwa ili muendelee kutawala.... Mnasahau kuwa Watanzania waleo wameamka wanajua kinachoendelea....

kabla ya kuja kubwabwaja hapa ebu jiulize...Wangapi wamekufa kwa kukosa ambullance? wangapi wamekufa kutokana na umasikini ufukara wakusababishiwa na Serikali ya CCM wakati nchi yetu imesheheni rasilimali kibao? wangapi walifariki kwenye mabomu ya mbagala na gongolamboto eti kwa sababu tu mlikuwa mnaficha siri za ufisadi uliotumika kununulia silaha!?? wangapi mmewaua migodini eti mnatetea wawekezaji?

Madaktari wasihusishwe na vifo vya watanzania kwa njia yoyote kwani lengo lao ni kutaka serikali iboreshe huduma za afya kwa kununua vitendea kazi za kisasa, wagonjwa kupatiwa malazi stahiki... ona akinamama wanavyo lala sakafuni, wengi wanafariki kwa kupata maambukizi wakiwa mahospitalini....

Inakeraaa..... grrrrr.....Mods tuachieni kidogo tu tuwanyooshe hawa watumwa wanafki waathirika wa bongo zao ....

....Namuombea Dr Ulimboka apone haraka Inshaallah...
 
Duh, sasa imegeuka kwamba halikuwa Leaders club na sio nyumbani! Kweli hata Simbachawene hakufumaniwa!!!?

Angalia habari hasa Clouds TV amehojiwa mwenyewe Dr Ulimboka ndiye kasema alikuwa ametoka na jamaa zake. Kova hajaunda stori tofauti na ya Dr mwenyewe.
 

Hivi unajua ni idadi ipi ya watu ambao wameshakufa hadi sasa kwa kukosa huduma ambazo zilipaswa zitolewe na serikali? Ni watu wengi sana waliofariki, ndugu zangu wakiwemo, waliokufa kwa kukosa huduma bora za afya. Wengine wamekufa wakiwa kwenye foleni za hospitali wakisubiri dawa! Wakati viongozi wanaishi kwenye viyoyozi na kuishi maisha ya anasa. Watu kama wewe mnanitia uchungu sana maana hata hamjijui kuwa hata nyie hali zenu ni mbaya. Mnatakiwa kuonewa huruma tu!!
 
Kama mzazi unaweza kufika sehemu ukasema bora uzae ndondocha kuliko kuzaa watu kama Zomba!!!!
 
Pole sana kwa Dr. Ulimboka.Naona jinsi spinning doctors wanavyoi'spin' hii Ishu.Maybe walifikiri wameshakuua kumbe umepoteza fahamu.Hata ukifa leo umeacha alama isiyoweza kufutika milele.Kwangu mimi wewe ni shujaa uliyejitolea maisha yako kwa ajili ya wengine.Umeonyesha njia kwa kuthubutu kufanya kile ambacho wengi wanakiogopa.Sio kwamba hukujua kuwa kuna watu wenye nguvu wanakuchukia.Ulijua sana na wala hukuwa na haja ya kutembea na ulinzi kwa kuwa unaamini upo upande wa haki.Nakuombea kwa Mungu upone kwa nguvu zake na kwa mapenzi yake.Yeye ndiye atoaye na achukuaye uhai.Kama akiamua kukuchukua ni kwa mapenzi yake.Na kama yeye hajaamua kukuchukua hata binadamu afanye nini hatoweza.Get well soon Dr.Ulimboka, the true son of Tanzania.
 
Mhh! hatushabikii watu watekwe na kuumizwa lakini pia sishabikii wananchi wa kawaida kukosa huduma za matibu. migomo ya mara kwa mara ya watu wa afya inaweza kuamsha hasira na chuki za wagonjwa, ndugu na jamaa za wagonjwa wenye maumivi ama kufariki na kuifanya kazi ya kudai haki zao kwa njia ya migomo iwe ngumu (confounding). Kazi ya kujua kama watekaji ni dola au wananchi itakuwa ngumu. Madakitari itabidi tutoke mitaani mkaishi barracks kama FFU ili kuepuka hasira za wanaopoteza ndugu na jamaa kwa migomo. Tunaodhulumiwa na mfumo tuko wengi sio madaktari tu hata daktari hatafurahi akisikia police wote, mabenki, wazibua mitaro, wazoa takataka, wauza matunda na mchele wamegoma. Hapo ndipo utakapojulikana umuhimu wa kila fani. Suluhisho si kuumizana walalahoi wenyewe kwa wenyewe kama mnavyofanya madaktari wetu bali tuunde tahariri square yetu itakayowahusisha hata waokota chupa za plastic kwenye mitaro ya maji machafu
 
Inatia uchungu sana kwa kweli. Ina saidia nini kumuumiza Dr. Ulimboka kiasi hiki kwa nia ya kuwatisha madaktari wasigome. Hao waliofanya huo unyama ni zaidi ya wanyama! Sasa madaktari na wagome kabisa! Aghaaaa!
 

Mkuu Michael P Aweda, hii ndo serikali tunayosema inawajali wananchi wake. Sijathibitisha kuhusu serikali kuhusika ila kwa vyovyote vile Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haiwezi kukwepa lawama hizi!!!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa Dr. Ulimboka.Naona jinsi spinning doctors wanavyoi'spin' hii Ishu.Maybe walifikiri wameshakuua kumbe umepoteza fahamu.Hata ukifa leo umeacha alama isiyoweza kufutika milele.Kwangu mimi wewe ni shujaa uliyejitolea maisha yako kwa ajili ya wengine.Umeonyesha njia kwa kuthubutu kufanya kile ambacho wengi wanakiogopa.Sio kwamba hukujua kuwa kuna watu wenye nguvu wanakuchukia.Ulijua sana na wala hukuwa na haja ya kutembea na ulinzi kwa kuwa unaamini upo upande wa haki.Nakuombea kwa Mungu upone kwa nguvu zake na kwa mapenzi yake.Yeye ndiye atoaye na achukuaye uhai.Kama akiamua kukuchukua ni kwa mapenzi yake.Na kama yeye hajaamua kukuchukua hata binadamu afanye nini hatoweza.Get well soon Dr.Ulimboka, the true son of Tanzania.
 
Nakuwa mgumu wa kuamini kama serikali yaweza kufanya this poor operation kwa Ulimboka, hakika tutajua ukweli.
 
Hii habari imetolewa BBC Swahili jioni hii, inasemekana Dr Ulimboka kavunjwa meno, wameng'oa kucha (painful!). Sijui Serikali na hasa Waziri mkuu atasema nini kesho? Ni maneno ghani yatatolewa ili wananchi waamini serikali ya ccm sio wauaji? Ni lugha gani atatumia Pinda itakayowashawishi watanzania kuwa serikali ya CCM sio mafia? Ukweli nimehuzunishwa sana sana sana na hili tukio.

Kama kweli mungu yupo na kama anasikiliza vilio vya wanyonge basi naamini ataonesha utukufu wake nchi hii. Wanyonge wa nchi hii wanaangamia, hawana silaha, hawana polisi, hawana magari ya washawasha na sasa wanateswa na wenye nguvu. Mungu tunusuru.
 

mimi mwenyewe nakua na mawazo km yako,wajanja wanaweza wakatumia hii loophole kuitia serikali kitanzini,ufanyike uchunguzi huru nawa haki kabisa ili kuiondoa hii sintofahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…