Sasa uchokozi umefikia pabaya na hii sasa ni vita!!
Taarifa iliyonifikia hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.
Taarifa zimekwisha fikishwa polisi na sehemu zingine kwa ajili ya ufuatiliaji. (source chanzo cha kuaminika).
UPDATE:
Inaelekea waliomteka si watu wema kabisa, Dr. Ulimboka kaokotwa sehemu akiwa katika hali mbaya sana!
Tutaendelea kutoa updates kadiri muda unavyoruhusu.
PICHANI: Dkt. Ulimboka akiwa katika hali mbaya mara baada ya kuokotwa akiwa hajitambui.
Ulimboka alitekwa jana usiku mida ya saa 6 usiku baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abeid na alitekwa na watu wawili waliokuwa na silaha. Kufuatia hali hii wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili nao wamegoma na mgomo huenda ukawa mkubwa zaidi!