Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

hivi madaktari huwa hawavamiwi na majambazi? madaktari hawaibiwi? je jambazi anachagua huyu daktari huyu siye????
HAYA WASOMI WETU......MMEAMUA KUTUAMINISHA KUWA AMETENDEWA UBAYA NA ""A"" NA SIO ""B""
 
Hapa tunapofikia na swala la Ulimboka si sawa kabisa! Nalaani kupigwa kwake, nalaaani kutekwa kwake! Lakini nalaani ziadi juhudi za kulifanya swala hili ni la kisiasa!! Watu naona kwenye thread kadhaa wanadai wenye silaha ni TISS na Polisi pekeake, hivi huu nao unataka kuitwa ukweli?? wale majambazi nao ni tiss na polisi?

hizi sasa ni siasa za maji taka kwa jambo sensitive kama hili

Kumbe wewe huijui vizuri bongoooo.....Majambazi wengi ni polisi au walikuwa mapolisi au wanashirikiana kwa UKARUBUUUU na polisi....uliza kaka
 
swala kupigwa kwa dokta ulimboka ni kweli sikizeni cluds sasa
 
WaTanzania kote nchini sasa tunasema tena kwa sauti kwamba waliomteka Dr Ulimboka WAMWACHIE MARA MOJA na akiwa hana jeraha lolote lile!

Hili lisipotekelezwa kwa haraka basi huenda kukafuatia mgomo mkubwa zaidi wa sehemu kubwa zaidi ya wananchi kila kona ya nchi wakati wowote tangu sasa!

Jamani wengine mbona wagumu wa kuelewa? Mbona mleta thread kasema ameokotwa na watu wa Legal Human Rights Center kule Mabwepande, kalazwa MOI. Wamwachie kina nani sasa?
 
Ukishindwa kuelewa kauli rahisi na ya wazi km hiyo uanweza kuelewa kauli tata? Alichomaanisha ni kuwa Wamejitahidi kuwadekeza kwa kadri ya uwezo wao lakini inavyoonekana wanayonena si yaliyo moyoni mwao, na yaliyo moyoni mwao hawayaneni kwa vinywa vyao! Km shida kila fani katika utumishi wa umma zimo, na kuwa waganga hawawezi kuishi in isolation na wakawa salama...wanawahitaji wengine wa fani tofauti...na hao pia wanastahili ahueni katika kutimiza majukumu yao, kwa kugawana equitably keki ya taifa.
Huu ni upumbavu wa viongozi wetu...wanataka sana madaktari waonekane ni watu wabaya kwa kutaka maslahi zaidi wakati kuna issue muhimu kabisa ya ubora wa huduma za afya inayowakimbiza wenyewe kila siku India. Kwenye katiba mpya ni lazima watu tuliangalie hili...kama kiongozi akitaka kutibiwa nje ni lazima atumie hela zake mweyewe...hii itasaidia kuwarudisha kwenye reality hawa mamburukenge....
 
Hila la Dr. Ulimboka kuokotwa na wanaharakati wa LHRC likoje? Nilitegemea wawe madaktari wenzake au labda wanafamilia wake
 
Sasa hii serikali dhaifu ndio hapo inapokosea yaani wamemteka, wakampiga ili wamuue ila mungu bado anampigania na ninauhakika atahudumiwa na wenzie kwa hali ya juu...
 
Guys, I feel so ashamed of this government! How comes they do this to our people? is this true or fiction?

What the hell is not happening? can this be fair, how comes the MPs who spend so much time politicing around are earning so much with huge incentives as compared to our life savers who are put to rsik without good working environment?

Can this be the solution to such sound grienvances? We are coming down the line! If the government push us so much to the wall we will push back then they will know that we fear no guns neither do we frea ht armed forces!
 
Napita,ngojni subirie breaking news nyingine ya kunihakikishia hilo tukio before i comment.
 
Unawaita madaktari.....halafu unawaita Vilaza...
wewe ndo kilaza........kama vipi ungesoma MD basi kama una kichwa!!
mambwiga wengine bana!!!
We punguani nlichosoma mimi kinahitaji akili mara kumi ya akili inayohitajika huko medicine(what i earn in a month ..hao Madoctor inawihataji 1 year and a Half kufikia)...

Kuwa Doctor hakukufanyi usiwe kilaza ..hawa madoctor si wanawafanyia watu opresheni za kichwa wakati walitakiwa wafanye opresheni za miguu ?...

Pia katika mgomo uliopita waliwakejeli wananchi badala ya kuwahudumia wakakata roho mbele yao! sasa hawa madoctor kama sio vilaza ni nani ? for your record ,na wewe ni kilazaaaaaaaaaaaa
 
Atawafahamu ?, maana hizi ni proffesion za watu !! wanaweza kuwa ni watu ambao tangu azaliwe hajawahi kukutana na hatakutana nao maishani, katika issue kama hizo watu wanatolewa nje ya nchi au wanafunika nyuso zao.

Ulimboka hawawezi kuwafahamu lakini serikali inawajua. Maana Watekaji walikuwa wakiwasiliana naye kwa kutumia mawasiliano ya simu kwa siku kudhaa.

Lakini kwa kuwa serikali ndiyo inayodhibiti hata makampuni ya simu watajitahidi wasijulikane. Watanzania hatuna haja ya kujua majina ya waliohusika lakini tunajua ni mwendelezo wa vitendo vya mauaji vinavyofanywa na serikali. Tawala nyingi kabla ya kuanguka, mara nyingi hufanya mauaji mengi maana humwona kila mtu ni adui.

Kwa mambo yanvyokwenda, na jinsi wananchi wengi wanavyozidi kuichukia CCM na serikali, ni lazima tutarajie matendo kama haya kuongezeka katika uwingi na kiwango. Kwa sababu kuna watu huwa wanaamini kuwa unaweza kuzuia kila kitu kwa kutumia nguvu. Mkumbuke hotuba ya JK alipokuwa akijibu kauli ya wapinzani kuwa ni dikteta, alisema, 'mimi dikteta, hamuwajui madikteta?

Kama ningekuwa dikteta ungeweza kutamka hata hayo unayotamka na ukaendelea kuwepo? Kama kuna jambo nalaumiwa, hasa ndani ya chama changu ni kuwa mpole mno.' Kwa hiyo si ajabu, wakati mwingine, hata bila amri ya Rais watu wengine wakaamrisha mambo kama haya kwa kisingizio cha mamlaka waliyo nayo kwaajili ya usalama wa Taifa.
 
hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwa sababu hapumui vizuri,
 
Jamani huu ni uuaji!ni habari za kusikitisha sana, madaktari msirudi nyuma!endeleeni na msimamo wenu
 
Hii sasa ni hatari sana, tumaelekea wapi?:A S confused:
 
Mbona wameharibu sana kufanya hivyo maana sasa hii vita naona inazidi kuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa. Na kwa nini imekuwa ndo njia ya serikali kuziba midomo ya watu wanaokuwa mstari wa mbele kuwa sauti ya wengine? Hivi wanafikiri watazuia watu kugoma kwa vitisho na ubabe kama huo? Ngoja tuone itakuwaje sasa
 
Serikali inapochoka kushughulikia matatizo ya wananchi wake na ikatukuza ufisadi, humuoana kila mwananchi/raia mpenda haki na ukweli kuwa ni adui mkubwa, hasa anapojitokeza kudai haki na kueleza ukweli. Madai ya madaktari ni mapana na yanagusa ustawi wa jamii. kwa mfano wanaposema vitendea kazi havipo, je ni kosa? mbona wao matumbo yakiunguruma tu, tunawasikia INdia. Hoja kwamba serikali haina pesa ni uongo wa mchana kweupe. Tujiulize serikali isiyo na pesa inakuaje na mabilioni ya pesa benki za nje kama uswisi n.k, serikali isiyo na pesa inakuaje ripoti ya CAG ionyeshe mabilioni ya pesa yakiwa yamepotea/yameliwa na taasisi moja tu/mtu mmoja,serikali isiyo na pesa inakuaje viongozi wake kila kukicha kiguru na njia kwenda ng`ambo kwa kisingizio cha kuona utendaji kazi wa balozi zetu,ooh mara kutafuta wafadhili wa bajeti, mara kutafuta wawekezaji, mara marafiki(sijui wa kike au kiume), mara kutangaza utalii. hiyo ni serikali ambayo viongozi wake wamechoka kufikiri, na viongozi wanaofikiri wapo uraiani na hao ndio wapambanaji wakweli. sas kazi ni moja tu, nayo ni kung`oa magugu yote ya CCM

serikali yetu imejaa majambazi ndo maana hata kule kibondo kwenye kura za maoni walipitisha jambaz ambaye alikuwa kaua watu wengi. Na kama mnabisha Jaribu kuangalia matukio kuanzia sasa hivi. Yaan nimejikuta nimeinGiza gari mtaron kwa mshangao. Every beginning has an ending, you might be leaving as in paradise but end up leaving as chokoraa. Jk time will tell, I swear in the name of god you have very disappointing ending. Wait and see
 
We punguani nlichosoma mimi kinahitaji akili mara kumi ya akili inayohitajika huko medicine(what i earn in a month ..hao Madoctor inawihataji 1 year and a Half kufikia)...Kuwa Doctor hakukufanyi usiwe kilaza ..hawa madoctor si wanawafanyia watu opresheni za kichwa wakati walitakiwa wafanye opresheni za miguu ?...pia katika mgomo uliopita waliwakejeli wananchi badala ya kuwahudumia wakakata roho mbele yao! sasa hawa madoctor kama sio vilaza ni nani ? for your record ,na wewe ni kilazaaaaaaaaaaaa

Mapato ya mtu hayategemei intelligency ya mtu bali hutegemea mbinu na motives za mtu.
 
Back
Top Bottom