Kiongozi wa umma kumiliki vitu vya anasa huku kundi la unaowatawala wakipitia dhiki haijengi taswira nzuri

Daaah kusema kweli kwenye hilo suala la saa ya Rais Samia kama ina gharama hiyo na aliinunua kwa fedha za uma litakuwa jambo la kipuuzi saba! Ila kama ni hela yake halali mi sina neno! Ila viongozi wa kiafrika wengi ni malimbukeni sana!
 
Kawaida ya nyumbu kumtetea mmiliki wao. Kama ni tajiri wa kuzaliwa angeng'ang'ania uenyekiti?
Mjinga hufikiri kila kiongozi anatafuta kuiba. Mbowe angeweza kuishi maisha mazuri juu ya miti bila kupoteza muda wake na kudhalilishwa na siasa chafu za Tanzania. Ana mahoteli kibao na majumba makubwa ya kifahari. Anachofanya Mbowe ni kuplay his party in Tanzanian politics and development, huyu mtu sio maskini kama wanasiasa wa CCM wanaopiga magoti kuomba kura ili wapate kula na kuishi!
 
Onesha Hotel ya Mbowe? Nyinyi nyumbu mnapenda kusifiana ujinga ujinga! Nitajie Hotel moja hapa Dar!?
 
Onesha Hotel ya Mbowe? Nyinyi nyumbu mnapenda kusifiana ujinga ujinga! Nitajie Hotel moja hapa Dar!?
Kwa kifupi tu na uone jinsi Mbowe alivyodhulimiwa na kupoteza mabilioni kwa kuwa kiongozi wa upinzani, sitaji zile chains of hotels, haka ni ka-hotel kadogo tu ka huko migombani kwa Mbowe:
Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.
 
Jamaa ni tajiri haswa tuache utani
 
We lazima utakuwa wa jinsia ya kike, mana nyie ndo huwa mnaoneana wivu kikekike
 
Kiongozi huyu kufanya anasa za kiwango hicho inatutafakarisha kuhusu rasilimali zetu anazomilikishwa mwarabu, je, hizo ni miongoni mwa zawadi anazopewa ili kulainisha madili?
Yaani mpaka mseme
 
Nimepita mitandaoni, hata Biden hana saa inafikia hio gharama.

Inasikitisha kwa kweli.
 
Taswira nzuri hujengwa na KATIBA... Watanzania wa sasa wengi hawajui umuhimu wa KATIBA!
Labda tusubirie vizazi vinavyokuja pengine wakawa na akili za mabadiliko!
 
Hakuna mtawala wa kiafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzak
 
Siku wewe nyumbu ukipata akili njoo ufute hii comment yako. Hakunaga mfanyabiashara anayefanya kazi za hasara. Siasa imempa Mbowe pesa nyingi sana. Hela za msaada kutoka Ulaya kwa ajili ya chama alifungulia kampuni yake binafsi ya magazeti ambayo wanunuzi wakuu ni nyie nyumbu. Mwaka 2010 alikikodishia chama chenu magari ya kampeni na kujilipa mamilioni kupitia ruzuku baadae. Hapo sijazungumzia mishahara ya ubunge na mafao. Na bado asali anayolambishwa. Mbowe hawezi kuacha siasa kwasababu inampa utajiri, sifa na heshima kwenye jamii. Halafu elewa pesa haijawahi tosha kwa mfanyabiashara yeyote akiwemo Mbowe. Hadi leo kina Bill Gates wanazisaka pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…