Kiongozi wa umma kumiliki vitu vya anasa huku kundi la unaowatawala wakipitia dhiki haijengi taswira nzuri

Ukweli ni kwamba Hatutomsahau aliempokea na Hatutomsahau Aliepita.

Yani Wote wawili hatutowasahau katika hili taifa.

RECORD zao ni za viwango vya Juu, Mwenye Mazuri alifanya Mazuri PRO MAX na tulienae anavurunda ki PRO MAX 16 (ambayl hata haijatoka)
 
Kha!
wacha wamsagie kunguni maana doh naye kazidi sasa
 
Kama amepata kihalali?
 
Mkuu wahenga walisema angalia ulipojikwaa; si ulipoangukia. Watu wengi hupenda maisha ya anasa bila kiasi fursa inapokuwepo. Hii ni kanuni ya msingi kuhusu binadamu - duniani kote. Nchi makini wameweza kuidhibiti hali hii kwa sheria, mifumo na taasisi imara sana.

Viongozi wanapata madaraka toka kwa wananchi. Hivyo, wanapokuwa na vitu vya anasa na wanapoishi maisha ya anasa sana, tunachopaswa kuuliza ni kama kuna sheria walizovunja? Fedha wanazotumia kibinafsi ni halali yao au wanazipata na kuzitumia kijinai? Tumefanya na tunafanya nini kuhakikisha wanatuongoza vyema na kutumia rasilimali/hazina ya taifa kwa usahihi?

Kama tumewapa “blank cheque” na “guarantee” ya kujimilikisha uongozi na rasilimali za taifa kibinafsi kwa kadiri wanavyotaka au kujisikia basi HATUNA sababu ya kulalamika.

Harakati za kudai katiba mpya makini inayoweka uwiano sahihi wa madaraka ya Rais, mihimili ya dola na taasisi imara za umma; sheria na kanuni zinazohakikisha uchaguzi huru na wa haki; na nguvu ya wananchi kuwajibisha wawakilishi wao na viongozi wasiotenda kazi kwa umakini. Ndiyo mambo muhimu ya kukamilisha sasa. Vinginevyo, ni kuendelea kushuhudia mabilioni yakitumika kuneemesha maisha ya viongozi, familia zao na machawa wao.
 
Inastaajabisha kwa kweli hebu ona gari zima ni dhahabu

Wangeliuza hili huyu mzazi angekuwa hata na ka ist

Haya matatizo ya kidunia nayo.

 
Huwa tunaambiwa kila kitu mnaagiza kutoka nje, istohe wengi hapa huwa wanasema, 'mlikuwa hamjui chochote kila kabla ya Mzungu' Elimu, Hesabu n.k n.k

Ati mpaka nguo na viwalo tumefundishwa na kuvalishwa na kutumia na Wazungu.

Sasa tunavaa, ati imekuwa anasa.

Tunafanya mengi kwa waliotufundisha na hadi wametoa vyeti vya kufaulu n.k, lakini bado wanasema haya tunayoyafanya sio sawa.

Sasa huo ustaarabu wanaofundisha ndio naona una kasoro.

Ikiwa masuala mengi wanayosema huwa yanatokea Ulaya na nchi zingine, kwanini wanatusakama kwa nongwa kwa mambo hayo hayo.

Sasa tukisema tuache ya kwao tuyafanye tunayoyajua sisi, wanasema, mmefunga nchi-nchi na mipaka walizobuni wao?

Tufanyeje?

Tule kwa Urefu wa kamba za mbuzi zetu tu.
 
Inastaajabisha kwa kweli hebu ona gari zima ni dhahabu

Wangeliuza hili huyu mzazi angekuwa hata na ka ist

Haya matatizo ya kidunia nayo.

Ok. Sawa. Kumbe hatuna tofauti na UK?

Kule nako viongozi wanaishi kwenye utajiri wa kufuru wakati wananchi wa kawaida wametopea kwenye ufukara wa kutisha!

Basi Sawa mkuu. Hatutawalaumu tena mabosi wa CCM kwa kutufukarisha huku wao wakiishi kianasa. Kumbe ndio dunia ilivyo.
 
"Acha wacheke kwa muda tu,watalia sana kilio kisicho na mwisho."
 
Ni kwamba tumejifunza tumefaulu, tena kwa elimu yao....

Ati....Kuvaa nguo, viwalo, viatu nasikia mpaka kula...mpaka kulalama lalama(critisizing) kutoka kwa Nchi zilizoendelea.

Sasa, tumestaarabika! Nchi imefunguliwa na tunafanya Diplomasia ya uchumi(ndicho kilichotokea)....tatizo lipo wapi?



Nimezingatia haya katika kujibu malalamiko yake.
Mbona hizi zote ni sifa zenu waafrika
Na haya
Kitu pekee kikubwa nilicho vuna toka elimu ya Tanzania ni kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Kiukweli elimu yetu ya Tanzania ni useless hakuna kitu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…