Kiongozi wa Upinzani Msumbiji, Venancio Mondlane anakabiliwa na Mashtaka Matano ya Jinai

Kiongozi wa Upinzani Msumbiji, Venancio Mondlane anakabiliwa na Mashtaka Matano ya Jinai

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Nchini Mozambique, mwanasiasa wa upinzani Venancio Mondlane amefunguliwa mashtaka matano ya jinai, likiwemo la uchochezi wa ugaidi, kufuatia machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2024. Mondlane, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa chama tawala cha FRELIMO, anadai kuwa anashtakiwa kwa sababu ya kufichua kile anachokiita "wizi mkubwa wa kura" katika uchaguzi wa Oktoba 9, 2024, uliompa ushindi Rais Daniel Chapo

Baada ya uchaguzi huo, Mondlane aliongoza maandamano yaliyodumu kwa miezi kadhaa na kuenea nchi nzima. Ghasia hizo zilisababisha vifo vya watu takribani 400 na kujeruhi wengine 600, ambapo polisi wanadaiwa kuhusika moja kwa moja. Kufuatia hayo, maafisa polisi 31 sasa wanakabiliwa na kesi mahakamani kwa kuhusika na ukandamizaji huo

Mondlane amesema anaingia mahakamani akiwa na dhamira safi na timu ya wanasheria wa kimataifa. Amemtuhumu Rais Chapo kwa kuvunja makubaliano ya amani waliyosaini mwezi Machi, yaliyowasha matumaini ya maridhiano ya kitaifa na mageuzi mapya, ikiwemo sheria mpya ya maridhiano iliyopitishwa Aprili. Hata hivyo, hali ya kisiasa imeanza tena kuwa ya wasiwasi, huku demokrasia ya Mozambique ikitetereka

====

In Mozambique, opposition politician Venancio Mondlane has been hit with five criminal charges, including instigation to terrorism, following last year’s post-election unrest

Mondlane, a fierce critic of the ruling FRELIMO party, says he’s being targeted for exposing what he calls "massive electoral fraud" during the October 9 election. That vote was won by President Daniel Chapo

After the election, Mondlane led months of protests that spread across the country. The violence left at least 400 dead and 600 injured, allegedly at the hands of police

Now, 31 officers are facing trial for their roles

Mondlane says he’s entering court with a clear conscience and an international legal team. He accuses the Chapo government of betraying a peace deal they both signed in March

That agreement had sparked hope, leading to new reforms and a national reconciliation law passed in April.

But tensions are rising again, and Mozambique’s fragile democracy hangs in the balance



Source: African news​
 
They don't want peace they want problems......sasa kama walishasaini makubaliano ya amani why ampeleke mwenzie mahakamani......Africa ni shithole.
 
Serikali ya FRELIMO wanaiga ya serikali ya chama dola kongwe ya Tanzania kutengeza kesi mchongo ya uhaini kwa Tundu Lissu, kule (Msumbiji) siyo Tanzania. Watu wanaweza kuingia barabarani wakati wowote kumtetea kiongozi wao Venancio Mondlane

TOKA MAKTABA:

 
Mwamba Venancio Mondlane

22 July 2025
VENÂNCIO MONDLANE REACTS TO THE ACCUSATIONS FORMALIZED BY THE PGR

View: https://m.youtube.com/watch?v=totoWnJWX30
Mondlane is charged with five crimes: advocating a crime, inciting collective disobedience, publicly instigating a crime, instigating terrorism, and inciting terrorism...
 
Haikuitwa bara la giza kimakosa na kwa bahati mbaya kuna watu wajinga (ignorant) wanafikiri Afrika kuna demokrasia kwani wenyewe kuwa na katiba inayosema nchi itakuwa ni ya mfumo wa vyama vingi kwao ndio demokrasia.

Hawajui kwamba hiyo ni kipengele kidogo sana katika kutafsiri mfumo wa kidemokrasia.

Kiuhalisia Afrika tuna mfumo wa kiimla tu hiyo ya katiba kusema nchi itakuwa ya mfumo wa vyama vingi ni chambo tu ya kutafuta uhalali wa kupewa misaada na mikopo toka kwa mataifa ya magharibi.
 
Back
Top Bottom